Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,968
- 727
Nimekutana na hizi picha mtandaoni ambazo zimepigwa hapa nchini Tanzania. Hizi picha si za kuvijunia hata kidogo. Na hili suala si lazima mtu aende darasani kujua ni makosa kumruhusu mtoto kunywa kilevi cha aina yeyote kama hajafikia umri wa miaka 18.
Katika hizi picha Mama mzazi wa huyu mtoto anaonekana kama kufurahia ustadi wa mwanae kufakamia bia.
Wewe ndugu Mtanzania na mwanaJF una ushauri gani kwa serikali juu ya hizi picha. Ni hatua gania mbazo zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya Mzazi wa huyu mtoto au mmiliki wa sehemu walipokuwa wanaburudika. Fungua hapo chini utaona hizo picha
Huyu mwanamke anapaswa kufunguliwa mashtaka
Hayp ndiyo madhara ya kusherehekea sikukuu, huyu mama alifany amakosa na naamini hata yeye mwenyewe alikuwa kalewa. Kwa mzazi mwenye busara huwezi kufanya ujinga wa namna hiyo.
Labda tuangalie ni nani mwenye jukumu la kwanza, tukikumbuka methali ya kiswahili "asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu" hivyo ni baada ya mama kushindwa ndio akina serikali watakuja. Hata ukimshika ukamfunga huyo mama au akalipa faini kama yeye mwenyewe anaamini kuwa yuko sawa basi atakachofanya ni kuhamisha mahali pa kufanyia hayo, ndio maana pamoja na serikali kuwa na sheria ya kuzuia kinywaji "kitamu" cha gongo, bado kinashamiri kwa vile wahusika hawajijali. Tuanze na kuwaelimisha Wazazi kuhusu malezi maana ndipo tunapanga maisha yetu ya kesho, huwezi kupanda ndimu uvune machungwa, walimu wanalazimishwa kutengeneza mazezeta (mwezi Octoba 2008, mwalimu mmoja alimfinya mtoto wa kigogo mmoja asubuhi ya saa 4, saa 11 baba kaja chukua kabomu kake kakuta kanalia, kisa!!!!!!!! mwalimu kanikata na kisu, WAPI???? (maana alipokatwa hapaonekani) anaonyesha mahali hata alama ya ukucha hakuna, kesho yake asubuhi Baba na mama wakafunga safari kwa mwalimu mkuu, "nionyeshe huyu mwalimu, utakosa kazi, nitamfundisha adabu huyu mwalimu..........." bahati nzuri huyu mwalimu mkuu ni sawasawa, akamwambia sitakuonyesha na kama hutaki mtoto wako aguswe hata akikosa sasa hivi mchukue mtoto wako sasa hivi peleka huko kunamkomfaa...... Wakatoka mkuku na mtoto wao wakaenda polisi, nako wakaulizwa alama ya kukatwa iko wapi "ilikuwepo jana" inabidi ucheke lakini NI SISI WAZAZI WA SASA NDIO MABOMU, Tufanyeje?????????Serikali ina lawama zake hata sisi wazazi tuna lawama. Japo sishauri kunywa pombe, lakini kuna sheria tunazivunja tukiona. Mfano, Serikali ina sheria ndogo ndogo za kuzuia kelele kama sauti za disko katika makazi ya watu, sababu ni usumbufu kwa wazee, watoto, wagonjwa hata kwa walio wazima (wenye afya) sababu ni usumbufu wanapopumzika. Lakini nani anazifuatilia hizi sheria, kila kona kuna vilabu vya pombe na mziki kwa kwenda mbele. Kuna wale wa kufanya matangazo ya biashara (promotion), siku hizi wanaweza weka kambi sehemu, tena katika makazi ya watu na kupiga mziki hadi asubuhi. Hivyo sheria nyingi tuliowapa dhamana ya kuzisimamia wala ni kama hawazioni.
Upande wa sisi wazazi, siku hizi mfumo wa kulea mtoto kama wa jamii unaondoka. Zamani ilikuwa mtoto ni wa jamii, ukifanya kosa unapewa adabu na mtu mzima, na ukirudi nyumbani ukisema ama wenzako wakiripoti kuwa ulipewa adabu, unapata karipio linine toka kwa wazazi. Hata waalimu walikuwa na usemi mkubwa sana na kujua udhaifu wa kila mtoto na kujaribu kwa kila njia kumnyoosha. Lakini sasa ukiona mtoto anafanya kosa ukampa karipio, usishangae wazazi wake kukufuata na kukwambia "zaa wako umkaripie", "wakaripie wakwako" nk. Hata waalimu wakitoa adhabu hupata matatizo kwa wazazi. Hata wazazi kuambiana ukweli juu ya watoto nayo imepungua kwa sababu hizohizo, mzazi mwingine kuja kukwambia naona mwanao anapotea siku hizi ni nadra. Wazazi haohao wanaenda katika kumbi za starehe usiku mpaka majogoo na watoto wao,
Hivyo, kwa Serikali ijaribu kufuata sheria tulizojiwekea, na sisi wazazi tujaribu kuwalea watoto wetu kijamii, mtoto wangu ni mtoto wa wanaJF, na watoto wa wanaJF ni wanangu.
Kuna ka imani ka ki-albinoalbino hivi kwamba watoto wakionja pombe katika umri huo ukubwani hazitawasumbua!
Pili mbona mambo haya yanafanyika tangu zamani kwenye pombe za kienyeji? Au wengi wenu humu mmezaliwa WODINI?
Mkubwa unamaanisha nini katika hiyo red? Nadhani umetoka nje ya uungwana na ni vema ukaomba radhi kwa kupotoka katika lugha uliyotumiaKuna ka imani ka ki-albinoalbino hivi kwamba watoto wakionja pombe katika umri huo ukubwani hazitawasumbua!
Pili mbona mambo haya yanafanyika tangu zamani kwenye pombe za kienyeji? Au wengi wenu humu mmezaliwa WODINI?
Mkubwa unamaanisha nini katika hiyo red? Nadhani umetoka nje ya uungwana na ni vema ukaomba radhi kwa kupotoka katika lugha uliyotumia
really? kuna watoto 4 wamelipuwa bomu kule moshi, 19 wamekufa Tabora...
Naamini Afande Kova au IGP Mwema wana mahudhurio mazuri hapa jamvini ingawa kwa kificho. Picha wanaziona, wanachotakiwa ni kumshughulikia huyu Mama kwa kujibu wa sheria.