Unafiki wa Vyombo vya Habari Tanzania

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,603
29,748
Sakata la kukamatwa mchora vibonzo Optter Fwema limetokea huku kukiwa na kilio cha kukosekana kwa uhuru wa maoni na ukandamizaji haki za raia.

Ukiondoa mitandao ya kijamii, hakuna chombo cha habari kilichoratibu mtiririko wa kesi ya ugaidi dhidi ya Mbowe.

Na kibaya zaidi kwenye hili sakata la mchora katuni Optter hakuna chombo cha habari kilichoripoti, hakuna tamko hata kutoka kwa Baraza la Habari Tanzania (TMC) wala MISA-Tan

Mashirika kama BBC, DW na mengineyo wameshaanza kutoa updates za kinachoendelea nchini.

Hii ndoa ya mitala baina ya vyombo vya habari na serikali ni wazi itapelekea ugumba kwenye uzishaji wa habari zenye mantiki.

Mitandao ya kijamii inageuka kuwa reliable source kwa taarifa nyingi muhimu kijamii.

Idumu JamiiForums
 
Kinachoendelea sasa ni muendelezo wa mwendazake, vyombo vya habari kufungiwa, kupewa onyo, kwa habari za kweli watakazo ripoti kama zitawaudhi watawala, ndio mtindo mpya wa siku hizi.

Serikali ya CCM siku hizi imeamua kuendesha nchi kwa mtindo wa kidikteta, wameshindwa kuwashawishi watanzania wazielewe sera zao sasa kilichobaki ni kuwatisha na kuwaadhibu wote wanaoripoti mabaya yao.
 
Hata jeifu hakuna uhuru wala kuheshimu maoni ya mwingine, mtu akikomenti mawazo tofauti na haya mavyama ya waganga njaa sisiemu au cdm unaoga matusi, so lazima kuheshimu maoni kuanzie jeifu kwanza.
 
Rushwa ni adui wa haki, wanaogopa kuukosa uDC, siku hizi hawalali masikio yao yamesimama kama mbwakoko wanasikilizia teuzi.
 
Hata jeifu hakuna uhuru wala kuheshimu maoni ya mwingine, mtu akikomenti mawazo tofauti na haya mavyama ya waganga njaa sisiemu au cdm unaoga matusi, so lazima kuheshimu maoni kuanzie jeifu kwanza.

Unachanganya mambo.

Ulichoeleza ndio uhuru wenyewe wa habari - unaopatikana hapa JF. Maoni yako sio lazima yaheshimiwe. Lakini umeruhusiwa kuyatoa. Ingekuwa wamekuzuia kutoa maoni ndipo ungelalamika. Basi kubali wengine nao wakujibu. Matusi ni tafsiri yako.

Labda udai kuwa JF kuna uhuru uliopitiliza; usio na mipaka.
 
Huyo Optter mwambieni hana kipaji cha kuchora cartoon, labda afanye ya kuchonga vinyago au kupaka rangi Kuta.

Huwezi kuchora cartoon ambayo tafsiri yake unaiandika mwenyewe. Yeye abakie msomaji tu wa cartoon za akina Masoud Kipanya.
 
Kila mtu ana namna yake kufikisha ujumbe.

Unachokitaka wewe usikazimishe kwa wengine.

Nakushauri anzisha darasa la wachoraji katuni labda
 
Kila mtu ana namna yake kufikisha ujumbe.

Unachokitaka wewe usikazimishe kwa wengine.

Nakushauri anzisha darasa la wachoraji katuni labda
Kamsaidie sasa kumtoa huko anakoshikiliwa. Siyo lazima wote tuwe wachora cartoon, inatosha kuwa msomaji
 
Akili za watu kuhusu consciousness zishadumaa mmmno kisa ubabe wa mwenda.

Hata yale ma NGO's yaliyoteteaga haki zawatu sahivi kimyaaaa!

Umeona saivi wazir Mweugulu anakopa kujenga barabara chakechake pemba. Nchi imekua holaaa kabisa mxyiuuuu
 
Hata jeifu hakuna uhuru wala kuheshimu maoni ya mwingine, mtu akikomenti mawazo tofauti na haya mavyama ya waganga njaa sisiemu au cdm unaoga matusi.......so lazima kuheshimu maoni kuanzie jeifu kwanza.......
Sema kweli usiogope matusi wala vitisho. Usilazimishwe kuchagua usikoamini kama Watz wengi wanavyozidi kuwa waganga njaa.
 
Back
Top Bottom