Unahitaji utajiri wa fasta? Pitia hapa

Unahitaji utajiri wa fasta? Pitia hapa

Mkuu mimi ninachojua ili uwe tajiri, lazima uwe na roho mbaya. Asilimia kubwa ya matajiri ni wana roho mbaya, wanadhulumu watu mishahara/pesa wakati wao wanaingiza mabilioni, wengi ni wezi(wa kalamu), wafitinishaji, watafanya lolote ili wabaki juu nk.

Roho nzuri na utajiri hata haviendani.

Ni kweli usemacho
 
Sawa unaweza kuwa sahihi kwa namna fulani, lakini je hayo ni maneno sahihi ya kusema mbele ya kadamnasi na mtu mwenye ushawishi kama yeye humu JF?

Sasa swali lako sasa limejikita katika maadili.

Sijajua sheria nchi, hususani za JF zinasemaje na ama zinakataza Mambo kama haya kufanywa na JF member maarufu Kama Mshana Jr.

Hilo linahitaji mjadala tena.

Lakini kuna msemo unasema "To be rich you have to break the rules", Yaani ili ufanikiwe/ uwe tajiri ni lazima uvunje kanuni
 
Utajiri upo mkubwa tu we fanya mila za kwenu muombe Mungu na mizimu yako ikupe mali wala hakuna garama maziwa na pombe au kondoo
upo mle mle nyie warombo mnachinja sana mambuzi #mamseri nyie ni warombo busara ungeniuliza taratibu za kuachana na mambo ya kimila kabisa kuchinja chinja mambuzi upo utaratibu wake na mizimu yako itakuogopakabisa mbinu ambayo hutumika kuvunja mikataba hata kwa wale waliosaini na shetani
 
Nilivyifungua Uzi kwa mbwembwe nikijua nitapata jibu la kichwa Cha habari Sasa..mweeh🙄
 
Unahitaji utajiri wa fasta? pitia hapa.

title na maelezo yako ni tofauti kabisa, nilitegemea ungekuja na hizo mbinu(connection) za kupata huo utajiri ila umeishia kupiga porojo tu.
...Na Mimi ndicho nilichofikiri, Comrade Kitombise.
Nilifungua Uzi haraka haraka nikijua nitakuta madata ya kuniwezesha kupata Utajiri....ili angalau Krisimasi na New Year yangu I we njema
Nakutana na Maelezo kibaooo ambayo hayaniambia chochote cha jinsi ya kupata Utajiri fasts!
Kichwa cha habari cha post kinafaa kurekebishwa !!!
 
Boss nilimiss post zako kila nikiingia huku lzm nikuserch
Naomba kujua ili
1-:uitwe tajiri unatakiwa kumiliki fedha kiasi gani
2-:Ni nini kipimo cha umaskini
 
Ila inauma! Unakuta mtu amekaa viti virefu akipiga beer huku ameshika tama! Anafikiria namna ya kwenda kwenye chumba kilichotengwa ili kulisha watu pumba. Utajiri ni "kuthubutu "
Nimecheka sana huu uzi una mambo
 
...Na Mimi ndicho nilichofikiri, Comrade Kitombise.
Nilifungua Uzi haraka haraka nikijua nitakuta madata ya kuniwezesha kupata Utajiri....ili angalau Krisimasi na New Year yangu I we njema
Nakutana na Maelezo kibaooo ambayo hayaniambia chochote cha jinsi ya kupata Utajiri fasts!
Kichwa cha habari cha post kinafaa kurekebishwa !!!
kabisa kinafaa kubadilishwa
 
Boss nilimiss post zako kila nikiingia huku lzm nikuserch
Naomba kujua ili
1-:uitwe tajiri unatakiwa kumiliki fedha kiasi gani
2-:Ni nini kipimo cha umaskini
Ili uitwe tajiri basi ni lazima uwe na pesa ya ziada ya kutosha ya kufanya mengine utakayo baada ya kuwa na uwezo wa kujihudumia matumizi ya lazima na yasiyo ya lazima
Utajiri una viwango kuanzia vidogo mpaka vikubwa
Kuna utajiri ngazi ya familia
Kuna utajiri ngazi ya ukoo
Kuna utajiri ngazi ya kijiji tarafa, wilaya,mkoa Taifa mpaka kimataifa...

