Unaishi kwa kipato chako?

Jamani wana JF kuna kitu nimekuwa nikijiuliza kwa muda, kwa maisha ya sasa yalivyokuwa magumu kwa mtanzania aishie Dar ni shilingi ngapi kwa mwezi kama mshahara yaweza kumtosha angalau kupambana na hali ya maisha ya sasa.

Tuangalie kwa mtu ambae yuko single na anaishi peke na kapanga chumba/vyumba na mtu ambaye ameoa,kapanga na ana mtoto mmoja au wawili.Kuna watu kadhaa nimeongea nao na wenyewe wamekuwa na maoni tofauti wengine wanasema 500,000-800,000 na 1000,000-1,300,000.

Wana jf naomba kuwakilisha na natumai nitapata maoni mengi kutoka kwenu, natanguliza shukrani kwenu
 
Kwa watu wa kimya cha chini cha mshahara ni ngumu, lakini kwa wafanya kazi wanaopokea kuanzia 600,000 na kuendelea, unaweza mradi tu uwe na adabu ya katiaka CAE ( yaani consume as you earn), sio unakuwa na tamaa ya kupata vikubwa zaidi ya unachoingiza!
 
Jamani wana JF kuna kitu nimekuwa nikijiuliza kwa muda, kwa maisha ya sasa yalivyokuwa magumu kwa mtanzania aishie Dar ni shilingi ngapi kwa mwezi kama mshahara yaweza kumtosha angalau kupambana na hali ya maisha ya sasa.

Tuangalie kwa mtu ambae yuko single na anaishi peke na kapanga chumba/vyumba na mtu ambaye ameoa,kapanga na ana mtoto mmoja au wawili.Kuna watu kadhaa nimeongea nao na wenyewe wamekuwa na maoni tofauti wengine wanasema 500,000-800,000 na 1000,000-1,300,000.

Wana jf naomba kuwakilisha na natumai nitapata maoni mengi kutoka kwenu, natanguliza shukrani kwenu
 
This is not realistic. If one makes shake deals for survival its not a sin but a sin is to make surplus out of shake deals.

Naamini kumwezesha mwandishi kwa kibahasha cha nauli ya cha 20,000 kila akija kwenye story sio rushwa na sio dhambi ili mradi mwandishi huyo afanye kazi yake kwa objectivity na sio kufagilia kwa ajili ya kile kijibahasha. Bila uwezeshaji hakuna investigative journalism, jee hii nayo ni rushwa?. Jee uweseshaji wa Ikulu kwa local media to cover presidential visits, nayo hii ni rushwa?. Its not.

Mwandishi anayekwenda kwa kiongozi na kusema anayo skendo ya kiongozi huyo na kupanga bei ili asiitoe, hii ni blackmail na rushwa mbaya ambayo ni dhambi.
Ama editor atakayepokea kijibahasha cha 50,000 ili makala zangu za PR za makampuni zitoke, is doing me justice wakati editor huyo huyo akivuta fungu nene ili kuzuia habari fulani isitoke, this is sin.

Hakuna ubishi kuhusu maisha magumu ya mtumishi wa serikali. Wale wenye kuweza kuongeza kipato kihalali kwa safari, vikao, semina, warsha na makongamano, they are doing the right thing. Wale wanaotumia njia zisizo halali kama kwenye deals za zabuni, they are doing the wrong thing.

Amini usiamini Per Diem ya serikali kwa mwaka juzi ilikuwa ni 45,000 kwa ofisa wa juu. Hii ndio per diem ya katibu mkuu, waziri mpaka rais!. Kinachowakomboa ni posho na stahili mbalimbali ikiwemo kulipiwa hoteli full board na mengineyo and its not wrong. Its only wrong kama unatafuta hiyo per diem kwa makaratasi tuu huku safari halisi haipo.

Katika hali kama hii, dhana ya MMKJJ ya kidole kimoja kikielekezwa kwa fisadi na vitatu ukivielekeza kwako ni ya ukweli mtupu. The truth life is a struggle for existance and survival for the fittest. What matters more is 'The End Justify The Means'.

Kuna baadhi ya mambo umeongea ambayo ilikubidi ufanye utafiti wa kina kama issues za per diem za serikali, tafadhali tafuta waraka wa mwongozo wa posho za serikali kuu na taasisi zake kwa miji ya ndani na nje ya nchi kutoka kwa msajili wa hazina .....usiongee tu ili mradi uonekane umechangia
 
MwanaKijiji,

Neno "Kipato" maana yake nini? Kama kipata maana yake ni malipo unayoyapa kihalili kutokana na kazi unayofanya/unazofanya, basi jibu ni HAPANA..

Maana sisi wafanyakazi wa Serikalini huwa hatufanyi kazi lakini tunalipwa mshahara mnono!
 
Mwanakijiji mie hata sitaki kusema naishije kabisa mwisho mniitie takukuru waanze kuchunguza ,
maisha ni magumu na hali ni ngumu kwa ujumla ..
 
