Uchaguzi 2020 Umuhimu wa Mawakala wa Wagombea Urais, Ubunge na Udiwani kupatiwa nakala za matokeo ya uchaguzi katika vituo vya kupiga kura

KILA WAKALA WA MGOMBEA URAIS, UBUNGE NA UDIWANI KATIKA KITUO CHA KUPIGA KURA ANA HAKI YA KUPATIWA NAKALA YA FOMU YA MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS, MBUNGE NA DIWANI.

SEHEMU 1: UTANGULIZI.

Makala hii inaangazia haki ya kisheria ya wagombea Urais, Ubunge na Diwani kupatiwa Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais, Mbunge na Diwani kutoka kwa Wasimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura (Presiding Officers), Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi (Assistant Returning Officers) na Wasimamizi wa Uchaguzi (Returning Officers) pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Haki ya mawakala au wagombea kupatiwa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi hiko wazi sana bila utata wowote katika ngazi ya Taifa, Jimbo la Uchaguzi na Kata lakini haki hii imezungukwa na utata mkubwa sana wa kisheria katika ngazi ya Kituo cha Kupiga kura.

Haki ya mawakala wa wagombea Urais, ubunge na udiwani ya kupatiwa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi katika ngazi ya Kituo cha Kupiga Kura imezungukwa na utata mkubwa sana, hivyo, ufafanuzi wa kina unaitajika kuondoa utata huu

Hivyo basi, makala hii itajikita zaidi katika swala la haki ya wagombea Urais, ubunge na udiwani kupatiwa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi katika ngazi ya Kituo cha Kupiga Kura huku msisitizo mkubwa ukiwekwa katika nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na unyeti wa ofisi hii tukufu.

Utangulizi huu umegawanyika katika sehemu A na B kama ifuatavyo hapo chini.

[ A. ] ⛔ Umuhimu wa Nakala za Matokeo ya Uchaguzi Katika Uchaguzi Mkuu.

Mojawapo ya sifa ya Uchaguzi Huru na wa Haki ni kuwa na mfumo wa uchaguzi ambao ni wa uwazi, unaodhibitishika, unaokagulika, unaowajibika, salama, sahihi, rahisi, unaoaminika na unaofikika yaani kwa Kiingereza tunasema Election System which is transparent, verifiable, auditable, accountable, secure, accurate, simple, reliable, and accessible.

Sifa hizi za Uchaguzi Huru na wa Haki zimekubalika kimataifa na ni za viwango vya kimataifa na pia sifa hizi zinatambuliwa na Katiba na sheria za nchi kadhaa duniani ikiwemo Ibara ya 81 (e) na 86 ya Katiba ya Jamhuri ya Kenya, 2010 kama ilivyotafsiriwa na Mahakama ya Juu ya Kenya (Supreme Court of Kenya) na Mahakama ya Rufaa ya Kenya katika kesi zifuatazo;

(i) Raila Odinga Vs Uhuru Kenyatta & Others, Petition No. 5 of 2013

(ii) Raila Odinga & Another Vs Uhuru Kenyatta & Others, Petition No. 1 of 2017

(iii) National Super Alliance (NASA) Vs IEBC, AG & Jubilee Party, Civil Appeal No. 258 of 2017 (Mahakama ya Rufaa).

Pia, mwaka 2009, Mahakama ya Katiba ya Shirikisho la Ujerumani ya Seneti ya Pili (“Bundesverfassungsgericht") katika kesi ya muunganiko ya kikatiba (consolidated constitutional case) ambayo inafanyiwa rejea rasmi kama [BVerfG] 2 BvC 3/07 and 2 BvC 4/07 iliamua kuwa mfumo wa uchaguzi wa kielektroniki (Electronic Voting System) wa Ujerumani ni batili kisheria na kuupiga marufuku kutumika nchini Ujerumani kutokana na kukiuka Ibara ya 38, 20 (1) na 20 (2) ya Katiba ya Shirikisho la Ujerumani, 1949 ( Grundgesetz für die Bundesrepublik Deutschland ) kutokana na mfumo wa Uchaguzi wa kielektroniki kukosa sifa za kuwa na uwazi (transparency), uthibitishikaji (verifiability), kuaminika (reliability) na usalama (security) hususani usalama wa kimtandao (Cyber Security).

Ili mfumo wa uchaguzi uwe na uwazi , udhibitishike, ukagulike , uwajibike, uaminike, uwe salama na sahihi lazima wagombea wote wapatiwe nakala za matokeo katika ngazi zote kuanzia ngazi ya kituo cha kupiga kura, ngazi ya kata ngazi ya jimbo la uchaguzi na ngazi ya Taifa katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Hii ndo njia pekee inayoweza kufanya Election System kuwa transparent, verifiable, auditable, accountable, secure, reliable and accurate.

Swali ni je sheria za uchaguzi za Tanzania zinatoa haki kwa wagombea Urais, ubunge na udiwani kupatiwa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi katika ngazi zote? Hili ndo swali muhimu sana ambalo litajibiwa na makala hii.

[ B. ] ⛔ Haki ya Mgombea Kupatiwa Nakala za Matokeo ya Uchaguzi Katika Ngazi Zote.

Jibu ni ndio
, wagombea Urais, ubunge na udiwani wana haki ya kupatiwa nakala za matokeo ya uchaguzi katika ngazi zote kama ifuatavyo;

(a) Kila wakala wa Mgombea wa nafasi ya Urais, ubunge na udiwani ana haki ya kupatiwa nakala ya za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais, Mbunge na Diwani kutoka kwa Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura katika ngazi ya Kituo cha Kupiga Kura chini masharti ya Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020, Kanuni ya 56 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani, 2020 na Aya ya 9.19 ya Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020.

(b) Kila mgombea udiwani au wakala wake ana haki ya kupatiwa nakala ya fomu za matokeo ya uchaguzi wa diwani katika ngazi ya Kata kutoka kwa Msimamizi Msaadizi wa Uchaguzi chini masharti ya Kanuni ya 60 (1) (c) ya Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani, 2020.

(c) Kila mgombea ubunge au wakala wake ana haki ya kupatiwa nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa mbunge kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi katika ngazi ya Jimbo chini masharti ya Kanuni ya 69 (1) (c) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020.

(d) Kila mgombea Urais au wakala wake ana haki ya kupatiwa nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi katika ngazi ya Jimbo chini masharti ya Kanuni ya 67 (1) (b) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020.

(e) Kila mgombea Urais au wakala wake ana haki ya kupatiwa nakala ya matokeo ya uchaguzi wa Rais ngazi ya taifa kutoka kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini masharti ya Kanuni ya 68 (4) (c) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020.

SEHEMU 2: MSIMAMO SAHIHI WA SHERIA.

Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kila wakala wa mgombea Urais na ubunge alikuwa na haki ya kupatiwa nakala ya fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais. Sheria ilimtaka kwa lazima Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ( Presiding Officer ) kumpatia kila wakala wa mgombea Urais na ubunge nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais na mbunge kwa mujibu wa Kanuni ya 60 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 307 la 2015).

Katika Kanuni za Uchaguzi Rais na Wabunge za mwaka 2015 haki ya wakala wa mgombea Urais na ubunge kupatiwa nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais nambunge ilikuwa wazi na bayana sana bila utata wowote.

Lakini Katika Kanuni za Uchaguzi Rais na Wabunge za mwaka 2020 haki imepunguzwa makali kwa sababu kupewa nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais na mbunge imefanya kuwa hisani (privilege) kwa mujibu wa Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 ( Tangazo la Serikali Na. 402 la 2020) ambapo Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura anaweza kumpatia au kukataa kumpatia wakala wa mgombea Urais na ubunge nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi iwapo atajisika kufanya hivyo kwa kuwa hashurutishwi na sheria kutoa nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais na mbunge.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2020, Msimamizi wa Kituo "anaweza" kumpatia wakala wa mgombea Urais katika Kituo cha kupiga kura nakala ya fomu ya matokea ya uchaguzi wa Rais au mbunge "iwapo kuna nakala za kutosha za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais au mbunge", hii ni kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 402 la 2020).

