Unaamini katika uchawi? Tushirikishe uliyowahi kukumbana nayo

ilipoishia sayansi ndipo uchawi ulipoanzia in mshana sound Mshana Jr
And vice versa.Pia sayansi ni jibu la uchawi,unaanza kwanza uchawi ndipo sayansi ujidhihirisha.
Ilikua miaka ya 2005 kijiji kimoja pande za Kondoa kinaitwa Kidoka nilikua nikiishi kwa Ustadh mmoja ivi mtu wa Kigoma ambae mda mwingi hakua nyumbani alikua mtu wa kusafiri sana

Mbele ya nyumba tuliokua tukiishi kulikua na barabara then kajishamba kadogo na mbele ya hiko kishamba kulikua na Mbuyu mkubwa sana

Story kijijini ni kua huo mbuyu ni maskani ya wazee wa ucku wanakutana hapo na kufanya mambo yao

Nilikua na tabia ya uoga wakati huo kutokana na experience ya mauzauza niliyokua nikiyaona nyumbani Dom kabla ya kwenda hapo kijijini.

Nyumbani kwa huyo Ustadhi nilikuwepo mimi, maustadh wengine wawili (watu wa Kigoma pia) na dogo mmoja (Marehem) na mke wa huyo Ustadh

Kulikua na mlango wa mbele (upande wenye ule mbuyu) na wa nyuma ni upande wa barabara kuu. Upande wa mbele kulikua na choo cha nyasi chenye mlango wa gunia ambacho binafsi nilikua ckitumii ucku, natokea mlango wa nyuma nabaua kwenye majani then narudi kulala

Basi bhana siku ya kwanza kuona mauzauza nilitoka ucku kama kawaida kukojoa nikamuamsha yule dogo tutoke nje. Wakati nakojoa nikiwa nimeface barabarani nikiupa mgongo ule mbuyu, niliona nimemulikwa na mwanga mkali kama wa taa ya gari ukinimulika kutokea nyuma ghafla then ukazima. Nikageuka nyuma kuangalia nikaona kitu kinaruka kuelekea juu ya ule mbuyu kikiwa kimeshika kama kijinga cha moto ivi. Niliamini kua yule ni mchawi alikua kwenye mishe zake lkn akaona kwa kua niko nje bac niutambue upeo wake, nikamshtua dogo turudi ndani fasta

Siku nyingine ucku wakati nimelala nilishtuka ucku nikawa nackia purukushani upande wa ule mbuyu nikaona nichungulie dirishani nione kuna nin. Ile kuchungulia kule mbuyuni namuona mtu akiwa anatoa nuru mwili mzima anafloat kutoka juu ya mbuyu kuelekea nyumba moja ya jirani na ule mbuyu, nikiwa namuona kupitia dirishani bac akafloat alivofika juu ya paa la ile nyumba akazima ghafla ckumuona tena

Visa ni vingi ila naona nisiwachose na ukizingatia mwalimu wangu wa kiswahili hakuhakikisha nimeelewa somo la Ufupisho
Tegesha camera ya simu kuelekea mbuyu huo kisha turushie
 
And vice versa.Pia sayansi ni jibu la uchawi,unaanza kwanza uchawi ndipo sayansi ujidhihirisha.

Tegesha camera ya simu kuelekea mbuyu huo kisha turushie
Afu ata ningekua huko wachawi wa cku izi wako smart sana wanafanya mambo kwa usiri mkubwa coz wanajua wanaweza wakarekodiwa
 
Back
Top Bottom