Unafiki wa CCM wafikia kilele!

Ehud

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
2,685
337
Katibu mkuu wa CCM amesema kuwa katika kikao kikuu cha halmashauri kuu ya CCM iliyokaa mjini Dodoma haikumtaja mwanachama yoyote wa chama hicho kuwa ni fisadi! Pia alitolea mfano dhana ya kujivua gamba ni sawa na yai linavyoatamiwa na kisha kutoa kifaranga.Ndiyo kusema sasa hivi CCM baada ya kujivua gamba imekuwa kifaranga!

My take: Kwa mtaji huu CCM haiwezi kuaminiwa kwa jinsi inavyojigeuza geuza kama kinyonga
 
Hii ni ajabu lakini mungu hamfichi mnafiki kifo kimeiandama ccm!

Nape alitaja hadharani kuwa wamewapa siku tisini mafisadi wajitoe wenyewe na kila mwanachama hata yeye mkama alitamka hivyo!
 
Ha ha haaaa!
Hii ni kali...sasa hivi wameacha kuwa NYOKA, wamegeuka KUKU!..My hairs!:A S cry:
 
CCM ni watu wa hatari sana kama nyoka. Wamewaogopa mafisadi imebidi waitishe press conference ili wawatetee ama kweli mafisadi na ccm damu damu na mafisadi ndio ccm yenyewe. Bila mafisadi hamna ccm. Kama wao ccm ni wanaume wawape barua wale mapacha watatu na siyo kuwatetea kama walivyojichoresha leo.

Down with CCM!
 
Sasa tumwamini nani,labda wanaona wameharibu wanafanya mpango wa kurekebisha
 
CCM walikuwa wanafanya mchezo wa kuigiza na kauli mbiu yao ya kujivua gamba. Bora janja yao imejulikana mapema!
 
poleni mashabiki wa ccm,mtakufa bure na chama chenu cha mawazo...hamia cdm
 
Back
Top Bottom