Umuhimu wa kuhonga katika mapenzi

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
1. KUHONGA HUBORESHA MAPENZI:

Fahamu kuwa unapomhonga mpenzi wako unamfanya ajihisi kama ni wapekee kwako, atajiona kama ni mmoja wapo kati ya watu wenye thamani kwako na huamini kama kweli upo karibu yake na unamjali.

Hali hii humfanya yeye kushindwa kutolipa mazuri kwako.
Wengi kabla ya kuomba papuchi hutanguliza hongo kwanza, si lazima iwe pesa hata hongo ya sifa za uongo na ukweli.

Kwa kuhonga kwako inamlazimu na yeye kulipa fadhila kwa kuonesha upendo wa dhati na utamfanya azidishe mapenzi kwako.



2. KUHONGA KUNAJENGA SANA KUMBUKUMBU KATIKA MAPENZI:

Fahamu kuwa unapomhonga mpenzi wako inakusaidia wewe kujijenga katika mawazo yake na endapo kama itatokea mkaachana nae basi pindi mpenzi wako atakapokuwa anaziona zawadi zako zitamfanya akukumbuke kwa mengi na atahisi kama kuachana na wewe kwake kuna tofauti na atajihisi kupoteza vingi toka kwako na kamwe kumbukumbu yako kwake haitofutika kila anapoona vitu ulivyomhonga.

Jitahidi sana unapohonga usihonge pesa tu, honga vitu vya kudumu maana huwa asset yako ya baadaye, pindi unapotokea mkwaruzano baina yenu.

Pesa huwa ni hongo inayovutia kwa muda mfupi na husaidia kupata kile unachokitaka kwa muda mfupi, ila jua atazitumia zitaisha utakuwa hujajenga misingi imara ya mapenzi.

Simaanishi kuwa usimpe mpenzi wako hela, hapana ila inabidi ufahamu kuwa pesa hutumika katika kukidhi mahitaji na sio katika kuboresha mapenzi.

Aisee jifunzeni kuhonga mpunguze stress za mapenzi.
 
Bora nihongwe pesa, ukihongwa asset siku ya kuachana jiandae kufedheheka. Wananyang`anya kila kitu. We nipe pesa ninunue nachotaka na sio unileteee hakuu sitaki.
Mh.

Nikikupa asset siku tukiachana ukiziona asset utanikumbuka tu.

Lazima utabip tu.
 
UPO
1. KUHONGA HUBORESHA MAPENZI:

Fahamu kuwa unapomhonga mpenzi wako unamfanya ajihisi kama ni wapekee kwako, atajiona kama ni mmoja wapo kati ya watu wenye thamani kwako na huamini kama kweli upo karibu yake na unamjali.

Hali hii humfanya yeye kushindwa kutolipa mazuri kwako.
Wengi kabla ya kuomba papuchi hutanguliza hongo kwanza, si lazima iwe pesa hata hongo ya sifa za uongo na ukweli.

Kwa kuhonga kwako inamlazimu na yeye kulipa fadhila kwa kuonesha upendo wa dhati na utamfanya azidishe mapenzi kwako.



2. KUHONGA KUNAJENGA SANA KUMBUKUMBU KATIKA MAPENZI:

Fahamu kuwa unapomhonga mpenzi wako inakusaidia wewe kujijenga katika mawazo yake na endapo kama itatokea mkaachana nae basi pindi mpenzi wako atakapokuwa anaziona zawadi zako zitamfanya akukumbuke kwa mengi na atahisi kama kuachana na wewe kwake kuna tofauti na atajihisi kupoteza vingi toka kwako na kamwe kumbukumbu yako kwake haitofutika kila anapoona vitu ulivyomhonga.

Jitahidi sana unapohonga usihonge pesa tu, honga vitu vya kudumu maana huwa asset yako ya baadaye, pindi unapotokea mkwaruzano baina yenu.

Pesa huwa ni hongo inayovutia kwa muda mfupi na husaidia kupata kile unachokitaka kwa muda mfupi, ila jua atazitumia zitaisha utakuwa hujajenga misingi imara ya mapenzi.

Simaanishi kuwa usimpe mpenzi wako hela, hapana ila inabidi ufahamu kuwa pesa hutumika katika kukidhi mahitaji na sio katika kuboresha mapenzi.

Aisee jifunzeni kuhonga mpunguze stress za mapenzi.[/QUOT

Upo sahihi mkuu ingawa inahitaji mtu muelewa zaidi ktk huo uhongwaji na anaejitambua na kuona thamani yake kwa anaemuhonga, ukikutana na kichwa maji hashindwi kukutangazia wewe ni buzi lake, unajipendekeza n.k.
 
Nipo malisak .

Vipi, wewe hupendi kuhongwa??
Napenda sana tu kuhongwa hasa nikibaini anaenihonga ananihonga kwa upendo wa dhati na si kwa sababu ya kitu fulani, maana mwengine anakuhonga kwa vile anahitaji kitu fulani kwako so anajaribu kukuweka karibu na akishakipata anapotea. lkn kama anakuhonga kidhati sio shida.
 
Back
Top Bottom