Kutoka na matumizi ya neno "anaweza" (may) katika Kanuni ya 63 (2) tajwa hapo juu, kisheria inamaanisha kuwa Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ana hiyari (discretion) ya kumpatia au kukataa kumpatia wakala wa mgombea Urais au ubunge katika Kituo cha kupiga kura nakala ya fomu ya matokea ya uchaguzi wa Rais au mbunge.

Sababu ya hiyari (discretion) hii ya Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura inatokana na matumizi ya neno "anaweza" (may) katika sheria kwa msingi kwamba neno hili linapotumika katika sheria limaanisha kuwa mtu ana hiyari kufanya au hiyari ya kukataa kufanya kitu ambacho sheria inasema kifanyike (discretionary power), hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 52 (1) cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1 kama kilivyotafsiriwa na Mahakama Kuu katika kesi ya Laula Edmund Vs Barke Ahmed Said, PC Civil Appeal No. 1 of 2020.

Kwa maneno mengine, ni kwamba kwa mujibu wa Kanuni ya 63 (2) tajwa hapo juu, Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ana mamlaka ya hiyari (discretionary power) ya kukataa kumpatia wakala wa mgombea Urais katika Kituo cha Kupiga Kura nakala ya fomu ya matokea ya uchaguzi wa Rais au mbunge hata kama kuna nakala za kutosha za matokeo ya uchaguzi wa Rais au mbunge.

Hatahivyo, Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 inakinzana na masharti ya Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 ambacho kinaelekeza kwa lazima kwa kutumia kitenzi kisaidizi "ata" (shall) kuwa iwapo kuna nakala za kutosha lazima Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ampatie wakala wa mgombea Urais au ubunge katika Kituo cha kupiga kura nakala ya fomu ya matokea ya uchaguzi wa Rais.

Kwa maneno mengine, ni kwamba kwa mujibu wa Kifungu cha 79 A (1) (e) tajwa hapo juu, Msimamizi wa Kituo cha kupiga analazimishwa na sheria bila hiyari yake kumpatia wakala wa mgombea Urais katika Kituo cha kupiga kura nakala yafomu ya matokea ya uchaguzi wa Rais iwapo kuna nakala za kutosha za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais au mbunge.

Kama kuna nakala za kutosha lazima Msimamizi wa Kituo cha kupiga ampatie wakala wa mgombea Urais au ubunge nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa sababu kitenzi kisaidizi "ata" (shall) kinapotumika katika sheria kinamaanisha kuwa mtu hana kabisa hiyari bali ni lazima afanye kama alivyoelekezwa na sheria (mandatory duty), hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 52 (2) cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1 kama kilivyotafsiriwa na Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Shaaban Iddi Jololo and 3 others Vs Republic Criminal Appeal No. 200 of 2006.

Iwapo Sheria Ndogo Ndogo (subsidiary legislation) iliyotungwa na mamlaka iliyokasimishwa (delegated) mamlaka ya kutunga sheria na bunge "inakinzana" na Sheria Kuu (principal legislation) iliyotungwa na bunge lenyewe basi Sheria Ndogo Ndogo inakuwa batili tangia mwanzo (null and void ab initio) kwa kiwango ambacho Sheria Ndogo Ndogo inakinzana na Sheria Kuu iliyotungwa na bunge, haya ndo matakwa ya masharti ya Kifungu cha 36 (1) cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1 kama kilivyotafsiri na Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Morogoro Hunting Safaris Ltd. Vs Halima Mohamed Mamuya, Civil Appeal No. 117 of 2011 na pia huu msimamo wa sheria uliwekwa na Mahakama zaidi ya miaka 80 iliyopita katika kesi ya Nanal Damodar Kanji Vs Tanga Township Authority [1940] 1 T.L.R. 239.

Kirai "Sheria Ndogo Ndogo" (subsidiary legislation) kimetafsiri na Kifungu cha 4 ya Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1, pamoja na mambo mengine kumaanisha A, Maelekezo, Kanuni, Notisi na Tamko ambalo limetungwu chini ya mamlaka ya sheria iliyotungwa na bunge au mamlaka nyingine ya kisheria, hivyo, basi, kisheria Kanuni ni sheria Sheria Ndogo Ndogo.

Tume ya Taifa Uchaguzi imekasimishwa (delegated) na bunge Mamlaka ya kutunga Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge chini ya Kifungu cha 124 cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 ambazo kisheria ni sheria ndogo ndogo.

Kwa msingi huu basi, iwapo Kanuni za Uchaguzi zilizotungwa na Tume ya Taifa Uchaguzi zinakinzana na Sheria Kuu ya Uchaguzi iliyotungwa na bunge basi Kanuni za Uchaguzi ambazo zimetungwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinakuwa batili tangia mwanzo (null and void ab initio) kwa kiwango ambacho zinakinzana na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, haya ndo matakwa ya masharti ya Kifungu cha 36 (1) cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1.

Hivyo basi, msimamo sahihi wa sheria sio ule ambao umeelekezwa kwenye Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 kwa sababu msimamo wa sheria ambao umeelekezwa na Kanuni ya 63 (2) tajwa hapo juu ni batili tangia mwanzo kwa kukinzana na Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Hivyo basi, msimamo sahihi wa sheria (correct position of law) ni kama ulivyoelekezwa kwenye masharti ya Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 kwamba kama kuna nakala za kutosha "lazima" Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ampatie wakala wa mgombea Urais au mbunge nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais au mbunge.

Swali muhimu hapa ni je kutakuwepo nakala za kutosha za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais na mbunge katika Kituo cha Kupiga Kura? Jibu la swali hili linapatikana sehemu inayofuatia hapo chini baada ya sehemu yaani Sehemu ya 3.

SEHEMU 3: JE KUTAKUWEPO NA NAKALA ZA KUTOSHA ZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KATIKA KITUO CHA KUPIGA KURA?

Jibu ni ndio.

Ndio kisheria lazima kuwepo na nakala za kutosha za matokeo ya uchaguzi wa Rais katika Kituo cha Kupiga Kura kwa sababu ambazo nitazielezea hapa chini.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa mamlaka ya kutunga au kutengeneza Maelekezo ya Uchaguzi (Election Directives) yenye nguvu ya kisheria chini ya Kifungu cha 126 cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 na chini ya Kanuni ya 79 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitengeneza Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020 ambayo yanataja idadi ya nakala za matokeo ya uchaguzi wa Rais na mbunge ambazo zinapashwa kuwepo katika Kituo cha Kupiga Kura.

🟧 A. UTOSHELEVU WA NAKALA ZA FOMU ZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS.

Aya ya 9.19 ya Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020
inaelekeza kwa lazima kuwa kila Kituo cha Kupiga Kura lazima kiwe na Kitabu cha Fomu za Matokeo ya Uchaguzi Rais chenye "nakala 24" za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ( Fomu 21 A ) ambazo zitagawiwa kama ifuatayo;

(1) Nakala ya Kwanza ya Fomu ya Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ambayo iko ukrasa wa 1 wa Kitabu cha Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais atapewa Msimamizi wa Uchaguzi (Returning Officer) ngazi ya jimbo. Nakala ya kwanza ni nakala halisi (original copy).

(2) Nakala ya Pili ya Fomu ya Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ambayo iko ukrasa wa 2 wa Kitabu cha Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais itabandikwa ukutani na Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura katika Kituo cha Kupiga Kura husika kwa ajiri ya kuwajulisha wananchi au umma wa Watanzania matokeo ya Uchaguzi wa Rais katika Kituo husika. Nakala ya Pili sio nakala halisi bali ni nakala rudufu (photocopy) ambayo inarudufiwa kutoka katika nakala halisi yaani nakala ya kwanza.

(3) Nakala ya Kumi na Tatu (13) ya Fomu ya Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ambayo iko ukrasa wa 13 wa Kitabu cha Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais itapewa Tume Taifa ya Uchaguzi kwa ajiri ya matumizi yake ya kiofisi. Nakala ya 13 nayo ni nakala halisi (original copy).

