Umuhimu wa Mfumo Dume (Ubaba)

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,604
1,704
Baada ya makuzi mema yanayopingana na mfumo dume sasa ni wakati wa kuuangalia upande wa pili wa shilingi. Kwanza kabisa tafsiri ya neno patriarchy ambalo wanaharakati wa jinsia wanadai ni mfumo dume sio sahihi. Tafsiri yake halisi ni ubaba. Hii ni hali ya uongozi ama utawala uliojikita katika baba akisaidiwa ama kusaidiana na mama.

Wanaokubaliana na patriarchy inayotafsiriwa kama ubaba wanaamini kazi kubwa ya ubaba ni 'p' tatu yaani protecting (kulinda), providing (kutoa) na preside (kuongoza) japo wapo wanaodai p ya tatu ni profess (kuaminisha). Kama tulivyoona kwenye mjadala wa maamuzi, mapenzi hayawezi kwenda bila ubaba huu wa kuongoza, kulinda na kutoa.

Pamoja na kupinga ukatili wa mfumo dume ukweli ndio huo, ili mapenzi yafanikiwe lazima ubaba uongoze. Na tunapoongelea kutoa tunaongelea pesa - bila fedha penzi linakuwa mahututi na mwisho wake ni kufa tu. Pesa posa.
 
its about time mtu aanzishe a thread kuhusu hili
it was long overdue
namsubiri DC....na wengine
tafadhali muanzisha thread kiswahili zaidi kitumike
 
Wewe tangu jana unaongelea pesa tu.

kwenye mapenzi ni kosa kubwa kukubaliana na msemo wa Nyerere kuwa fedha sio msingi wa maendeleo bali ni matokeo tu - pesa ndio msingi mkuu wa mapenzi, bila pesa hakuna protection(ulinzi), provision(utoaji) na presiding (uongozi); kwa ufupi, bila pesa hakuna penzi.
 
its about time mtu aanzishe a thread kuhusu hili
it was long overdue
namsubiri DC....na wengine
tafadhali muanzisha thread kiswahili zaidi kitumike

kiswahili kimetumika vilivyo, kila neno la kiingereza limetafsiriwa hapo
 
hata kama mke anakuzidi pesa
baba lazima awe baba
awe kiongozi wa familia

sipendi mume b.w.e.g.e jamani
mie hata limbwata sijui huwasaidia nini kama linampumbaza mtu

unakuta baba anachomwa na kidole machoni anacheka cheka tu.
 
mimi siamini haya mambo ya pesa.mkipendana,mnasaidiana,kwa aliekuwa nacho,anajaribu kumsaidiana mwenzake.mambo ya kuweka hela mbele,naona kama hakuna mapenzi hapo.mimi nikikupenda,haijalishi unacho au huna muhimu kuwa happy katika relationship.ukiwa happy,vyengine vinakuwa easy.mkiwa pamoja tu,nafsi yako inaburudika,hata katika ndoa,mkiwa na mapenzi,hata kama maisha ndio hivyo hivyo,mnaridhika tu.usione watu na majumba yao katika ndoa na mali zao,wengine huwa na stress tupu utajiuliza huyu kulikoni,mbona ana kila kitu.
 
uliye naye hana pesa? kama anazo kwa nini huko na ambaye hana pesa?
 
hata kama mke anakuzidi pesa
baba lazima awe baba
awe kiongozi wa familia

sipendi mume b.w.e.g.e jamani
mie hata limbwata sijui huwasaidia nini kama linampumbaza mtu

unakuta baba anachomwa na kidole machoni anacheka cheka tu.

mkuu umuhimu wa pesa usitufanye tusahau msingi mkuu wa mada hii, yaani, umuhimu wa ubaba unaoongoza, unaotoa na unaolinda
 
"Now you're too young for girls right now But there's going to com a time And when it does You treat them like princesses ‘Cause that's what they are When you say you're going to do something, you do it Because your word is your bond Son and that's all you have And money…you make money Whenever you get the chance Even if you got to sell out once in a while You make as much money as you can Don't be stupid like your father Everything is so much easier with money son" - JOHN Q
 
hela nazitafuta mimi mwenyewe.kwa kujituma,huna tabia ya kumtegemea mtu,kwa the way nilivyolelewa.mapenzi kwangu,naangalia kikubwa tabia.

hujajibu swali

ps. kuna maskini wengi hawana pesa ila wana tabia nzuri
 
kwenye mapenzi ni kosa kubwa kukubaliana na msemo wa Nyerere kuwa fedha sio msingi wa maendeleo bali ni matokeo tu - pesa ndio msingi mkuu wa mapenzi, bila pesa hakuna protection(ulinzi), provision(utoaji) na presiding (uongozi); kwa ufupi, bila pesa hakuna penzi.

Kwangu fedha siyo "msingi mkuu wa mapenzi". Labda kwako na kwa wengine, lakini kwa baadhi ya watu wa karibu niwajuao mimi wakiwemo babu na bibi zangu sikuwahi kusikia wala kuona katika matendo yao kuwa fedha ndiyo msingi wao mkuu wa mapenzi yao.
 
tatizo lako unadhani pesa ni benjamins tu, pesa come in many forms including paperless and coin-less forms ndio maana inabidi urudi kwenye zile p 3: protection, provision and presiding
 
acha kubeba maboksi uone cha moto, hata kabula atakushangaa ukiwa pesaless
 
tatizo lako unadhani pesa ni benjamins tu, pesa come in many forms including paperless and coin-less forms ndio maana inabidi urudi kwenye zile p 3: protection, provision and presiding

Kuna mamilionea na mabilionea wangapi ambao love life yao ni hovyo?

Acha kuendekeza pesa dogo....umekutana na shoree gani wewe anayekuharibu fikra zako?
 
Back
Top Bottom