Umuhimu wa Mfumo Dume (Ubaba)

Kuna mamilionea na mabilionea wangapi ambao love life yao ni hovyo?

Acha kuendekeza pesa dogo....umekutana na shoree gani wewe anayekuharibu fikra zako?

mkuu hapa inshu sio utajiri inshu ni pesa, mtu kuwa na pesa haimaanishi kuwa ni tajiri
 
kwa the way nilivyolelewa.mapenzi kwangu,naangalia kikubwa tabia.
Haya yapo kwenye tamthilia tuu dada, binadamu kama mashine ya kibayologia inachoka na itafikia wakati ile tabia nzuri itafunikwa na ufukara wa mwanaume. Uwezo wa kujikimu kwa mwanaume ni muhimu sana katika mahusiano vinginevyo mwanamke sikumoja atajichokea. Elewa hapa simaanishi mwanaume kuwa na pesa nyingi kumzidi mwanamke lakini aweze kujikimu yeye kama yeye na familia yake bila ya kumtegemea mwanamke.
 
mkuu hapa inshu sio utajiri inshu ni pesa, mtu kuwa na pesa haimaanishi kuwa ni tajiri

Pesa kiasi gani? Manake hata senti moja nayo ni pesa. Hebu weka kiwango basi ili tujue nini hasa unachotaka kusema. Na weka wazi unazungumzia mapenzi ya namna gani..
 
Mi' ngoja ni pasue jipu.....

Wanawake wengi tunaogopa kusema pesa muhimu kwa sababu tunaogopa kuitwa materialistic, lakini kimsingi hasa wengi wanataka mwanamme awe nazo hizo [p] tatu

Binafsi nisingependa kuwa breadwinner wa familia maisha yangu yote. Kimsingi hata kipato ningependa chake kiwe kikubwa kuliko changu (ili nijiskie mwanamke???)
 
Haya yapo kwenye tamthilia tuu dada, binadamu kama mashine ya kibayologia inachoka na itafikia wakati ile tabia nzuri itafunikwa na ufukara wa mwanaume. Uwezo wa kujikimu kwa mwanaume ni muhimu sana katika mahusiano vinginevyo mwanamke sikumoja atajichokea. Elewa hapa simaanishi mwanaume kuwa na pesa nyingi kumzidi mwanamke lakini aweze kujikimu yeye kama yeye na familia yake bila ya kumtegemea mwanamke.

nakukabidhi hii mada, naona unaielewa kwa undani kuliko hata mimi, hebu mpige shule na nyani ngabu hapo maana naona analeta ubishi usio na tija japo kakiri mwenyewe humu kuwa asipobeba maboksi kabula atakula wapi
 
Mi' ngoja ni pasue jipu.....

Wanawake wengi tunaogopa kusema pesa muhimu kwa sababu tunaogopa kuitwa materialistic, lakini kimsingi hasa wengi wanataka mwanamme awe nazo hizo [p] tatu

Binafsi nisingependa kuwa breadwinner wa familia maisha yangu yote. Kimsingi hata kipato ningependa chake kiwe kikubwa kuliko changu (ili nijiskie mwanamke???)

si mchezo, naomba usaidiane na chamoto hapo juu kutoa somo, naona na wewe unalielewa hili suala kuliko mimi
 
hela nazitafuta mimi mwenyewe.kwa kujituma,huna tabia ya kumtegemea mtu,kwa the way nilivyolelewa.mapenzi kwangu,naangalia kikubwa tabia.

Tabia na maadili ni vigezo muhimu sana vya kuzingatia kwani hivyo huwa haviji na kupotea kama ambavyo pesa zinaweza.
 
pesa muhimu katika mapenzi jamani tuacheni tamthilia.tena sisi wanawake bila kuwa na mwanamme mtoaji mara nyingi mahusiano hayawi sawa.mwanaume lazima awe mwanaume na uanaume wake uko kwenye izo p tatu
 
Tabia na maadili ni vigezo muhimu sana vya kuzingatia kwani hivyo huwa haviji na kupotea kama ambavyo pesa zinaweza.

wewe bana you have outgrown that fairy tale thing acha ligi a ubishi for the sake of ubishi, mambo ya snow white na cinderella tuyaache vitabuni
 
pesa muhimu katika mapenzi jamani tuacheni tamthilia.

da mbona vitufe vya thanks havijitokeze, nilitaka kukugongea thanks ya nguvu kwa kuusema ukweli kama ulivyo; ni vyema wanaume tuandaliwe toka tukiwa wadogo la sivyo tutaishia kujuta ukubwani, si umeona maneno hayo hapo juu ya kutoka kwenye john q - pesa ni muhimu sana
 
nakukabidhi hii mada, naona unaielewa kwa undani kuliko hata mimi, hebu mpige shule na nyani ngabu hapo maana naona analeta ubishi usio na tija japo kakiri mwenyewe humu kuwa asipobeba maboksi kabula atakula wapi

Wewe hueleweki! Weka mada yako vizuri ili usije kueleweka visivyo na ulivyokusudia. Unaposema pesa ndiyo msingi mkuu wa mapenzi wengine hatukuelewi kwa sababu tuna ndugu na tumeshawahi kuwa na ndugu ambao kwa kweli hawana na hawakuwa na chochote zaidi ya mapenzi ya kweli.

Wengine wameishi kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 50! Sasa ni wazi walikuwa hawashindi wala kulala njaa lakini pia hawakuwa na 'pesa'. Sasa pesa ndiyo msingi mkuu wa mapenzi...pesa kiasi gani? Za kutosha tu kujipatia mahitaji muhimu au nyingi za kusaza na kumwagia radhi?

Weka kiwango watu tujue unachokiongelea. Kama ni mshahara wa milioni kumi kwa mwezi sema, usiogope.
 
pesa muhimu katika mapenzi jamani tuacheni tamthilia.tena sisi wanawake bila kuwa na mwanamme mtoaji mara nyingi mahusiano hayawi sawa.mwanaume lazima awe mwanaume na uanaume wake uko kwenye izo p tatu

Pesa kiasi gani? Mbona mnaruka ruka tu kutoa generalities? Senti moja, milioni moja, au bilioni moja?
 
money is necessary but not sufficient/pesa ni lazima japo haijitoshelezi
 
Back
Top Bottom