Mshahara hautatosha hata ukiwa mkubwa kiasi gani. Kama mchangiaji mmoja hapo juu alivyosema, kadri mshahara/kipato kinavyoongezeka, mahitaji pia yanaongezeka. Hivyo, nidhamu ya matumizi ndio njia pekee katika kuwezesha kuishi maisha bora. Kuna gharama nyingi zisizo za msingi katika maisha yetu ya kila siku. Tujitahidi kuainisha mahitaji yetu muhimu na jinsi ya kuyapata kwa gharama nafuu.[/QUOTE]

Recta, umeargue vizuri hili swala mpaka nimefurahi...labda kwasababu na mimi ni mlengwa na pia kwa vile ninajua per diem sio favour bali ni stahiki yangu kwa kazi niliyofanya na katika mazingira niliyokuwa....(malazi, chakula, other social amenities, usafiri wa hapa na pale na emergency) ila ningependa kutofautiana na wewe katika hili suala la kwamba mshahara hauwezi kutosha hata ukiwa mkubwa kiasi gani. jambo la muhimu hapa linaloongelewa na wengi ni mshahara wenye kukidhi standard ya maisha haya:

Single Person

1) Usafiri kwa mwezi (daladala) - 50,000
2) Chakula - 300,000
3) Vocha na mambo mengine - 50,000
4) Mavazi - 50,000
5) Malazi - 50,000
6) Matibabu - 50,000
7) Akiba - 150,000
Jumla 700,000

Mtu aliyeoa/olewa na watoto 2
1) Usafiri kwa mwezi (daladala) - 150,000
2) Chakula - 400,000
3) Vocha na mambo mengine - 100,000
4) Mavazi - 150,000
5) Malazi - 200,000
6) Matibabu - 150,000
7) Akiba (Ada) - 200,000
Jumla 1,350,000

Tentative estimates, hapo kuna mambo ninaweza kuwa nimesahau au nimeyakoleza lakini hiyo ndio picha mkuu....kumbuka hayo ni maisha anayopaswa kuwa nayo mtanzania wa kawaida kabisa aliyeajiriwa.
 
Mtanganyika tangu vita vya maji maji hafanyi tena Active Resistance ila ni Passive Resistance tu, we mwambie mshahara hata shilingi elfu ishirini (Tshs.20,000/=) per month hatopinga, yeye anachoangalia ni kuna DILI?!? Anaweza kuiba, kula rushwa, kufanya ubadhirifu etc etc au anaweza kutumia ofisi kama kijiwe cha biashara. Mianya ya rushwa, wizi,ufisadi na ubadhirifu ikifungwa kabisa, hapo ndiyo tutaona watanzania wakidai haki zao kama Tunisia, Egypt, Yemen etc ila kwa sasa wachache watadai coz wanajua chakula kipo cha halali na haramu! Tatizo la Passive Resistance hii haimgusi the opressor inawaumiza walalahoi zaidi
 
siyo kuhalalisha ndugu yangu bali kujaribu kufocus tatizo letu hasa ni nini? ndugu yangu Nyani ana msemo kuwa "Waafrika ndivyo tulivyo". Wengi wetu tunakerwa na ufujaji wa mali ya umma na matumizi mabaya ya ofisi (hasa inapohusu wanasiasa). Najaribu kuona kuwa yawezekana tunawanyoshea kidole kimoja wao, vitatu sisi wenyewe na kimoja Mungu shahidi yetu.

Swali la msingi ni kuwa hivi kweli ikiingia serikali makini ikakata mianya yote ya "kipato cha ziada" na kulazimisha watu kuishi kwa malipo yao ya mwezi, wangapi kati yetu wataipigia kura serikali hiyo?

Hapo ndio utajuwa kuwa migomo na fujo zote za warabu ambazo zinatokea sasa hivi ni cha mtoto!
 
Kwakweli nchi hii wezi wengi ila tunawanyooshea vidole wakubwa tu.
Vidole viwili kwao vitatu vyote vinatuangalia.
Hiyo mishahara na hizi extended families zetu ndio dah....
 
Do you know Why Slaa didnt win the Election?
Do you know why it is said that Sokoine's accident was somehow planned?

Read this thread, You will get a clear answer!!

Nami niliskia hili. Rumours zilianza kusambaa kuwa Slaa atabana vibaya. Watu wasahau visemina,wrkshp etc. Though am not sure to what extent did these rumours affect Slaa.
Mkjj amaeuliza kitu ambacho kabla ya kujibu vizuri ujiangalie na ujiulize. Personally naamini maadili yamepotoka kwa jamii yetu na kuaffect mpaka wale 'innocent'. 2006 baada ya kumaliza chuo (kwa kubeba box) nilipata kazi ya 600,000 kwa mwezi hapa bongo. After 3 months nikaona mbona wale vilaza darasani waliokua hawanikuti wanatesa vibaya. Watoto wa kike wanababaika na hata nikiwa na gf unaona ana admire lifestyle ya washkaji. Nikasema Nyamgluu dont be a fool as long as ur not hurting anybody piga dili.
Frankly hivi sasa nimekua mishen town mpaka washkaji wa nje nilioonana nao wanashangaa na kuniuliza where have my dreams and visions for prosperous africa and tz gone. Lakini niliona ni ujinga na maisha mazuri yananipita nikijifanya mtu wa maadil sana!
 
Na mshahara wa 1.5 ila naendesha vx ltd wife ana ka rav4. Vx nilipata kwa mlolongo mrefu lakini ultimately ni jamaa alishindwa kukomboa hapo bandarini nikaitoa kwa mil 6 mshkaji nikampa 5 kwa installment. Sasa nikiingia kokote dili zingine zinajileta tu. Sadly i've come to enjoy such living ya ujanja janja na tuko wengi hapa.
 
Hivi tunawezaje kuishi kwa matumizi yafuatayo kila mwezi? Fikiri; Matumizi nyumbani; chakula, umeme, gesi, maji, soda/juisi za wageni.Ada za watoto zinazolingana na za chuo kikuu Matibabu hospitalini,pesa ya walinzi kwamwezi, sherehe za kuaga na kukaribisha mwaka mpya, Zaka ya kanisani na misikitini Kupanda Mbegu/ Sadaka Shukurani ya Neno Tozo za Flying (wazoa taka wa mikokoteni ambao huzitupa hapo hapo) Madalali wa nyumba/viwanja Pango la nyumba Fremu ya biashara/ofisi Mazakayo wa mitandao ya simu [airtime vouchers] Mafuta ya gari Walinda/waosha magari (oya sista/blaza, mdogo wako nipo apaaa) Tozo za kuegesha magari Makato ya Mikopo Tozo za internet cafe ili uweze ku-surf Rambirambi ya mfiwa mtaani kwetu Harusi ya ndugu yako wa ukoo na zawadi Sendoff ya mtoto ya mdogo wake rafiki yako na zawadi Kumuaga mfanyakazi mwenzetu na zawadi Michango ya komunio ya 1 & 2 na kipaimara Michango ya besdei party na zawadi Ndugu wa kule kijijini Mshahara wa Hausigeli na na hausiboi Bodaboda, teksi na bajaj Duka la dawa Tuisheni ya mtoto Kuchangia wahanga wa mabomu na mafuriko.Kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa, Kununua CD/DVD ya Uzinduzi wa Kwaya yetu Chakula cha mbwa Machango wa Ujenzi wa Kupanua Kanisa Kuchangia Uinjilisti Masasi Auting ya kitimoto Ujenzi wa Nyumba Mwabepande Kuendeleza shamba mkuranga (linalotaka kutaifishwa kwa kutoendelezwa) Na kwa wale wenzetu wanaokwenda umbali wa Viti Virefu, moja moto moja baridi Maji ya Traffik Chai ya Nesi na Daktari, Kahawa ya Hakimu, Karani na PP Vishoka waunganisha maji na umeme Kidogodogo cha mjumbe na mtendaji wa mtaa Hivi hali inakuwaje? Mia mbili ya watoto wa mtaani/ombaomba, kitu kidogo cha wale wanaolazimisha kuosha kioo cha gari kwenye foleni. umeme uliopanda bei, gesi iliyopanda bei, maji yaliyoadimika, bado contingency mana huu usafiri unaotembelea ball joint,bush,fen belt havijafa...bado service,bado msosi wa mchana kazini esp kama maofisi yetu mama ntilie wanakaribiana bei na restaurants bado mchango wa kitchen pati na sare,baby shower...bado hujatoa watoto outing jumapili n.k

Hapo mwajiri amekuongezea mshahara kwa 7% tu wakati inflation ni above 19%. Ndipo unapoimba "...Mwokozi nitoe roho niepuke hili balaaa..."


Ukifikiria kwa makini unajiuliza watanzania wanasurvive vipi kwa style hii???
 
  • Thanks
Reactions: ral
The higher you go the hotter it became.....Mimi nilishaamua sichangii mchango wowote ambao sio wa matatizo na tatizo lenyewe liwe ni msiba au sort of that nature na mchango wenyewe ni mpaka niwe nazo....chakula ni dagaa, combat (maharage) na spinach au mcicha with ugali au mchele. Gari nimeliacha ni daladala kwa kwenda mbele...kama ni kariakoo - posta au ubungo -mwenge ninatembea.

Maisha ni magumu lakini inabidi tukomae nayo mpaka wazee huko juu wastaafu au wafe.
 
bongo ni ujanja tu ndo mana kule TRA na kwingineko ambako kuna mianya ya kutengeneza rushwa imekuwa kama himaya ya watu fulani, angalia maisha ya wale maafisa wa TRA wanaokagua mafuta yanayoingizwa nchini toka nje, wanaokagua makontena, nenda pale TICTS na TPA upate takwimu za makontena yanayopotea kila siku, yote hayo na mengine zaidi ya hayo hayatokei kwa bahati mbaya yanapangwa makusudi - wanapeana ulaji. Kwani unadhani maepa yaliwanufaisha kina nani?
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Back
Top Bottom