(4) Kuanzia Nakala ya 3 na kuendelea (consecutively) mpaka Nakala ya 24 katika Kitabu cha Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ambazo ziko kuanzia ukrasa wa 3 na kuendelea mpaka ukrasa wa 24 wa Kitabu tajwa hapo juu watapewa mawakala wa wagombea Urais kulingana na idadi yao isipokuwa Nakala ya 13 ambayo itakuwa Nakala ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kwa kuwa kuna wagombea Urais 15, hivyo, basi mawakala wa wagombea Urais katika Kituo cha Kupiga Kura watapewa kuanzia nakala ya 3 mpaka ya nakala 18 isipokuwa nakala ya 13 ambayo itapewa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Pia, isipokuwa nakala ya 13, kuanzia Nakala ya 2 na kuendelea mpaka nakala ya 24 ni nakala zilizorudufiwa (photocopies) kutoka katika nakala halisi yaani nakala ya 1 na 13 na sio nakala halisi (original copy).

Nakala ya 3 kati ya nakala 24 ni kwa ajiri ya matumizi ya kiofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa maana ya Nakala ya 1, 2 na 13.

Fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais katika kituoni cha Kupiga Kura ambayo ni Fomu Na. 21 A iko kwenye umbo la kitabu ambacho kitakuwa na kurasa ishirini na nne (24) ambapo nakala 12 za awali zimetenganishwa na nakala 12 za mwisho kwa karatasi ngumu (separator). Nakala 12 za mwisho zinaanzia ukrasa wa 13 mpaka ukrusa wa 24 yaani ni kuanzia nakala ya 13 na kuendelea mpaka nakala ya 24.

Karatasi za Fomu Na. 21 A zimetayarishwa katika namna ambayo inawezesha kuandika na kutoa nakala rudufu (photocopies) bila kuweka karatasi ya kaboni (Carbon Papers) yaani ni "Self copying".

Hivyo basi, kila kituo cha kupiga kura kinatakiwa kuwa na nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais ( Form 21 A ) zisizopungua Nakala 24 , basi kwa kuwa wagombea Urais ni watu 15 ambao watapewa nakala 15 za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais na Tume ya Taifa ya Uchaguzi itapewa nakala 3 za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi Rais, hivyo, zitabaki nakala 6 za fomu za matokea ya uchaguzi wa Rais za ziada ambazo hazitatumika.

Kutokana na uchambuzi wa hapo juu basi kisheria lazima zitakuwepo nakala 24 za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais katika Kituo cha Kupiga Kura ambazo zinatosha kuwapatia mawakala wote 15 wa wagombea Urais 15 wote.

🟧 B. UTOSHELEVU WA NAKALA ZA FOMU ZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA MBUNGE NA DIWANI.

🔹 (a) Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Mbunge.

Utaratibu na masharti ya kisheria yanayotumika katika kutoa nakala za fomu za matokeo uchaguzi wa Rais kwa mawakala wa wagombea Urais katika Kituo cha Kupiga Kura unafanana karibu kwa kila kitu na utaratibu na masharti yanayotumika katika kutoa nakala za fomu za matokeo uchaguzi wa wabunge kwa mawakala wa wagombea ubunge na sheria inayotumika ni moja.

Hivyo basi, kutakuwepo na nakala 24 za fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa mbunge kwenye kila Kituo cha Kupiga Kura. Kati ya nakala 24 za Matokeo ya Uchaguzi wa mbunge, nakala 21 zitakuwa kwa ajiri ya kuwapatia mawakala wa wagombea ubunge katika Jimbo la Uchaguzi husika. Na nakala 3 zitakuwa kwa ajiri ya matumizi ya kiofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Mojawapo ya nakala kati ya nakala 3 tajwa hapo juu itakuwemo nakala moja (1) ya matokeo ya uchaguzi wa mbunge kwa ajiri ya kubandika katika ukuta wa Kituo cha Kupiga Kura kuutaarifu umma wa Watanzania na wapiga kura matokeo ya Uchaguzi wa mbunge katika Kituo husika.

Hatahivyo, nakala za matokeo ya uchaguzi wa mbunge katika Kituo cha Kupiga Kura zitakuwa kwenye Fomu Na. 21 B.

🔹 (b) Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Diwani.

Kwenye uchaguzi wa diwani sheria zinazotumika katika mchakato wa kutoa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa diwani katika Kituo cha Kupiga Kura kwa upande moja ni tofauti na sheria zinazotumika kwenye Uchaguzi Rais na mbunge kwa upande mwingine isipokuwa Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020 ambayo yatumika katika uchaguzi wa madiwani pamoja na Uchaguzi wa Rais na wabunge.

Sheria zinazotumika kwa upande wa uchaguzi wa udiwani katika kutoka nakala za matokeo ya uchaguzi wa diwani ni hizi zifuatazo;

(i) Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura 292

(ii) Kanuni ya Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani, 2020

(iii) Aya ya 9.19 ya Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020.

Hatahivyo, pamoja na utofauti wa sheria bado utaratibu na masharti ya kisheria yanayotumika katika kutoa nakala za fomu za matokeo uchaguzi wa diwani kwa mawakala katika Kituo cha Kupiga Kura kwa upande mmoja unafanana karibu kwa kila kitu na utaratibu na masharti ya kisheria yanayotumika kwa wagombea wa nafasi ya Rais na nafasi ya mbunge kwa upande mwingine.

Isipokuwa nakala za matokeo ya uchaguzi wa diwani katika Kituo cha Kupiga Kura yanakuwa kwenye Fomu 21 C.

SEHEMU 4: NI LAZIMA MAWAKALA KUPATIWA NAKALA YA MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS.

Kisheria ni lazima Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ampatie kila wakala wa mgombea Urais nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais ambayo ni Fomu Na. 21 A kwa sababu nne zifuatazo:

🔴 (1) Masharti ya Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 yanaelekeza kwa lazima kwamba iwapo kuna nakala za kutosha za fomu za matokeo ya Rais basi ni "lazima" Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ampatie kila wakala wa mgombea Urais nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais ya Kituo cha Kupiga Kura.

(2) Aya ya 9.19 ya Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020 inaelekeza kwa lazima kuwa kila Kituo cha Kupiga Kura lazima kiwe na Kitabu cha Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais chenye "nakala 24" za fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ( Fomu Na. 21 A ) na kati ya nakala 24 tajwa hapo juu, nakala 21 ni kwa ajiri kuwapatia mawakala wa wagombea Urais ili wazipeleke kwa wagombea Urais na vyama vyao vya siasa ambavyo wanawakilisha katika Kituo cha Kupiga Kura.

🔴 (3) Kwa kuwa kisheria lazima ziwepo nakala 21 za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa ajiri ya kuwapatia mawakala wa wagombea Urais ili wazipeleke kwa wagombea Urais na vyama vyao vya siasa basi kutakuwepo na nakala za kutosha kuwapatia mawakala 15 wa wagombea Urais 15 ambao wameteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kugombea nafasi ya Rais katika uchaguzi mkuu wa 2020.

🔴 (4) Kwa kuwa kutakuwepo na nakala 21 za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais ambazo zinatosha kuwapatia mawakala 15 wa wagombea Urais 15 basi Wasimamizi wa Vituo vya Kupiga Kura lazima wawapatie nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais mawakala wote wa wagombea Urais kama inavyoelekezwa kwa lazima na masharti ya Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 kwamba iwapo kuna nakala za kutosha "lazima" Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura awapatie wakala wote wa wagombea Urais nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais.

Pia, Kisheria ni lazima Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ampatie kila wakala wa mgombea Ubunge na udiwani nakala ya matokeo ya uchaguzi wa mbunge na diwani ambayo ni Fomu Na. 21 A na Fomu 21 C mtawalia (respectively) kwa sababu nne ambazo zimetajwa hapo juu kwa kufanya mabadiliko muhimu hapo juu (mutatis mutandis).

SEHEMU 5: HITIMISHO.

