Apollo
JF-Expert Member
- May 26, 2011
- 4,920
- 3,221
- Thread starter
- #21
I can see you soul inavyopenda kuwa huru. Ni swali zuri sana mkuu.
Ili kuweza kujua jinsi ya kukaa bila wazo, ni vyema kwanza kufahamu "wazo" ni nini na "akili" ni nini. Ili kutambua kipi kinatoka wapi na kinakua vipi.
Akili (mind) ni kisima cha mawazo ambacho mawazo hutokea. Unaweza ukatuliza kisima hicho kitulia mpaka maji yake yakawa kioo kwa mazingira yanayozunguka. Sawa na mto ulio na maji yaliyotulia mpaka unaweza kuitazama na kujiona utazamapo maji yake.
Unaweza kukaa bila mawazo kwa kufocus katika kitu kimoja. Mfano meditation inamfanya mtu asiwaze bali atazame mawazo. Unakuwa unayatazama mawazo yanavyotoka akilini.
Wazo sio kitu chochote, wazo likiwa kichwani usipolipa kipaumbele lenyewe linapotea kwa kukosa nguvu. Hivyo badala ya kuwa mtumwa wa thoughts unakuwa mfalme wake, unakuwa unaweza kuamua kulipa wazo nguvu kwa kulifuatilia au kwa kuliacha. Pia unaweza kufanya Yoga, Mantra Chants, Music (hasa classic musics au melodies zilizotulia).
Kukaa bila thoughts ni taabu sana mwanzoni. Ni sawa na kuacha tabia ambayo umeizoea tangu ulipozaliwa.
mfano elimu dunia inasema kitu halisi ni kile unachokiona,kukishika,kukinusa au kutumia ile milango ya faham,unaweza vipi kutoa kitoa kitu kwenye imarginary world to real world.
Milango ya ufahamu inakusaidia kuingiza informations katika akili. Akili imegawanyika katika pande kuu hasa 2. Akili ya Conscious na Sub conscious. Milango ya ufahamu ni milango ya information kwenye akili ya Conscious Mind na sio Subconscious mind. Akili ya sub conscious haijui logics, haifahamu nyakati wala haifahamu sayansi na facts zinasemaje, whatever unachoimagine na kuamini nayo inaamini. Ndio akili ya VISUALIZATION, Na ndio akili ambayo artists wengi, painters, poetry masters, n.k wameweza kuitumia kwa kuvisualize kazi zao na kuweza kukufanya ukapenda kazi yake kupitia creativity yake ya subconscious. Mfano mchoraji, ili achore creativity yake lazima aiweke katika Subconscious mind na hapo inajitokeza katika physical world.
Hauwezi kuiacha the present world moja kwa moja, labda mpaka ukishauacha mwili wako baada ya kifo cha mwili. Lakini unaweza kuishi katika dunia zote (Ya sasa na dunia ya imagination/visualization).