Baada ya kuona mafuta yemepanda bei nakuletea njia mbadala

MartinCoder

JF-Expert Member
Feb 20, 2018
700
629
Njia mbadala za mafuta ya kupikia kwa afya

Mafuta ya kula ni kiungo muhimu sana kwenye mapishi yetu ya kila siku. Baadhi yetu hatuwezi kuandaa chakula bila kutumia mafuta kabisa. Lakini kila mtu anafahamu madhara ya mafuta, hasa ukitumia kwa wingi na kutumia mafuta yasiyo na kiwango bora - ambayo hupatikana kwa wingi na bei nafuu zaidi. Je kuna njia gani mbadala za kupunguza matumizi haya ya mafuta? Leo hii tunaangalia njia mbadala za mafuta ya kula ili kulinda afya zetu na wale tuwapendao.

Mara nyingi kutokana na pilika za maisha, huwa hatujali tunakula nini na kila tunachonunua vina viambato gani. Si kila mtu ana muda na kasumba ya kuchunguza mafuta au bidhaa anazonunua - wengi tunaangalia gharama na upatikanaji. Si kila mchuuzi anajali anachowauzia wateja wake, kwa hiyo afya zetu ziko mikononi kwa wale wanaotupa huduma. Je ungependa kuwa makini zaidi na unachokula?

"We are what we eat" - wamelonga wenye lugha yao.

Ili kuwa makini na afya zetu, ni vizuri kutafuta njia mbadala za kuondokana na kasumba ya kulundika mafuta hatarishi kwenye chakula. Hii haina maana kuondoka uhondo wa chakula, hapana. Hapa tunatafuta njia mbadala za kukuwezesha wewe kupika chakula chako kwa kuzingatia kanuni za afya yako na wale uwapendao.

Tuzungumzie juu ya njia mbadala za mafuta ya kula. Unaweza kujaribu njia moja au zaidi na kubaki na zile zinazoweza kuwa rahisi na bora kwako, lakini ni vizuri ukajaribu vitu tofauti ili kuongeza utamu zaidi.

Tumia nazi
Nazi ni kiungo mahsusi kwa jamii ya watu wa pwani na ni kiungo muhimu sana tunachotumia kwenye mapishi kila siku. Kuna watu hawawezi kupika bila nazi - wali nazi au maharage ya kiporo yaliyopikwa na nazi - hakosi mtu kwenye maakuli. Nazi inaweza kutumika kwa aina tofauti za mapishi. Unaweza kutumia kama tui la nazi au unaweza kutumia mafuta yake kwa kupikia. Uzuri wa nazi ni kuwa unaweza kupikia vyakula tofauti, kuanzia wali hadi mboga mbalimbali. Zaidi ya yote nazi ni kiungo mbadala sababu ni bidhaa asili haina kemikali za viwandani. Chakula chenye nazi huwa na ladha ya kipekee tofauti na vile vya mafuta. Hii ni sababu tosha ya kutumia nazi tofauti na mafuta.

Tumia mafuta mbadala
Kama vilivyo vidole havifanani, basi na mafuta ya kula huwa hayafanani. Mafuta ya kula huwa na viambato tofauti kutokana na chanzo chake. Kwa kusema hivyo basi jua kuwa kuna mafuta bora na yale yasiyo bora. Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa mafuta yasiyo bora yana kiwango cha juu cha saturated fats ambayo husababisha kuongezeka kiwango cha koresteroli (Cholesterol) mwilini. Madhara ya koresteroli mwilini ni kuwa husababisha matatizo ya ugonywa wa moyo kwa kujaza mishipa ya damu na mafuta.

Inabidi kuwa makini sana kwenye kuchagua mafuta ya kula, kwani ni vitu vidogo sana vinaweza kukuletea matatizo makubwa mwilini mwako. Kuna aina nyingi za mafuta unaweza kutumia ambazo hupatikana kwa bei rahisi na nafuu. Mfano wa aina tofauti za mafuta haya ni mafuta ya salmi, mizeituni, nazi, parachichi n.k.

Tumia maziwa
Mie ni mpenzi mkubwa wa kuunga chakula na maziwa - unaweza kusoma post hii au hii ili kuona maujuzi ya maziwa. Najua maziwa si kiungo cha kila siku kwenye jamii yetu, lakini ukiweza kujaribu, maziwa ni kiungo kizuri sana kwenye vyakula. Maziwa huleta ladha tofauti kwenye chakula na kuleta hamu ya kula - hasa kwenye maharage na wali - unaweza kujing'ata kidole.

Maziwa yanayotumika hasa kwenye mapishi ni sour cream (maziwa mgando au mtindi) lakini unaweza pia kutumia maziwa halisi ya ng'ombe. Hiki ni kiungo kimojawapo kikubwa cha vyakula vyangu ukitoa nazi. Natumia maziwa kwenye kuandaa wali, maharage, na aina nyingi za mboga. Kitu muhimu cha kuzingatia kama ukiandaa chakula na maziwa ni kukihifadhi vizuri maana hakitochelewa kuchacha kama hutohifadhi kwenye jokofu.

Acha kutumia kabisa mafuta
Mazoea yana tabu, kama wasemavyo waswahili. Lakini, je wajua kuwa vyakula vingi tunavyoandaa huwa vina mafuta ya kutosha na hakuna haja ya kuongeza mafuta zaidi? Nafahamu kwa baadhi ya watu ni vigumu sana kupika bila mafuta sababu wamezoea kuogelea kwenye mafuta wakati wanakula - unakuta mtu midomo inang'aa kama amewamba lipshine kumbe wese. Hata hivyo, kuacha kutumia mafuta inawezekana, hasa kama unajali afya yako.

Mfano mzuri ni kufanya mapishi mbadala, unaweza kukaanga kitunguu bila kutumia mafuta, maana kitunguu kina mafuta. Unaweza kutokaanga nyama bali ukachoma, au pia ukatumia mafuta yaliyo kwenye nyama kumalizia mapishi yako. Unahitaji jitihada na muda kiasi kusahau kutumia mafuta, na hivyo kufikia malengo yako ya kulinda afya. Mie nilipoanza kuacha kutumia mafuta kwenye kupika nyama za kusaga niliona ni ajabu, lakini baadae baada ya kujifuza kiasi nikagundua kuwa ni kitu kinachowezekana na matokeo yake ni kula chakula kinachokuwa bora na afya.

Mfano wa vyakula unaweza kupika bila mafuta ni kama nyama aina zote, mboga unazopika kwa kutumia nyanya za kopo - maana nyanya za kopo zinahifadhiwa na mafuta.

Je una maoni mbadala kuhusiana na matumizi mbadala ya mafuta ya kula? Tuambie hapa kwenye maoni na pia ni vizuri kama utashare haya mawazo na wenzio - kama ukimjali utataka ajue pia, basi bofya hapa kushare hii na rafiki zako.
 
Nazi.
Karanga.
Alizeti.
Ufuta.

Zinapatikana kila kona ya tz,ila kimbembe ni bei kwa wale tunaoishi dar.

Maharage ni Nazi na karanga.
Dagaa ni Nazi.
Vegies ni vyote vinafaa.
 
ACHENI UONGO
mafuta ni mafuta tu hiyo alizeti wakishaivuna bei itakaa sawa tu ila kwa sasa nunueni tu
mbona Petrol inapanda na kushuka wenye uwezo wanainunua na kufanya yao
ukiogopa Chelesteroil utaondoka na UKIMWI, sukari au ajali
Huwezi kaanga chips kwa nazi
huwezi oka mikate kwa mafuta ya karanga
kila mtu apambane na hali yake awezapo kupakuna
 
Vyote ulivyo sema ni ghali kuliko mafuta Nazi hapa dar ya bei ndogo 800 wakati mafuta kipimo mia tatu alizeti ndio balaa kalanga kilo 4000 niambie nafuu inatoka wapi
 
Back
Top Bottom