Wagombea wa nafasi ya Urais, ubunge na udiwani wana haki ya kupatiwa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi katika ngazi zote za kiuchaguzi kuanzia ngazi ya kituo cha kupiga kura, ngazi ya Kata, ngazi na Jimbo la Uchaguzi mpaka ngazi ya Taifa kutoka kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hivyo basi, ni raia yangu kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi pamoja na Wasimamizi wa Vituo vya Kupiga Kura kuheshimu sheria za Uchaguzi za nchi hii kwa kuwapatia Wagombea Urais, ubunge na udiwani au mawakala wao haki yao ya kisheria ya kupatiwa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi Rais, Mbunge na Diwani katika ngazi zote za kiuchaguzi ili kufanikisha kufanyika kwa uchaguzi Huru na wa Haki ambao una uwazi na unakagulika, unadhibitishika, unawajibika, sahihi na salama.

Kutoa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais, wabunge na Madiwani kwa wagombea au mawakala wa wagombea katika Kituo cha Kupiga Kura na katika vituo vya kujumlisha matokeo ya uchaguzi katika ngazi ya Kata, Jimbo la Uchaguzi na ngazi ya Taifa kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi utaondoa kwa sehemu kubwa tuhuma za wizi wa kura na tuhuma za hujuma za Uchaguzi Mkuu na kufanya matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2020 kuwa ya kuaminika, kuheshimike na kukubalika kwa wagombea wote, vyama vyote vya Siasa, wapiga kura wote, watazamaji wa ndani na wa kimataifa wote na wadau wote wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

imeandikwa na Matojo M. Cosatta, (Senior JF Member).
Kwenye hii nchi kuna watu wameamua kuwapeleka wengine namna wanavyo taka wao tu kama vile nchi ni mali yao binafsi.
Yaani ukianzia katiba, sheria, kanuni na utaratibu vyote wamechakachua kwa maslahi yao badala ya nchi.
Nchi nyingi zilizo ingia kwenye mizozo sababu kuu ni kuharibu/kutofuata vitu muhimu kama hivi katika suala zima la kuiongoza nchi.
 
Mtoa mada kuhusu kutolewa kwa nakala ya fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ameamua kwa makusudi kupotosha maana halisi ya kifungu cha 79A(1)(e) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kanuni ya 67(1)(b) ya kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020.

Nakushauri usome Sheria kwa ujumla wake na si kusoma in “isolation”. Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, kifungu cha 79A (1) (e) inasomeka, 79(1) “upon conclusion of the counting of the votes in accordance with section 73, the Presiding Officer shall- (e) if available in sufficient number; give each polling agent a copy of the report of results;”
Maana yake ni kwamba Msimamizi wa Kituo (Presiding Officer) “ata” (shall) atampatia kila wakala nakala ya fomu ya matokeo, “if” kama zipo za kutosha. Hii ni sheria mama. kwanini umeruka neno “if” makusudi ili apotoshe umma?? pasipo na sababu za msingi za kufanya hivyo??
 
Mapungufu ya uzi huu yako bayana
 
Ikumbukwe kwamba vyama vya Siasa ni wadau wakubwa wa NEC hushirikishwa katika utungaji wa Kanuni, Hivyo hata utolewaji wa Maoni na kupitishwa kwa kanuni hiyo ni Matokeo ya kikao cha NEC na wadau wake.

Andiko hili pamoja na mambo mengi. Lina mapungufu!!

Sheria ndogo (kanuni za Uchaguzi) zimeelez,a kanuni ya 67(1)(b) -“67(1) The Returning Officer shall after the addition of votes for Presidential election- (b) issue to every candidate or his agent a copy of Form No. 24A.

Kanuni inamtaka Msimamizi wa Uchaguzi kumpatia mgombea au wakala wake nakala ya fomu ya matokeo.
Mtoa mada anapotosha kwa makusudi. Hii inaonesha mambo mawili-
(i) Hana ufahamu na uelewa wa kutosha kuhusu Sheria za Uchaguzi na kanuni zake; au
(ii) Hana nia njema na mchakato wa uchaguzi.

Namshauri akasome upya kifungu cha 79(A)(1)(e) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kanuni ya 67(1)(b) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020, kwa utulivu ili aelewe.
Kwa taaluma yake ya kama sheria, naamini mtoa mada ameenda kwa mwendokasi kuzidi lengo la Sheria na kanuni husika.
 
Mapungufu ya uzi huu yako bayana

Pia Sheria ndogo (kanuni za Uchaguzi) zimeelez,a kanuni ya 67(1)(b) -“67(1) The Returning Officer shall after the addition of votes for Presidential election- (b) issue to every candidate or his agent a copy of Form No. 24A.

Kanuni inamtaka Msimamizi wa Uchaguzi kumpatia mgombea au wakala wake nakala ya fomu ya matokeo.
Mtoa mada anapotosha kwa makusudi. Hii inaonesha mambo mawili-
(i) Hana ufahamu na uelewa wa kutosha kuhusu Sheria za Uchaguzi na kanuni zake; au
(ii) Hana nia njema na mchakato wa uchaguzi.

Namshauri akasome upya kifungu cha 79(A)(1)(e) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kanuni ya 67(1)(b) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020, kwa utulivu ili aelewe.
Kwa taaluma yake ya kama sheria, naamini mtoa mada ameenda kwa mwendokasi kuzidi lengo la Sheria na kanuni husika.
 
Mtoa mada kuhusu kutolewa kwa nakala ya fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ameamua kwa makusudi kupotosha maana halisi ya kifungu cha 79A(1)(e) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kanuni ya 67(1)(b) ya kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020.

Nakushauri usome Sheria kwa ujumla wake na si kusoma in “isolation”. Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, kifungu cha 79A (1) (e) inasomeka, 79(1) “upon conclusion of the counting of the votes in accordance with section 73, the Presiding Officer shall- (e) if available in sufficient number; give each polling agent a copy of the report of results;”
Maana yake ni kwamba Msimamizi wa Kituo (Presiding Officer) “ata” (shall) atampatia kila wakala nakala ya fomu ya matokeo, “if” kama zipo za kutosha. Hii ni sheria mama. kwanini umeruka neno “if” makusudi ili apotoshe umma?? pasipo na sababu za msingi za kufanya hivyo??

Huu utopolo ulioandika ni ushahidi wa wazi kwa Mwanasheria yoyote anayejua kwa kina sheria uchaguzi kujua kwa haraka sana kuwa uelewa wako kuhusu maswala ya sheria za Uchaguzi ni mdogo sana.

Kwa sasa niko busy lakini baadae nitakujibu mpaka wewe mwenye utajiona mjinga sana wa swala hili.
 
Sheria ndogo (kanuni za Uchaguzi) zimeelez,a kanuni ya 67(1)(b) -“67(1) The Returning Officer shall after the addition of votes for Presidential election- (b) issue to every candidate or his agent a copy of Form No. 24A.

Kanuni inamtaka Msimamizi wa Uchaguzi kumpatia mgombea au wakala wake nakala ya fomu ya matokeo.
Mtoa mada anapotosha kwa makusudi. Hii inaonesha mambo mawili-
(i) Hana ufahamu na uelewa wa kutosha kuhusu Sheria za Uchaguzi na kanuni zake; au
(ii) Hana nia njema na mchakato wa uchaguzi.

Namshauri akasome upya kifungu cha 79(A)(1)(e) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kanuni ya 67(1)(b) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020, kwa utulivu ili aelewe.
Kwa taaluma yake ya kama sheria, naamini mtoa mada ameenda kwa mwendokasi kuzidi lengo la Sheria na kanuni husika.

Wewe ndo hauna ufahamu ndo maana umeshindwa kutofautisha kati ya Returning Officer na Presiding Officer, hivi ni vyeo viwili tofauti kabisa kwenye sheria.

Baade nikipata muda nitakujibu nikioneshe jinsi ulivyo mjinga wa sheria za Uchaguzi.
 
Huu utopolo ulioandika ni ushahidi wa wazi kwa Mwanasheria yoyote anayejua kwa kina sheria uchaguzi kujua kwa haraka sana kuwa uelewa wako kuhusu maswala ya sheria za Uchaguzi ni mdogo sana.

Kwa sasa niko busy lakini baadae nitakujibu mpaka wewe mwenye utajiona mjinga sana wa swala hili.
Kenge kabisa wewe. Ulamwambia mtu uelewa wake ni mdogo. Halafu huna JUSTIFICATION za kukosoa hoja zake?
Bure kabisa Wewe!!
 