Ili uitwe maskini ....sahihi zaidi ni fukara maana yake ni ile hali ya kukosa hata hela ya kujihudumia mahitaji ya msingi...ufukara(umaskini) nao una viwango vyake

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Ahsante Sana boss nashukuru kwa majibu yako mazuri nimejifunza kitu
 
Pesa haina rafiki..pesa haina utu..bali pesa hujisimamia yenyewe...ndio maana unaambiwa ya kwamba PESA HUENDA KWENYE PESA..
Pesa ina mikondo yake
Pesa ina mifereji yake
Pesa ina formula zake
Pesa huambukiza pesa, kwa hiyo ukihitaji pesa ni lazima uwe na pesa na hili sio utani

Kama bado hata hela ya kujihudumia inakupiga chenga usijihangaishe kutafuta utajiri huu wa shortcut. Utaishia maumivu ya kutapeliwa.

Mi ndo nafanya mikakati natakiwa nipate pete itakayo fanya biashara zangu ziende alafu na wale wa vijicho niwadhibiti....ngoma zikikaa sawa nitaleta mrejesho...sitanii
 
Habarini ndugu zangu wa JamiiForums,

Mada hii ni maalum kwa wale wanaotaka utajiri wa haraka bila kujali madhara yake

Kabla sijaendelea na muktadha wa mada lazima niwaambie na mlitambue hili kwa hakika Dunia hii ndugu zangu ni katili tena ni katili hasa na viumbe wake ni watu wabaya na wenye rohombaya hasa.

Usisadiki kamwe wala kuaminishwa na stori za vijiweni za mafanikio ya wengine kupitia uchawi, ushirikina au ulozi.

Kumbuka hili kwenye kila fanikio la mtu nyuma yake kuna sehemu ya siri ambayo kamwe hatakuwa tayari ku share nawe hata umpe nini kumbuka sana hili na lizingatie

Sasa basi hiki kitu kinachoitwa utajiri ninini? Utajiri ni kuwa na makaratasi mengi sana yanayoitwa pesa. Ukiwa na haya makaratasi maalum mengi mengi sana ndio unaweza kuwa na uwezo wa kufanya chochote utakacho kwa matamanio ya kawaida ya kibinadamu.

Tunatofautiana kiwango cha wingi wa umiliki wa haya makaratasi maalum yaitwayo fedha au pesa au shekeli na kwa kadiri unavyoyamiliki kwa wingi ndio uchoyo ubinafsi ubahili na rohombaya unavyokutamaki ni jambo la kiasili mno.

Pesa haina rafiki..pesa haina utu..bali pesa hujisimamia yenyewe...ndio maana unaambiwa ya kwamba PESA HUENDA KWENYE PESA..
Pesa ina mikondo yake
Pesa ina mifereji yake
Pesa ina formula zake
Pesa huambukiza pesa, kwa hiyo ukihitaji pesa ni lazima uwe na pesa na hili sio utani wala sio maskhara!

Tafuta kwanza kianzio ndio upate kiendelezo chake kwa njia hizohizo!

Usitegemee wala usijidanganye kama kuna njia za mkato kwenye utajiri. Huo utajiri ili kuupata unahitaji pesa pia, pesa nyingi, pesa za kuharibu na kuangamiza ili upate maradufu yake!

Utajiri unaoitwa wa mkato ama haraka unahitaji makafara makubwa, hakuna kitu kinakula pesa kama haya makafara, lakini ni lazima umpate mtakatifu mwenye dhambi la sivyo utaishia kupigwa.

Hakuna cha bure duniani na kila mtu ni mhitaji. Usidanganywe na waganga wa mitandaoni na wale wanaotoa pesa za majini. Majini hayaendeshwi na kiumbe dhaifu aitwaye binadamu.

Katika hali hiyo uliyo nayo na changamoto ulizonazo kwenda kwa mganga akupe dawa ya utajiri ni kujitia dhambi bure na kumfaidisha mganga.

Utajiri wa pesa ni mali ya mkuu wa anga na ili uupate ni lazima utoe sadaka kubwa. HAKUNA CHA BURE DUNIANI. Kishapo uingie mikataba yenye masharti magumu na mazito.

Matajiri wetu kila mmoja ana siri yake binafsi na wana siri za jumla kulingana na kiwango cha ukwasi wao.

Kama bado hata hela ya kujihudumia inakupiga chenga usijihangaishe kutafuta utajiri huu wa shortcut. Utaishia maumivu ya kutapeliwa.
Asa umetuita kufanyani? Wazee wengine bhana sijui wakoje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom