Ni kweli, nilifanya operation ya kuwaua ili mwanangu asiwe na woga lakini siku mbili mbele wadudu top wamezagaa nikaacha kuwaua mijusi mara siku mbili mbele wamezaliana wa kutosha na wadudu ikawa ndo baibai
Kwenye jina hapo umechanganya kidogo mkuu ngoja nikuletee stori kamili za utotoni
Mjusi kafiri (enzi hizo tukiita MCHODO) ni yule mdogo mwekundu hakai ndani ya nyumba bali yupo kwenye vishimo maeneo ya vichaka vidogo hasa mashambani wakati nyasi zimekauka. Enzi zetu tukiwa wajinga tumewaua sana kwa manati eti tukiamini tunapata thawabu. Unampiga mkia ukikatika unarukaruka nao unaupiga mpaka utulie eti vile unavyorukaruka unakutukania mama yako. Tulikuwa tunasema mtu akitupwa motoni (jahanamu) eti mjusi kafiri wenyewe unakwenda kuchochea kuni ili aungue vizuri
Mjusi wa kawaida (nyumbani wanamwita GONDO) ni mweusi ana mistari kama kijivu fulani au myeupe mbavuni. Yeye umbo lake ni kubwa kidogo zaidi ya mjusi kafiri. Huyu anaishi ndani kwenye nyumba za zamani ilikuwa humkosi mjusi huyu. Tulimuheshimu sana eti tukiamini motoni atakuwa anaondoa kuni ili mtu asiunguzwe, kwahiyo wanashindana na mjusi kafiri!
Mjusi wa mapangoni na milimani (enzi hizo tukiwaita CHUNGULUBANTO) Hawa kila mtu anawajua nadhani ukienda milimani ni wengi sana na umbo lao ni kubwa zaidi kuliko mijusi wengine niliowataja halafu wana mabaka. Kuna mengine sijui ndo midume, likikua kubwa zaidi linabadilika rangi inakuwa ya bluu na kichwa chekundu. Tulikuwa tunawaweka kundi moja na mjusi kafiri, ni kuwaua tu. Sababu ya kuwaua hawa eti tuliamini wanatutukana pale wanapokuwa wametulia kwenye jiwe halafu wanachezesha (nod) kichwa
Kwa siku hizi kutokana na maendeleo nadhani, ndani hakuna tena mijusi wale weusi wenye nyeupe bali kumekuwa na mijusi yenye mabaka ambayo wanafanana na hao niliosema wa porini/milimani. Tofauti yao ni kwamba hii ya ndani inang'aa sana na ile ya milimani weusi umezidi. Nimesema ni maendeleo kwa sababu tangu zamani tulikuwa tunawakuta mijusi hawa wa mabaka kwenye nyumba zenye lipu na sakafu tu huku nyumba zetuza kawaida tukiwaona wale wenye nyeupe na nyeusi tu (rangi ya alizeti)
Kwenye nyumba za tembe hasa zile zisizokaa watu muda mrefu kulikuwa kuna mjusi mwingine anayetisha zaidi. Miguu yake mifupi na umbile lake ni kama nyoka kama ni mtoto akiona kwa haraka haraka anaweza kufikiri ni nyoka. Nyumbani wanamwita ZOLWE
Nimejikuta nakumbuka mbali sana aisee