KILA WAKALA WA MGOMBEA URAIS, UBUNGE NA UDIWANI KATIKA KITUO CHA KUPIGA KURA ANA HAKI YA KUPATIWA NAKALA YA FOMU YA MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS, MBUNGE NA DIWANI.

SEHEMU 1: UTANGULIZI.

Makala hii inaangazia haki ya kisheria ya wagombea Urais, Ubunge na Diwani kupatiwa Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais, Mbunge na Diwani kutoka kwa Wasimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura (Presiding Officers), Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi (Assistant Returning Officers) na Wasimamizi wa Uchaguzi (Returning Officers) pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Haki ya mawakala au wagombea kupatiwa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi hiko wazi sana bila utata wowote katika ngazi ya Taifa, Jimbo la Uchaguzi na Kata lakini haki hii imezungukwa na utata mkubwa sana wa kisheria katika ngazi ya Kituo cha Kupiga kura.

Haki ya mawakala wa wagombea Urais, ubunge na udiwani ya kupatiwa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi katika ngazi ya Kituo cha Kupiga Kura imezungukwa na utata mkubwa sana, hivyo, ufafanuzi wa kina unaitajika kuondoa utata huu

Hivyo basi, makala hii itajikita zaidi katika swala la haki ya wagombea Urais, ubunge na udiwani kupatiwa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi katika ngazi ya Kituo cha Kupiga Kura huku msisitizo mkubwa ukiwekwa katika nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na unyeti wa ofisi hii tukufu.

Utangulizi huu umegawanyika katika sehemu A na B kama ifuatavyo hapo chini.

[ A. ] ⛔ Umuhimu wa Nakala za Matokeo ya Uchaguzi Katika Uchaguzi Mkuu.

Mojawapo ya sifa ya Uchaguzi Huru na wa Haki ni kuwa na mfumo wa uchaguzi ambao ni wa uwazi, unaodhibitishika, unaokagulika, unaowajibika, salama, sahihi, rahisi, unaoaminika na unaofikika yaani kwa Kiingereza tunasema Election System which is transparent, verifiable, auditable, accountable, secure, accurate, simple, reliable, and accessible.

Sifa hizi za Uchaguzi Huru na wa Haki zimekubalika kimataifa na ni za viwango vya kimataifa na pia sifa hizi zinatambuliwa na Katiba na sheria za nchi kadhaa duniani ikiwemo Ibara ya 81 (e) na 86 ya Katiba ya Jamhuri ya Kenya, 2010 kama ilivyotafsiriwa na Mahakama ya Juu ya Kenya (Supreme Court of Kenya) na Mahakama ya Rufaa ya Kenya katika kesi zifuatazo;

(i) Raila Odinga Vs Uhuru Kenyatta & Others, Petition No. 5 of 2013

(ii) Raila Odinga & Another Vs Uhuru Kenyatta & Others, Petition No. 1 of 2017

(iii) National Super Alliance (NASA) Vs IEBC, AG & Jubilee Party, Civil Appeal No. 258 of 2017 (Mahakama ya Rufaa).

Pia, mwaka 2009, Mahakama ya Katiba ya Shirikisho la Ujerumani ya Seneti ya Pili (“Bundesverfassungsgericht") katika kesi ya muunganiko ya kikatiba (consolidated constitutional case) ambayo inafanyiwa rejea rasmi kama [BVerfG] 2 BvC 3/07 and 2 BvC 4/07 iliamua kuwa mfumo wa uchaguzi wa kielektroniki (Electronic Voting System) wa Ujerumani ni batili kisheria na kuupiga marufuku kutumika nchini Ujerumani kutokana na kukiuka Ibara ya 38, 20 (1) na 20 (2) ya Katiba ya Shirikisho la Ujerumani, 1949 ( Grundgesetz für die Bundesrepublik Deutschland ) kutokana na mfumo wa Uchaguzi wa kielektroniki kukosa sifa za kuwa na uwazi (transparency), uthibitishikaji (verifiability), kuaminika (reliability) na usalama (security) hususani usalama wa kimtandao (Cyber Security).

Ili mfumo wa uchaguzi uwe na uwazi , udhibitishike, ukagulike , uwajibike, uaminike, uwe salama na sahihi lazima wagombea wote wapatiwe nakala za matokeo katika ngazi zote kuanzia ngazi ya kituo cha kupiga kura, ngazi ya kata ngazi ya jimbo la uchaguzi na ngazi ya Taifa katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Hii ndo njia pekee inayoweza kufanya Election System kuwa transparent, verifiable, auditable, accountable, secure, reliable and accurate.

Swali ni je sheria za uchaguzi za Tanzania zinatoa haki kwa wagombea Urais, ubunge na udiwani kupatiwa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi katika ngazi zote? Hili ndo swali muhimu sana ambalo litajibiwa na makala hii.

[ B. ] ⛔ Haki ya Mgombea Kupatiwa Nakala za Matokeo ya Uchaguzi Katika Ngazi Zote.

Jibu ni ndio
, wagombea Urais, ubunge na udiwani wana haki ya kupatiwa nakala za matokeo ya uchaguzi katika ngazi zote kama ifuatavyo;

(a) Kila wakala wa Mgombea wa nafasi ya Urais, ubunge na udiwani ana haki ya kupatiwa nakala ya za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais, Mbunge na Diwani kutoka kwa Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura katika ngazi ya Kituo cha Kupiga Kura chini masharti ya Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020, Kanuni ya 56 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani, 2020 na Aya ya 9.19 ya Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020.

(b) Kila mgombea udiwani au wakala wake ana haki ya kupatiwa nakala ya fomu za matokeo ya uchaguzi wa diwani katika ngazi ya Kata kutoka kwa Msimamizi Msaadizi wa Uchaguzi chini masharti ya Kanuni ya 60 (1) (c) ya Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani, 2020.

(c) Kila mgombea ubunge au wakala wake ana haki ya kupatiwa nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa mbunge kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi katika ngazi ya Jimbo chini masharti ya Kanuni ya 69 (1) (c) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020.

(d) Kila mgombea Urais au wakala wake ana haki ya kupatiwa nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi katika ngazi ya Jimbo chini masharti ya Kanuni ya 67 (1) (b) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020.

(e) Kila mgombea Urais au wakala wake ana haki ya kupatiwa nakala ya matokeo ya uchaguzi wa Rais ngazi ya taifa kutoka kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini masharti ya Kanuni ya 68 (4) (c) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020.

SEHEMU 2: MSIMAMO SAHIHI WA SHERIA.

Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kila wakala wa mgombea Urais na ubunge alikuwa na haki ya kupatiwa nakala ya fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais. Sheria ilimtaka kwa lazima Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ( Presiding Officer ) kumpatia kila wakala wa mgombea Urais na ubunge nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais na mbunge kwa mujibu wa Kanuni ya 60 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 307 la 2015).

Katika Kanuni za Uchaguzi Rais na Wabunge za mwaka 2015 haki ya wakala wa mgombea Urais na ubunge kupatiwa nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais nambunge ilikuwa wazi na bayana sana bila utata wowote.

Lakini Katika Kanuni za Uchaguzi Rais na Wabunge za mwaka 2020 haki imepunguzwa makali kwa sababu kupewa nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais na mbunge imefanya kuwa hisani (privilege) kwa mujibu wa Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 ( Tangazo la Serikali Na. 402 la 2020) ambapo Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura anaweza kumpatia au kukataa kumpatia wakala wa mgombea Urais na ubunge nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi iwapo atajisika kufanya hivyo kwa kuwa hashurutishwi na sheria kutoa nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais na mbunge.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2020, Msimamizi wa Kituo "anaweza" kumpatia wakala wa mgombea Urais katika Kituo cha kupiga kura nakala ya fomu ya matokea ya uchaguzi wa Rais au mbunge "iwapo kuna nakala za kutosha za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais au mbunge", hii ni kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 402 la 2020).

Kutoka na matumizi ya neno "anaweza" (may) katika Kanuni ya 63 (2) tajwa hapo juu, kisheria inamaanisha kuwa Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ana hiyari (discretion) ya kumpatia au kukataa kumpatia wakala wa mgombea Urais au ubunge katika Kituo cha kupiga kura nakala ya fomu ya matokea ya uchaguzi wa Rais au mbunge.

