Unabii wa ajabu uliotimia bila shaka

Unabii wa ajabu uliotimia bila shaka

Vitabu vyote viwili ni tamaduni za nje, Kizungu na Kiarabu. Wewe Mwafrika utamadumi wako uko wapi? Sio kwamba napinga imani za watu, naziheshimu ila wasiingilie ninachoabudu Mimi kama Mwafrika. Mababu wetu wa kale walivijua hivyo vitabu?
Biblia hata wazungu wamepelekewa na paul zile ni tamaduni za wayahudi,
 
Ameiba character wa kiyahud akafanya wake na aka edit story za wayahudi
mkuu hebutuachane nahayo Mana huyaelewi. naomba nieleweshe hivi papa ameukubali uchoko nakuona nikitu chakawaida?
 
Zab 53:1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu
Katika watu nimetokea kuwadharau ni huyo anaitwa kiranga, umejibu vyema, sababu kiranga ameconclude hakuna Mungu watu waprove ya nin kwake, swala la kulazimisha watu wa prove kwake ni wazi kwake bado anayokiu ya kumjua Mungu

Mfano mim Sina haja ya kumfuata mtu wa dini ya Hindu au butha aniprove uwepo wa mungu wao sababu sipo interested, lakin nikianza kuwakomalia waniprove uwepo wa mungu wao inamaana niko interested na dini Yao
 
mkuu hebutuachane nahayo Mana huyaelewi. naomba nieleweshe hivi papa ameukubali uchoko nakuona nikitu chakawaida?
Kwa Nini tumuache mwizi wa kazi za watu?

Ungeleta andiko ndani ya biblia linalosema uchoko ni kitu Cha kawaida ungefanya la maana
 
Quran haikuchukuliwa kutoka kwenye biblia


(b)Dai la Kunakili Biblia


Aidha wengine wanasema Muhammad alinakili mafundisho ya biblia na halafu akadai kuwa yanatoka kwa Allah (s.w). Lakini inadaiwa kuwa hakunakili kila kitu bali alichagua sehemu fulani fulani alizoziona nzuri. Ushahidi wanaoutoa ni kuwa zipo sehemu katika Qur-an ambazo zinafanana na zile zilizomo katika Biblia. Hivyo, kwa kuwa ilitangulia Biblia kabla ya Qur-an ni wazi kuwa Qur-an ndiyo iliyochota kutoka katika Biblia. Madai haya ni dhaifu kwa sababu zifuatazo:

(i)Muhammad (s.a.w) alisema na kusisitiza kuwa Qur-an imetoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

(ii)Muhammad hakujua kusoma wala kuandika.

(iii)Nakala ya kwanza ya Agano la Kale (Old Testament) kufasiriwa kwa lugha ya Kiarabu ilipatikana mwaka 900 A.D.Wakati huo ilikuwa imekwishapita miaka 200 tangu Muhamad kutawafu. Ama Agano Jipya (New Testament) lilitolewa kwa mara ya kwanza mwaka 1616, miaka elfu baada ya Muhammad (s.a.w) kufariki dunia!

(iv)Qur-an (4:82) imesema kuwa lau kama hii Qur-an ingetoka kwa asiye kuwa Allah ingekuwa na khitilafu nyingi. Hivyo mtu mwenye shaka na aitumie fursa hiyo kutafuta khitilafu katika Qur-an.
(v) Isitoshe, ikiwa kuna tungo mbili au vitabu viwili vimefanana, kufanana huko peke yake si ushahidi wa kutosha kuwa kitabu kimoja kimenakili kutoka katika kitabu cha kwanza kuandikwa. Hii ni kwa sababu yawezekana pia kuwa vitabu vyote viwili vikawa vimetegemea au kunakili kutoka katika kitabu cha tatu ambacho sisi hatukijui. Ilivyo ni kuwa Taurati, Injili na Quran ni vitabu vya Mwenyezi Mungu. Hivyo ni wazi kuwa kama Biblia imenukuu aya halisi za Tourati na Injili lazima aya hizo zitafanana na aya za Qur-an,kwa vile zote zinatokana na Allah(s.w).

Isitoshe utafiti uliofanywa na baadhi ya wanazuoni umeonesha kuwa amri kumi za Mungu zilizomo katika Agano la Kale kwa mfano, zimekuwemo katika vitabu vya Wahindu kabla ya kuja kwa Agano hilo la kale. Je, tuseme biblia ilinakili amri hizo kutoka kwa Wahindu? Si lazima iwe hivyo. Pamoja na kufanana huko katika baadhi ya sehemu bado kimsingi Biblia na Qur-an zimetofautiana kiasi kikubwa.

