Nyalumana originally
JF-Expert Member
- Apr 24, 2019
- 408
- 1,312
Huku kwetu imekuwa balaa zaidi watu wanafake harambee na kuwaumiza waumini watiifu wenye ayaBasi wewe kwenye maisha huenda unapata tabu sana. Siku zote mchango siyo mashindano. Unaweza kutoa sh. elfu kumi ikawa umejitoa zaidi ya mtu aliyetoa sh. milioni mbili. Kwenye maisha ukishanza kuishi maisha ya ku-fake uko juu kuliko kipato chako utaumia. Kwa wale wakristo wanajua maandiko haya kutoka kwenye biblia: Kisha Yesu akaketi karibu na sehemu ya kutolea sadaka Hekaluni akawaangalia watu walivyokuwa wakiweka sadaka zao kwenye chombo cha sadaka. Matajiri wengi waliweka humo kiasi kikubwa cha fedha. Lakini mjane mmoja fukara, alikuja akaweka sarafu mbili zenye thamani ya senti kumi.
Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, “Ninawaambia hakika, huyu mjane ametoa zaidi kuliko wote! Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao; lakini huyu mama ingawa ni fukara, ameweka kila kitu alichokuwa nacho, hata na kile alicho hitaji kwa ajili ya riziki yake.”