Sababu ya hiyari (discretion) hii ya Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura inatokana na matumizi ya neno "anaweza" (may) katika sheria kwa msingi kwamba neno hili linapotumika katika sheria limaanisha kuwa mtu ana hiyari kufanya au hiyari ya kukataa kufanya kitu ambacho sheria inasema kifanyike (discretionary power), hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 52 (1) cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1 kama kilivyotafsiriwa na Mahakama Kuu katika kesi ya Laula Edmund Vs Barke Ahmed Said, PC Civil Appeal No. 1 of 2020.

Kwa maneno mengine, ni kwamba kwa mujibu wa Kanuni ya 63 (2) tajwa hapo juu, Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ana mamlaka ya hiyari (discretionary power) ya kukataa kumpatia wakala wa mgombea Urais katika Kituo cha Kupiga Kura nakala ya fomu ya matokea ya uchaguzi wa Rais au mbunge hata kama kuna nakala za kutosha za matokeo ya uchaguzi wa Rais au mbunge.

Hatahivyo, Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 inakinzana na masharti ya Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 ambacho kinaelekeza kwa lazima kwa kutumia kitenzi kisaidizi "ata" (shall) kuwa iwapo kuna nakala za kutosha lazima Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ampatie wakala wa mgombea Urais au ubunge katika Kituo cha kupiga kura nakala ya fomu ya matokea ya uchaguzi wa Rais.

Kwa maneno mengine, ni kwamba kwa mujibu wa Kifungu cha 79 A (1) (e) tajwa hapo juu, Msimamizi wa Kituo cha kupiga analazimishwa na sheria bila hiyari yake kumpatia wakala wa mgombea Urais katika Kituo cha kupiga kura nakala yafomu ya matokea ya uchaguzi wa Rais iwapo kuna nakala za kutosha za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais au mbunge.

Kama kuna nakala za kutosha lazima Msimamizi wa Kituo cha kupiga ampatie wakala wa mgombea Urais au ubunge nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa sababu kitenzi kisaidizi "ata" (shall) kinapotumika katika sheria kinamaanisha kuwa mtu hana kabisa hiyari bali ni lazima afanye kama alivyoelekezwa na sheria (mandatory duty), hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 52 (2) cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1 kama kilivyotafsiriwa na Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Shaaban Iddi Jololo and 3 others Vs Republic Criminal Appeal No. 200 of 2006.

Iwapo Sheria Ndogo Ndogo (subsidiary legislation) iliyotungwa na mamlaka iliyokasimishwa (delegated) mamlaka ya kutunga sheria na bunge "inakinzana" na Sheria Kuu (principal legislation) iliyotungwa na bunge lenyewe basi Sheria Ndogo Ndogo inakuwa batili tangia mwanzo (null and void ab initio) kwa kiwango ambacho Sheria Ndogo Ndogo inakinzana na Sheria Kuu iliyotungwa na bunge, haya ndo matakwa ya masharti ya Kifungu cha 36 (1) cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1 kama kilivyotafsiri na Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Morogoro Hunting Safaris Ltd. Vs Halima Mohamed Mamuya, Civil Appeal No. 117 of 2011 na pia huu msimamo wa sheria uliwekwa na Mahakama zaidi ya miaka 80 iliyopita katika kesi ya Nanal Damodar Kanji Vs Tanga Township Authority [1940] 1 T.L.R. 239.

Kirai "Sheria Ndogo Ndogo" (subsidiary legislation) kimetafsiri na Kifungu cha 4 ya Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1, pamoja na mambo mengine kumaanisha A, Maelekezo, Kanuni, Notisi na Tamko ambalo limetungwu chini ya mamlaka ya sheria iliyotungwa na bunge au mamlaka nyingine ya kisheria, hivyo, basi, kisheria Kanuni ni sheria Sheria Ndogo Ndogo.

Tume ya Taifa Uchaguzi imekasimishwa (delegated) na bunge Mamlaka ya kutunga Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge chini ya Kifungu cha 124 cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 ambazo kisheria ni sheria ndogo ndogo.

Kwa msingi huu basi, iwapo Kanuni za Uchaguzi zilizotungwa na Tume ya Taifa Uchaguzi zinakinzana na Sheria Kuu ya Uchaguzi iliyotungwa na bunge basi Kanuni za Uchaguzi ambazo zimetungwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinakuwa batili tangia mwanzo (null and void ab initio) kwa kiwango ambacho zinakinzana na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, haya ndo matakwa ya masharti ya Kifungu cha 36 (1) cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura ya 1.

Hivyo basi, msimamo sahihi wa sheria sio ule ambao umeelekezwa kwenye Kanuni ya 63 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 kwa sababu msimamo wa sheria ambao umeelekezwa na Kanuni ya 63 (2) tajwa hapo juu ni batili tangia mwanzo kwa kukinzana na Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Hivyo basi, msimamo sahihi wa sheria (correct position of law) ni kama ulivyoelekezwa kwenye masharti ya Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 kwamba kama kuna nakala za kutosha "lazima" Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ampatie wakala wa mgombea Urais au mbunge nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais au mbunge.

Swali muhimu hapa ni je kutakuwepo nakala za kutosha za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais na mbunge katika Kituo cha Kupiga Kura? Jibu la swali hili linapatikana sehemu inayofuatia hapo chini baada ya sehemu yaani Sehemu ya 3.

SEHEMU 3: JE KUTAKUWEPO NA NAKALA ZA KUTOSHA ZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KATIKA KITUO CHA KUPIGA KURA?

Jibu ni ndio.

Ndio kisheria lazima kuwepo na nakala za kutosha za matokeo ya uchaguzi wa Rais katika Kituo cha Kupiga Kura kwa sababu ambazo nitazielezea hapa chini.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa mamlaka ya kutunga au kutengeneza Maelekezo ya Uchaguzi (Election Directives) yenye nguvu ya kisheria chini ya Kifungu cha 126 cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 na chini ya Kanuni ya 79 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitengeneza Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020 ambayo yanataja idadi ya nakala za matokeo ya uchaguzi wa Rais na mbunge ambazo zinapashwa kuwepo katika Kituo cha Kupiga Kura.

🟧 A. UTOSHELEVU WA NAKALA ZA FOMU ZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS.

Aya ya 9.19 ya Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020
inaelekeza kwa lazima kuwa kila Kituo cha Kupiga Kura lazima kiwe na Kitabu cha Fomu za Matokeo ya Uchaguzi Rais chenye "nakala 24" za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ( Fomu 21 A ) ambazo zitagawiwa kama ifuatayo;

(1) Nakala ya Kwanza ya Fomu ya Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ambayo iko ukrasa wa 1 wa Kitabu cha Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais atapewa Msimamizi wa Uchaguzi (Returning Officer) ngazi ya jimbo. Nakala ya kwanza ni nakala halisi (original copy).

(2) Nakala ya Pili ya Fomu ya Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ambayo iko ukrasa wa 2 wa Kitabu cha Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais itabandikwa ukutani na Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura katika Kituo cha Kupiga Kura husika kwa ajiri ya kuwajulisha wananchi au umma wa Watanzania matokeo ya Uchaguzi wa Rais katika Kituo husika. Nakala ya Pili sio nakala halisi bali ni nakala rudufu (photocopy) ambayo inarudufiwa kutoka katika nakala halisi yaani nakala ya kwanza.

(3) Nakala ya Kumi na Tatu (13) ya Fomu ya Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ambayo iko ukrasa wa 13 wa Kitabu cha Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais itapewa Tume Taifa ya Uchaguzi kwa ajiri ya matumizi yake ya kiofisi. Nakala ya 13 nayo ni nakala halisi (original copy).