Tofauti za Kimsingi Kati ya Qur-an na Biblia

(1)Biblia si kitabu kimoja bali ni mkusanyiko wa vitabu 73 kwa mujibu wa madhehebu ya Wakatoliki au vitabu 66 kwa mujibu wa madhehebu ya Waprotestanti. Vitabu hivyo viliandikwa na waandishi wasiopungua 40. Qur-an ni kitabu kimoja kilichotoka kwa Mwenyezi Mungu na aya zake zote ziliandikwa mara tu baada ya kushuka.

(2)Biblia ni kitabu chenye mchanganyiko wa maneno ya Mwenyezi Mungu, Mitume na maoni ya wanahistoria. Qur-an ni neno la Allah (s.w) tu peke yake. Hata maneno ya Muhammad (s.a.w) hayamo katika Qur-an.
(3)Katika Agano la Kale na Jipya yapo maelezo juu ya historia ya maisha ya Mitume. Kumbukumbu la Torati siyo tu ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu bali pia historia ya maisha ya nabii Mussa (a.s). Injili ya Mathayo, Luka, Marko na Yohana zinaelezea historia ya Yesu kama ilivyosimuliwa na wanafunzi wake. Qur-an inataja habari za mitume waliopita ili kutoa mafundisho kwa watu lakini sio kama sira (biography) za mitume hao.

(4)Biblia inavyo vitabu kadhaa ambavyo viliandikwa miaka mingi sana baada ya kutawafu mitume hao. Ndio maana wanazuoni Wakikristo hupata matatizo sana katika uchambuzi wa maandiko hayo kwani hushindwa kumjua nani mwandishi na aliandika lini. Kwa mfano katika Biblia iliyotolewa na Collins iitwayo: Revised Standad Version ya 1971 uk. 12-17 imeandikwa kuwa Mwandishi wa 1 Samweli hajulikani, pia hajulikani mwandishi wa kitabu cha 2 Samweli, 1 Wafalme, 1 Mambo ya Nyakati, Esta, Ayubu, Yona na Habakuki.Hali kadhalika mpaka leo kuna wasiwasi kama kitabu cha Waebrania kiliandikwa na Paulo au na mtu mwengine.Na Encyclopaedia Britannica inakiri kuwa mpaka hivi hatuna uhakika jinsi au wapi vitabu 4 vya Injili vilizuka. Kinyume chake Qur-an yote iliandikwa wakati wa uhai wa Muhammad (s.a.w) na ikahifadhiwa vifuani na mamia ya watu.

(5)Injili 4 zilizomo katika Agano Jipya siyo Injili zote zilizoandikwa. Zilikuwapo Injili nyingine nyingi. Ilifanyika Sinodi (mkutano wa wawakilishi wa makanisa) mwaka 325 ili kuamua Injili zipi zichukuliwe na zipi zikataliwe. Injili ya Barnabas ilikataliwa.Na katika historia ya Kanisa viko vitabu vilivyokubaliwa na baadaye kukataliwa na kinyume chake. Ni binaadamu waliokuja baadaye ndio waliokuwa na uwezo wa kuamua lipi liwe neno la Mungu na lipi lisiwe. Katika Uislamu hakukuwa na Ijitimai yoyote iliyokaa kuamua sura ipi iwe Qur-an ama isiwe.
Nimependa jinsi ulivyojenga hoja tifautu na waislam wengine wanaojua kubisha tu hapa. Ila nataka nikuambie bado pia umekosea. .

Umesema inawezekana Biblia na Quran ilikopy kitabu Cha tatu ambacho hakijulikan kitu ambacho sio kweli. Ukweli wote Hawa wana copy kutoka Judaism. .

Zile amri kumi za Mungu kwa mtazamo ya kibinadamu ziko kumi tu ila kiuhalisia zile amri zilikuwa zaidi ya 600 sema tu zilizopata kurekodiwa ziko kumi. Hata ulisoma Taurati utaona Sheria ambazo ziliwalenga wayahudi. .

Kwa kuwa mwandishi hajukikani haimanishi hayakuwa matukio yanayowahusu wayahudi. Uzuri matukio haya yalirekodiwa na watu tofauti na wayahudi. Na pia matukio haya yameandikwa sehemu nyingi tu tofauti na wayahudi. .

