Hata kwenye daftari unaandika tu mzee. Toa ulichonacho
Ova
Ukiona aibu kuwa utaonekana umetoa kidogo, usiandike jina lako halisi kama tufanyavyoJF!!!
Hata kwenye daftari unaandika tu mzee. Toa ulichonacho
Ova
Sio mashindano lakini binadamu tumeumbwa na aibu mkuuKwani mashindano?
Matatizo mengine ni ya kujitakia tu.Sio mashindano lakini binadamu tumeumbwa na aibu mkuu
Sawa mkuuWe toa ulicho nacho ndugu
Sasa yanarudi mkuu, enzi za fanya kazi ndio upate pesa zimeenda na mwenye hiyo falsafa, sasa ni ongea maneno matamu ingiza mamilioni kilainiGood afternoon jamiiforums
Umeenda kwenye msiba wa baba yake rafiki yako sasa umefungua daftari la rambirambi unataka kuandika mchango wako wa 10,000/= mara ghafla unakutana na jina la mtu wa kwanza (sijui ni boss wa marehemu) amechangia 1,200,000/= unafanyaje? Yamenikuta sana haya miaka ya 2011 - 2017.
Unaweza ukajikuta unarudisha daftari la michango na kumuuliza mwenyeji wako "Frank, eti washroom ndio wapi?"
Mara nyingi nilipokuwa ninakutana na hali kama hii nilikuwa ninaamua kutokuandika kabisa katika daftari kisha ninaenda kwenye magenge ya hapo jirani na kununua nyanya, vitunguu na unga wa ugali kilo kadhaa au mikate ya waombolezaji kunywea chai asubuhi.
Nilikuwa ninaona aibu sana kuandika mchango mdogo wakati majina matatu ya juu wa kwanza ni 1,200,000, wa pili 900,000 na wa tatu 700,000/= alafu wa nne ndio niwe mimi na 15,000/= yangu? Hapana aisee bora nikampe mfiwa pesa mkononi.
Kuna mzee mmoja alikuwa ni dereva katika kampuni moja niliyokuwa ninafanyia kazi nilikuwa ninamuitaga mzee Juma.
Mzee nilimsimulia namna ambayo nimekuwa nikikutana na hali kama hii akacheka sana akniambia, babu hayo majina ya mwanzo ya waliochangia pesa kubwa huwa yanawekwa kwa makusudi ili kuhamasisha hawa wa chini wachangie nyingi pia kwa aibu.
Najua JF imejaa wamama na wababa wenye umri mkubwa (above 45) ambao wamepitia sana hali ya kubeba changamoto hizi za misiba majumbani mwao na wanaweza kutuambia kama ni kweli yale majina ya mwanzo yanatumiaka kama hamasa ama la. Ninaomba kuelimishwa.
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Wakati wa baba yetu JPM pesa ilikuwa ngumu sana kuipata.Sasa yanarudi mkuu, enzi za fanya kazi ndio upate pesa zimeenda na mwenye hiyo falsafa, sasa ni ongea maneno matamu ingiza mamilioni kilaini
Marehemu alikuwa ni mmasai nini?Sio bure.Hata kwenye daftari unaandika tu mzee
Toa ulichonacho
Hutakiwi kuwa na haya mzee mimi nishawahi kudai changu kwa marehemu,walipouliza tu kuna anayemdai marehemu nkatokeaa
Hutakiwi kuwa na haya mzee kwenye maisha
Ova
Niliona aibu nikaamua kumpa jamaa pesa mkononiMatatizo mengine ni ya kujitakia tu.
Basi wewe kwenye maisha huenda unapata tabu sana. Siku zote mchango siyo mashindano. Unaweza kutoa sh. elfu kumi ikawa umejitoa zaidi ya mtu aliyetoa sh. milioni mbili. Kwenye maisha ukishanza kuishi maisha ya ku-fake uko juu kuliko kipato chako utaumia. Kwa wale wakristo wanajua maandiko haya kutoka kwenye biblia: Kisha Yesu akaketi karibu na sehemu ya kutolea sadaka Hekaluni akawaangalia watu walivyokuwa wakiweka sadaka zao kwenye chombo cha sadaka. Matajiri wengi waliweka humo kiasi kikubwa cha fedha. Lakini mjane mmoja fukara, alikuja akaweka sarafu mbili zenye thamani ya senti kumi.Waswahili husema ya kwamba, "uso umeumbwa na haya"
OkayBasi wewe kwenye maisha huenda unapata tabu sana.
Ni bora kumpa mkononi mfiwa pesa ndogo kuliko kuandika kwenye daftariSiku zote mchango siyo mashindano. Unaweza kutoa sh. elfu kumi ikawa umejitoa zaidi ya mtu aliyetoa sh. milioni mbili. Kwenye maisha ukishanza kuishi maisha ya ku-fake uko juu kuliko kipato chako utaumia.
Kukubali maisha yako ni kitu muhimu sana, unayakubali halafu unakata mshipa wa noma.Niliona aibu nikaamua kumpa jamaa pesa mkononi
Asante mkuu, umefafanua vema sana. Thanks.Kukubali maisha yako ni kitu muhimu sana, unayakubali halafu unakata mshipa wa noma.
Hususan kama umeshajaribu kuyabadili ukashindwa
Na wewe una utu ambao haupimwi kwa hela, mtu anaweza kutoa hela nyingi lakini akawa hana mawazo mazuri, hela ikawa haijasaidia.
Au huyo mwenye hela akawa yuko busy sana hawezi kusaidia kazi fulani, sisi wengine ambao hatuna hela sana ndio tukapiga kazi.
Yote maisha tu, unyonge mwingine utajipa mwenyewe bila sababu.
Mwaka 1998 nishawahi kutoa Sh 10,000 kwenye msiba nikajiona mnyonge sana kwamba natoa kidogo.
Baadaye ikaonekana hiyo 10,000 ndiyo ilikuwa kati ya watemi, kuna watu walitoa mpaka 500.
Lakini unaweza kuambiwa kuna mama katoa 500 halafu kafanya kazi kubwa sana ya kupika msibani.
Nyerere alitufundisha, "Utu wa mtu ni kazi, pesa ni matokeo".
Mzalendo nafikiri unayajua haya mambo, basi tu.
Asante mtumishi wa MunguKisha Yesu akaketi karibu na sehemu ya kutolea sadaka Hekaluni akawaangalia watu walivyokuwa wakiweka sadaka zao kwenye chombo cha sadaka. Matajiri wengi waliweka humo kiasi kikubwa cha fedha. Lakini mjane mmoja fukara, alikuja akaweka sarafu mbili zenye thamani ya senti kumi.
Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, “Ninawaambia hakika, huyu mjane ametoa zaidi kuliko wote! Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao; lakini huyu mama ingawa ni fukara, ameweka kila kitu alichokuwa nacho, hata na kile alicho hitaji kwa ajili ya riziki yake.”
Kwanini mkuu?Marehemu alikuwa ni mmasai nini?Sio bure.
Mrangi na mmasai ni watani hivyo deni ni lazima lilipwe.Kama mkurya na mhaya.Kwanini mkuu?
OkayMrangi na mmasai ni watani hivyo deni ni lazima lilipwe.Kama mkurya na mhaya.