(4) Kuanzia Nakala ya 3 na kuendelea (consecutively) mpaka Nakala ya 24 katika Kitabu cha Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ambazo ziko kuanzia ukrasa wa 3 na kuendelea mpaka ukrasa wa 24 wa Kitabu tajwa hapo juu watapewa mawakala wa wagombea Urais kulingana na idadi yao isipokuwa Nakala ya 13 ambayo itakuwa Nakala ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kwa kuwa kuna wagombea Urais 15, hivyo, basi mawakala wa wagombea Urais katika Kituo cha Kupiga Kura watapewa kuanzia nakala ya 3 mpaka ya nakala 18 isipokuwa nakala ya 13 ambayo itapewa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Pia, isipokuwa nakala ya 13, kuanzia Nakala ya 2 na kuendelea mpaka nakala ya 24 ni nakala zilizorudufiwa (photocopies) kutoka katika nakala halisi yaani nakala ya 1 na 13 na sio nakala halisi (original copy).

Nakala ya 3 kati ya nakala 24 ni kwa ajiri ya matumizi ya kiofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa maana ya Nakala ya 1, 2 na 13.

Fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais katika kituoni cha Kupiga Kura ambayo ni Fomu Na. 21 A iko kwenye umbo la kitabu ambacho kitakuwa na kurasa ishirini na nne (24) ambapo nakala 12 za awali zimetenganishwa na nakala 12 za mwisho kwa karatasi ngumu (separator). Nakala 12 za mwisho zinaanzia ukrasa wa 13 mpaka ukrusa wa 24 yaani ni kuanzia nakala ya 13 na kuendelea mpaka nakala ya 24.

Karatasi za Fomu Na. 21 A zimetayarishwa katika namna ambayo inawezesha kuandika na kutoa nakala rudufu (photocopies) bila kuweka karatasi ya kaboni (Carbon Papers) yaani ni "Self copying".

Hivyo basi, kila kituo cha kupiga kura kinatakiwa kuwa na nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais ( Form 21 A ) zisizopungua Nakala 24 , basi kwa kuwa wagombea Urais ni watu 15 ambao watapewa nakala 15 za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais na Tume ya Taifa ya Uchaguzi itapewa nakala 3 za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi Rais, hivyo, zitabaki nakala 6 za fomu za matokea ya uchaguzi wa Rais za ziada ambazo hazitatumika.

Kutokana na uchambuzi wa hapo juu basi kisheria lazima zitakuwepo nakala 24 za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais katika Kituo cha Kupiga Kura ambazo zinatosha kuwapatia mawakala wote 15 wa wagombea Urais 15 wote.

🟧 B. UTOSHELEVU WA NAKALA ZA FOMU ZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA MBUNGE NA DIWANI.

🔹 (a) Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Mbunge.

Utaratibu na masharti ya kisheria yanayotumika katika kutoa nakala za fomu za matokeo uchaguzi wa Rais kwa mawakala wa wagombea Urais katika Kituo cha Kupiga Kura unafanana karibu kwa kila kitu na utaratibu na masharti yanayotumika katika kutoa nakala za fomu za matokeo uchaguzi wa wabunge kwa mawakala wa wagombea ubunge na sheria inayotumika ni moja.

Hivyo basi, kutakuwepo na nakala 24 za fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa mbunge kwenye kila Kituo cha Kupiga Kura. Kati ya nakala 24 za Matokeo ya Uchaguzi wa mbunge, nakala 21 zitakuwa kwa ajiri ya kuwapatia mawakala wa wagombea ubunge katika Jimbo la Uchaguzi husika. Na nakala 3 zitakuwa kwa ajiri ya matumizi ya kiofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Mojawapo ya nakala kati ya nakala 3 tajwa hapo juu itakuwemo nakala moja (1) ya matokeo ya uchaguzi wa mbunge kwa ajiri ya kubandika katika ukuta wa Kituo cha Kupiga Kura kuutaarifu umma wa Watanzania na wapiga kura matokeo ya Uchaguzi wa mbunge katika Kituo husika.

Hatahivyo, nakala za matokeo ya uchaguzi wa mbunge katika Kituo cha Kupiga Kura zitakuwa kwenye Fomu Na. 21 B.

🔹 (b) Nakala za Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Diwani.

Kwenye uchaguzi wa diwani sheria zinazotumika katika mchakato wa kutoa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa diwani katika Kituo cha Kupiga Kura kwa upande moja ni tofauti na sheria zinazotumika kwenye Uchaguzi Rais na mbunge kwa upande mwingine isipokuwa Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020 ambayo yatumika katika uchaguzi wa madiwani pamoja na Uchaguzi wa Rais na wabunge.

Sheria zinazotumika kwa upande wa uchaguzi wa udiwani katika kutoka nakala za matokeo ya uchaguzi wa diwani ni hizi zifuatazo;

(i) Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura 292

(ii) Kanuni ya Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani, 2020

(iii) Aya ya 9.19 ya Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020.

Hatahivyo, pamoja na utofauti wa sheria bado utaratibu na masharti ya kisheria yanayotumika katika kutoa nakala za fomu za matokeo uchaguzi wa diwani kwa mawakala katika Kituo cha Kupiga Kura kwa upande mmoja unafanana karibu kwa kila kitu na utaratibu na masharti ya kisheria yanayotumika kwa wagombea wa nafasi ya Rais na nafasi ya mbunge kwa upande mwingine.

Isipokuwa nakala za matokeo ya uchaguzi wa diwani katika Kituo cha Kupiga Kura yanakuwa kwenye Fomu 21 C.

SEHEMU 4: NI LAZIMA MAWAKALA KUPATIWA NAKALA YA MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS.

Kisheria ni lazima Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ampatie kila wakala wa mgombea Urais nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais ambayo ni Fomu Na. 21 A kwa sababu nne zifuatazo:

🔴 (1) Masharti ya Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 yanaelekeza kwa lazima kwamba iwapo kuna nakala za kutosha za fomu za matokeo ya Rais basi ni "lazima" Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ampatie kila wakala wa mgombea Urais nakala ya fomu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais ya Kituo cha Kupiga Kura.

(2) Aya ya 9.19 ya Maelekezo ya Uchaguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020 inaelekeza kwa lazima kuwa kila Kituo cha Kupiga Kura lazima kiwe na Kitabu cha Fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais chenye "nakala 24" za fomu za Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ( Fomu Na. 21 A ) na kati ya nakala 24 tajwa hapo juu, nakala 21 ni kwa ajiri kuwapatia mawakala wa wagombea Urais ili wazipeleke kwa wagombea Urais na vyama vyao vya siasa ambavyo wanawakilisha katika Kituo cha Kupiga Kura.

🔴 (3) Kwa kuwa kisheria lazima ziwepo nakala 21 za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa ajiri ya kuwapatia mawakala wa wagombea Urais ili wazipeleke kwa wagombea Urais na vyama vyao vya siasa basi kutakuwepo na nakala za kutosha kuwapatia mawakala 15 wa wagombea Urais 15 ambao wameteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kugombea nafasi ya Rais katika uchaguzi mkuu wa 2020.

🔴 (4) Kwa kuwa kutakuwepo na nakala 21 za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais ambazo zinatosha kuwapatia mawakala 15 wa wagombea Urais 15 basi Wasimamizi wa Vituo vya Kupiga Kura lazima wawapatie nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais mawakala wote wa wagombea Urais kama inavyoelekezwa kwa lazima na masharti ya Kifungu cha 79 A (1) (e) cha Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sura ya 343 kwamba iwapo kuna nakala za kutosha "lazima" Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura awapatie wakala wote wa wagombea Urais nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais.

Pia, Kisheria ni lazima Msimamizi wa Kituo cha Kupiga Kura ampatie kila wakala wa mgombea Ubunge na udiwani nakala ya matokeo ya uchaguzi wa mbunge na diwani ambayo ni Fomu Na. 21 A na Fomu 21 C mtawalia (respectively) kwa sababu nne ambazo zimetajwa hapo juu kwa kufanya mabadiliko muhimu hapo juu (mutatis mutandis).

SEHEMU 5: HITIMISHO.

Wagombea wa nafasi ya Urais, ubunge na udiwani wana haki ya kupatiwa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi katika ngazi zote za kiuchaguzi kuanzia ngazi ya kituo cha kupiga kura, ngazi ya Kata, ngazi na Jimbo la Uchaguzi mpaka ngazi ya Taifa kutoka kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hivyo basi, ni raia yangu kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi pamoja na Wasimamizi wa Vituo vya Kupiga Kura kuheshimu sheria za Uchaguzi za nchi hii kwa kuwapatia Wagombea Urais, ubunge na udiwani au mawakala wao haki yao ya kisheria ya kupatiwa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi Rais, Mbunge na Diwani katika ngazi zote za kiuchaguzi ili kufanikisha kufanyika kwa uchaguzi Huru na wa Haki ambao una uwazi na unakagulika, unadhibitishika, unawajibika, sahihi na salama.