Ni kweli wakati Biblia inakusanywa kukikuwa na vitabu vingi vimeandikwa na waandishi. Kazi ya shetani siku zote ni kupoteza ukweli. Lakini Historia hii uzuri waliweza wazee kutambua vipi ni vya historia iliyoandikwa mbeleni. Kwa hiyo vitabu ambavyo vilikuw a na historia husika vilikusanywa. .

Kitu usichokijua Biblia inazungumzia mahusiano kati ya Mungu na mwanadamu. Na kimebeba ujumbe ambao Mungu alizungunza na mwanadamu kupitia manabii. Leo hii Mungu akisema Jambo ukalinukuu ukaandika kitabu kilicho na maneno ya Mungu. Haibadilishi nadharia kuwa ni maneno ya Mungu kwa sababu kuwa imeandikwa na watu wengi.
Hujui kuwa Mungu amekaa na wayahudi miaka mingi na uzuri imerekodiwa miaka mingi sio tukio la siku moja? Angalia kipindi Cha daudi, kipindi Cha ayubu, kipindi Cha Isaya. Hao wafalme ambao wakitawala Israel

Nakala za old testament zilizotafsiriwa kiarabu kupatikana 900AD haimanishi hazikuwepo nakala nyingine kabla. Hizi ndio zilizopatikana. Nakala za Biblia za again za kale kama Isaya Ina date miaka 1400 BC. Nakala za again jipya complete ni 165 AD. Quran ikaja shushwa miaka 500 baadae. .

Kuna texts sumerian ambazo zinazungunzia Mungu mwenye nafsi tatu. Na kweli pia Kuna texts Hinduism ambazo zilianza kuwepo kabla ya Biblia kuwepo ambazo zinazungunzia vitu ambavyo vilikuwepo kwenye Biblia. Ila uzuri vyote vimetoka kwenye Judaism kwa kuwa hii ndo oldest manuscript zinazorekodi kwenye Bible.
Tofauti ya wayahudi na Christian ni kuamini kuwa Yesu kaja. Wayahudi hao hao ndo waligawanyika wengine wakawa Christian na wengine wakaendelea na uyahudi. Namanisha hawakuanini ujio wa Masihi. Walioamini ndio wanaitwa wakristo na wayahudi bado wanamsubiri Masihi. .

Kitendi Cha kuandika Injili ni biography iliyofanywa na wanafunzi wa Yesu. Umekubali kuwa neno hili lilirekodiwa wakati yanatukia. Sasa kwa nini Leo hii Muhammad aje azumgumzie historia ya wayahudi wakati yeye si myahudi.?
Kwa nini Quran yuache Abraham baba wa wote, inakuwaje kuhusu Mussa. Wakati kabisa Misri kuna ushahidi mwingi mpaka wa maandishi kutonyesha Mussa alivyowakomboa waisrael. Na ushahidi huu pia imerekodiwa kwenye Bible. Sasa Muhammed alihusika vipi na historia ya kiyahudi?
Je nyimbo za Daudi kweny Zaburi? Solomon Tena historia ya Suleiman na sanduku la agao la Israel Inapatikana Afrika mpak Leo hii huko Ethiopia na Zimbabwe, lakin muhhamed kaandika yeye inahusu vipi Islam?
Ukweli ni kuwa alileta kitabu ambacho kinavinasaba na Biblia. Mungu angemshushia kitabu ambacho kinawahusu waarabu tu bila kunasabiana na Bible. Hii pekee kinakifanya kisiwe perfect. .
Kama mnaamini wakristo ni wapagani na kitabu kitukufi kinarekodi matukio yaliyowatokea wapagani kweli hamuingiwi na wasiwasi?.

Kwanza kumuamini mtu ambae hakuwa msomi, hakuwa hajui kuandika na kwamba amekariri Quran kichwani make inatia shaka. Ila nifundishe kitu, kwa nini Mungu hakumshushia Quran siku moja? Kwa nini ilishushwa kwa muda mrefu wakati anapewa Muhammad?

Ndo kwanza nimeamka ngoja ninywe uji nikisuburia majibu yako. .
 
... Mtukufu ni yule aliyembeba mja wake usiku kutoka msikiti Mtakatifu (huko Makka) mpaka msikiti wa mbali zaidi (huko Jerusalem) ambao tumevibariki vilivyo jirani zake ili tumuonyeshe baadhi ya ishara zetu.

