Heri ya Mwaka mpya wana JF!
Nimekuwa nikifuatilia siasa za Tanzania ndani ya vyama mbalimbali nimekuja kungundua hakuna chama chochote hapa kwetu Tanzania chenye uwezo na nia ya kumkomboa mwananchi (Mtanzania) na kumpa maisha bora na yenye neema.
Si CUF na si CHADEMA na wala si hawa CCM walioshindwa kabisa toka uhuru! Vyama vyetu vimejaa nyufaa. Na ndani ya vyama vyetu vyote kuna matatizo makubwa ya mifumo, uongozi, ufisadi, rushwa, ukandamizaji, unyonyaji na tamaa mbaya ya madaraka.
Hakika si rahisi kuwa na chama kikamirifu kwa asilimia mia moja,Tokea uhuru tumekuwa na chama kilekile hadi leo kama ni mtu amezeeka sasa na anahitaji kupumzishwa. Lakin kwa kundi kubwa la vijana tuweni makini na tusikubali kundanganywa na mtu au chama chochote kile cha siasa na kukiamini kuwa ndo mkombozi wetu, kikubwa na cha kuamini ni kupunguziwa matatzo, kuonja malezi ya baba (Chama) kingine na wala siyo kumaliziwa matatizo yetu kwa asilimia mia moja hii ni tahadhali tu.