Iwapo patatokea serikali makini katika mfumo wa sasa wa maisha, na kubana miaya yote ya mapato ya ziada haitopata kura yoyote toka kwa wafanyakazi. Ingawa asilimia 80 ya Watanzania ni wakulima, sidhani hata hao wakulima kama wataweza kuipigia kura, kwani kwa namna moja ama nyingine nao hufaidika kuwa na ndugu zao wafanyao kazi serikalini.
Mimi kwa mtazamo wangu ni kwamba wafanyakazi wa serikali wanaweza kuishi kwa kipato chao halali kabisa. Kinachoitafuna bongo sasa hivi ni tamaa. Tamaa ndiyo inafanya maisha yawe magumu bongo.
99.9% ya wabongo wana ndoto za kuishi maisha ya luxury, hivyo kufanya watu wasiridhike na wanachopata. Na hili ni tatizo la kimfumo kwani mfumo wetu upo hivi ( Serikali, Mfanyakazi wa umma, Mfanyakazi wa sekta binafsi, mfanyabiashara(including wenye nyumba), mkulima, kibaka) hawa ndiyo players wa ugumu wa maisha ya bongo.
1. Kibaka, huyu yeye anatamani sana kuwa na maisha bora ila ni mvivu wa kufikiri kipato halali na hivyo kuzivia vya wenzake na kufanya uharibifu. Huyu yeye angeweza kudhibitiwa kwa kuwezeshwa na serikali makini kielimu na hata kupewa mbinu za kujitegemea kama kilimo n.k
2.Mkulima, huyu yeye ndiyo moyo na maisha kwa wote kwani anasaidia kulisha taifa, ila mtu huyu hapo mwanzo alikuwa anakopwa bidhaa zake na vitengo vinavyoanzishwa na serikali isiyo makini, wafanyabiashara pia wanamlipa pesa kidogo kiasi kwamba anaona kilimo hakifai na kupunguza tija na matokeo ni supply kuwa ndogo na vitu kupanda bei.
3.Mfanyabiashara/mwenye nyumba; huyu yeye anachofanya ni kunyonya kotekote yaani kwa mkulima anamlipa kidogo na mlaji anamcharge sana. Tena hawa wao wanafanya kazi zao zaidi kwa kuangali nini wanapata wafanyakazi. Mshahara ukiongezwa na serikali isiyo makini (ambayo hufanya hivyo kisiasa kwa kutangazia uma) basi hawa huhakikisha kuwa wanachukua zaidi toka kwa mfanyakazi, wenye nyumba nao kila mwaka wanapandisha kodi by 40% - 100% wakishirikiana na madalali bila sababu (free market hiyo).
4. Mfanyakazi sekta binafsi; hawa wapo makundi mawili, kubwa ni lile la wanaonyonywa sana kwa kulipwa mshahara chini ya kiwango cha kuishi hata kwa siku tano, hawa nao wakipata mwanya lazima waibe, mfano wa kituo cha mafuta wanauza 0.65litre kwa bei ya 1litre(ujanjaujanja).
Kundi la pili ni wale wanaolipwa vizuri sana, wao hawa ndiyo wanaishi kwa kipato chao halali, kwani wanatumika ipasavyo, hawana muda wa ziada.
3. Mfanyakazi wa uma. Huyu yeye ndiyo buyu la wanasiasa. kila May Day wanatangaza kuongezewa mishahara kwa kuanzi na Tshs 100, mpaka Tshs 20,000. Sasa hawa ndiyo target ya wafanya biashara, mshahara ukitangazwa umeongezwa kwa hakika shs 100, wao hupandisha bidhaa kwa shs 1000, kuna gap ya shs 900 hapo, hii itatoka wapi? (Jibu sahihi lipo, tumia nafasi uliyonayo kwa kuziba gap hilo na hutaulizwa na serikali kwani wao pia wanajua hilo).
Kwa serikali makini ikiziba mianya yote nilitaja hapo juu, hakika itapata kura nyingi sana, kwani kinachoongelewa hapa si nominal income (yaani unampa mtu mshahara wa millioni kumi, wakati kodi ya nyumba ni million 11) haisaidii, hapa kinachotakiwa ni Real income ( uwezo wa fedha kununua bidhaa) kama unampa mtu mshahara wa shs 10,000, kodi ya nyumba shs 1000 hata pata wazo la kuziba gap. Serikali makini ni lazima iangalie wafanyakazi katika mtazano wa Real income na si Nominal income. Pia waache kutumia mishahara ya wafanyakazi wa umma kisiasa, kwani kutangaza ni ku-alert "mafisi, vultures (wafanyabiashara) kuwa cha bure kipo.
Serkali makini lazima itumie sheria kulinda wananchi na si kuitumia pale panapokuwa na manufaa kwao. Naam! Bongo mtu unaweza kuishi kwa kipato halali kama hayo yatafanyika, vinginevyo tutaendelea kuziba GAP.