Hakika yeye pekee ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona
.
Hayo maneno kwenye mabano YAMEONGEZWA ,kwenye kiarabu hayapo
 
mkuu hebutuachane nahayo Mana huyaelewi. naomba nieleweshe hivi papa ameukubali uchoko nakuona nikitu chakawaida?
Papa na Uislamu Ni wamoja
download%20(8).jpg
 
Mwambie dini inafuata maandiko je maandiko yanaruhusu ushoga?
Ushoga ni tabia ya mtu
Mimi naamini mtu akiishiwa hoja analeta kashfa
Upo ushahidi ndoa zinafungishwa kanisani unataka ushahidi gani tena na nchi zote zinazoleta pigo za kishonga wakristo ni wengi na nchi inaendeshwa kikiristo kama uingereza na marekani ulisikia wapi nchi yenye tamaduni ya kiislamu ku supposed ushoga Qatar kasema hataki mashoga ila wanaolalamika ni wazungu ambao wamewaletea hyo bibilia wanasema hakuna haki za binadamu ukiristo na ushoga unaenda na Sisi waislamu acha tu support ugaidi siku mashoga wakizidi tuwasambaratishe
 
Mim mbona mkristo na sijawah lazimishwa kuwa shoga, unajua unaongea pumba sana Tanzania hakuna mtu aliyelazimishwa kuwa shoga ndo nimesikia kwako

Hata ukienda marekani au inchi yeyote dunian hakuna inchi inayolazimisha watu kuwa mashoga yaani ndo nasikia kwako kwamba Kuna watu wanalazimishwa kuwa mashoga

Nenda Zanzibar Kuna mashehe kibao wamewalawiti watoto wa madrasa huwez sema uislamu ndo umewatuma sio kweli, same kwa mapadre huwez sema kanisa limewatuma hizo ni tabia zoo, unavyosema watu wanalazimishwa kuwa mashoga ndo nasikia kwako
Nimemwakimbia nchi zinazo support mashoga zote zina ongozwa na wakristo kuanzia maraisi mpaka mawaziri lakini hawakemei na nimetoa mfano uingereza na marekani usijotoe ufahamu kwani ulivyosema waislamu ni magaidi Tanzania kuna gaidi au ulikuwa ushashiba mihogo tayari hawezi kutenganisha ukristo na ushoga na uislam na ugaidi pamoja na Uganga kazi za kiume kanisa lina bariki ushoga astaghafirullah
 
Hakuna namna yoyote Ile Kwa mtu yoyote yule anaweza kusema na kuthibitisha kuwa Qurani iliandikwa kabla ya BIBLIA TAKATIFU.
Qurani Kwa kifupi ni fabricated stories tu muhamad alipewa na majini basi.
Period.
 
Naandika kwa Elimu na hoja, Biblia ya kwanza iliandikwa lini ? Biblia imekuja baadae sana.

Vitabu vinne pekee ndiyo vimeitangulia Qur'aan, na si Biblia. Sasa wewe kama unasema ukweli tuambie Biblia iliandikwa lini kwa mara ya kwanza ?
Kuuliza si ujinga,
Hivi Taurati, Zaburi na Injili huwa vinasomwa msikitini Kwa rejea?
 
Hiki Kiswahili gani ? Nani amekwambia habari hizi ?

Lakini sifa ya Mtume kwa watu alio ishu nao alisikifika kwa tabia nzuri na uaminifu. Je Kuna lipi zito kushinda tabia njema na uaminifu ?

Sasa ndiyo utuambie wewe aliwezaje Hilo na hajui kusoma wala kuandika ?

Scholars gani wa Kiarabu wanakubali ya kuwa Biblia ilianza kabla ya Qur'aan ? Nitajie watatu nipate kuwajua.
Khurshid Ahmad (1999:86-87) serves as a classic example of a Muslim who believes that the Bible has something to say about Muhammad's revelation that is exegetically untenable. In his explanation on how the Qur'an influenced human history, he wrote:

In Islam religion has been perfected. That is another way of saying that with Islam the age of new revelation has come to a close, and that the age of realization of the principles revealed religion has been inaugurated. That is why in all the earlier scriptures references are to be found to the advent of the Prophet of Islam. Students of the Bible, for instance, know that Jesus had said: 'I have yet many things to say unto you, but ye cannot bear them now … He will guide you unto all truth: for he shall not speak of himself; but of whatsoever he shall hear, that shall he speak' (Jn 16:12-13).
 
Back
Top Bottom