Kutoa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi wa Rais, wabunge na Madiwani kwa wagombea au mawakala wa wagombea katika Kituo cha Kupiga Kura na katika vituo vya kujumlisha matokeo ya uchaguzi katika ngazi ya Kata, Jimbo la Uchaguzi na ngazi ya Taifa kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi utaondoa kwa sehemu kubwa tuhuma za wizi wa kura na tuhuma za hujuma za Uchaguzi Mkuu na kufanya matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2020 kuwa ya kuaminika, kuheshimike na kukubalika kwa wagombea wote, vyama vyote vya Siasa, wapiga kura wote, watazamaji wa ndani na wa kimataifa wote na wadau wote wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

imeandikwa na Matojo M. Cosatta, (Senior JF Member).

Nimesoma makala yote mwanzo mwisho....

Asante sana kwa elimu murua kuhusu sheria na kanuni za uchahuzi mkuu huu wa 2020...

SWALI KUBWA LA KUJIULIZA NI HILI....

Kwamba, iweje NEC watunge kanuni inayopingana na sheria kuhusu mgombea Udiwani ama Ubunge ama Urais yeye mwenyewe ama kupitia wakala wake kuanzia ngazi ya kituo cha kupigia na kuhesabia kura wawe na "uhiari" badala ya "ulazima" kumpatia kila mgombea yeye mwenyewe ama wakala wake nakala ya matokeo ya kura??

Lengo la TUME lilikuwa ni nini hasa? Je, siyo kwamba wanatengeneza chanzo cha vurugu kwa makusudi kabisa?

Ni matumaini yangu kuwa hawataendelea na mchezo wao huu hatari kwa sababu hakuna maana wala sababu yoyote kuhatarisha AMANI ya nchi hii kwa sababu ya fomu za matokeo ya kura kwenye vituo...!

Na kwa upande mwingine ni kuwa, kumbe ni wazi kabisa kuwa, kwa NEC kufanya mambo kinyume cha sheria, huwa ni jitihada za makusudi kabisa kutaka kumsaidia mgombea fulani kushinda uchaguzi kwa kuchakachua matokeo ya kura halali kwa kila mgombea....!

Hili halikubaliki....
 
Kenge kabisa wewe. Ulamwambia mtu uelewa wake ni mdogo. Halafu huna JUSTIFICATION za kukosoa hoja zake?
Bure kabisa Wewe!!

Wewe unafikiri Kenge ni nani hapa kama siyo wewe maana hata wewe huna "justification" ya unachokikosoa....!!

Na kingine kukuhusu wewe ni hiki;

"Anayejua" au mtu mwenye "ufahamu" wa jambo fulani na kutaka kushea na wengine huwa hatumii lugha ya matusi na isiyo ya kistaarabu kutaka kurekebisha ama kukosoa hoja ya mtu mwingine kama vile mlevi wa bar za pombe za kienyeji hususanj chang'aa au gongo...!

Hivi ndivyo ulivyo wewe. Wewe ni mlevi wa vilabu vya pombe ya chang'aa tu, huna lolote unalolijua. Ushahidi ni maandishi yako...!!

Ndo kusema, lugha yako na uandishi wako tu ni "justification" tosha kuwa huna ulijualo zaidi ya "mapenzi kipofu" uliyonayo juu mambo haya....!!

Pole na usiku mwema...
 
ni kweli wote tunajua hilo, ila bila kusisitiza hili, uhuni ni lazima utafanyika vituoni. Mkuu CCM hii unafikiri inaogopa sheria? angalia tu namna wagombea walivyoenguliwa kuhuni huni wakati sheria zipo wazi kabisa.
Dah! Uko vizuri bro. Umemwaga nondo za kutosha.
 
Nikuhakikushia kuwa sijatumwa na mtu bali nimeandika kwa utashi wangu na kwa hiyari yangu ni kawaida yangu kufanya uchambuzi wa maswala ya kisheria katika maeneo mbalimbali hata kabla ya uchaguzi.

Uchambuzi wangu ni wa kitaalamu na nimefanya uchambuzi wa sheria tu bila kutaja jina la mtu au jina la chama cha siasa ni uchambuzi wa maswala ya sheria na sio uchambuzi wa watu au vyama vya siasa.

Hakuna popote kwenye makala yangu nimeisema tume ya Uchaguzi kwa ubaya kwa lengo la kuleta chuki au uchochozi.

Makala yangu ililenga kutanua uelewa wa wadau wa uchaguzi kuhusu swala hili la wagombea na mawakala wao kupatiwa nakala za fomu za matokeo ya uchaguzi ili kuwa na uelewa wa pamoja na unaofafana kuhusu swala hili na wadau hawa ni pamoja na wagombea, mawakala wa wagombea, wapiga kura, Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi, Wasimamizi wa Vituo vya Kupiga Kura na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Kama kweli unadhamila njema utakuwa umenielewa.

Mheshimiwa, hawa ni walewale wakati mwingine ni wa kuwapuuza tu maana wanakuwa hawana nia ya kuelewa ama kujifunza..

Makala yako inafumbua ufahamu watu wengi sana...

Hili CCM na Allies wao (kama huyu hapo chini 👇 👇👇👇👇huyo hapo chini uliyemkwoti), hawataki watu watambue na kuujua ukweli huu ambao ndio moja ya mbinu ya NEC katika chaguzi zote zilizopita ya kuchakachulia matokeo ya kura za uchaguzi kwa kumpa ushindi mgombea ambaye hakushinda wala kustahili kuwa mshindi...

Kwao watu wakijua udhaifu huu wa NEC, aliyewafanya wajue ni MCHOCHEZI...!!

Fikra za namna hii ni za kijinga na za kipumbavu sana tena ule upumbavu uliovuka mipaka ya ustaarabu wa binadamu. Huyu hapa 👇 👇msomeni..
Elimu iliyoambatana na uchochezi wa chuki dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, sawa rudi kwa huyo aliyekutuma mwambie umeshafanya kazi uliyotumwa.
 
Mheshimiwa, hawa ni walewale wakati mwingine ni wa kuwapuuza tu maana wanakuwa hawana nia ya kuelewa ama kujifunza..

Makala yako inafumbua ufahamu watu wengi sana...

Hili CCM na Allies wao (kama huyu hapo chini 👇 👇👇👇👇huyo hapo chini uliyemkwoti), hawataki watu watambue na kuujua ukweli huu ambao ndio moja ya mbinu ya NEC katika chaguzi zote zilizopita ya kuchakachulia matokeo ya kura za uchaguzi kwa kumpa ushindi mgombea ambaye hakushinda wala kustahili kuwa mshindi...

Kwao watu wakijua udhaifu huu wa NEC, aliyewafanya wajue ni MCHOCHEZI...!!

Fikra za namna hii ni za kijinga na za kipumbavu sana tena ule upumbavu uliovuka mipaka ya ustaarabu wa binadamu. Huyu hapa 👇 👇msomeni..
Asante sana mkuu Kitaturu.
 
Mbona hukubali kufundishwa?... Yaani wewe ndio mjuzi na mtaalamu wa kila kitu ama sivyo?

Mimi ninakubali kufundishwa na kuelimishwa tena kwa roho safi, hatahivyo, siwezi kufundishwa na professionally incompetent person anayefanya makosa ya kisheria ambayo yako wazi sana, mtu ambaye hana hata uwezo wa kutofautisha kati ya Returning Officer na Presiding Officer.

Mimi haya mambo ya sheria za Uchaguzi nimeyachimba kwa kina sana, hivyo, mtu ukija kichwa kichwa bila maandalizi ya kina, bila kusoma kwa kina na bila kuelewa kwa mapana, kwa kina na kwa marefu utakwama sana kwangu.
 
Back
Top Bottom