Ushindi wa Konde; Mbadala wa CCM ni chama kipya kutoka ndani ya CCM

Mwande na Mndewa

Senior Member
Feb 26, 2021
105
500
USHINDI WA KONDE;MBADALA WA CCM NI CHAMA KIPYA KUTOKA NDANI YA CCM.

Na Chakat,Hapa Kazi Tu.

Tanzania inapaswa kuwa na vyama vya siasa vinavyojitambua na vinavyojua wajibu wao katika kuleta maendeleo ya Taifa kwani siasa sio chuki wala uhasama,siasa sio udini,siasa sio Ugaidi,siasa ni usawa,siasa ni upendo na amani.

Baada ya ushindi wa Konde, CCM itakuwa imegundua kuwa kwa sasa imepoteza mvuto kwa umma,ni muda muafaka kuwa na mkakati wa chini chini kuanzisha Chama mbadala ya upinzani ili kichukue nafasi ya Chama Cha Konde, kwani CCM inaona aibu kushindwa uko Konde, na kwa mujibu wa mtazamo,Chama Cha Konde kinajiandaa vyema kwa ajili ya mwaka 2025 na kinaweka mkakati wa ushindi na nini kitafuata baada ya ushindi,

Tumesikia wataileta code 259,tumesikia wakisema wao ni nchi huru,hapa wanaelekea kwenda kuuparula Muungano,ndipo nasema CCM iandae Chama kipya Cha Upinzani kitakachokwenda kudumisha mila na desturi za Mtanzania,Chama Cha Kizalendo mfano wa CCM kitakachokwenda kulinda rasilimali za Watanzania.

Huu ni muda wa kuanzisha mkakati wa kuanzisha chama kingine cha Kizalendo sio Cha upinzani, lengo ni kuwa chama hicho kiwe mshindani wa ccm,na hata ikitokea kikaishinda ccm, basi kitaachiwa dola, lakini kitaendelea kufanya kwa Uzalendo wa ccm ya sasa iliyopoteza mvuto,

Chama kipya kiwe Chama Cha Uzalendo,ni Chama kinachounga mkono maendeleo yanayofanywa na Chama tawala, kuenzi mazuri ya chama tawala cha sasa,Chama kitakachotembea katika nyayo za Mwalimu Julius Nyerere,Chama kitakacholeta usawa kati ya tajiri na masikini,Chama kitakachoongea sauti ya Mnyonge na mnyonge akaguswa kuwa anazungumziwa matatizo yake,na baada ya muda mchache matatizo yake kutatuliwa,

Fuatilia vizuri utajua ninachokiongea,Tazama hata mitandaoni,kwa sasa kuna post nyingi za kupima upepo juu ya kuanzishwa kwa hicho chama kingine cha Kizalendo,lakini kikwazo ni muda, na mkakati ni kuhakikisha Chama iko kinakubalika na wananchi,Matarajio ni kuwa hatua hizo zikikomaze Chama kipya ili kiweze kutembea katika nyayo za Chama kilichoasisiwa na Mwalimu Julius Nyerere na kuhuishwa na Daktari John Pombe Magufuli,Kitakapoanziswa kitapigiwa debe kuwa ni chama cha kitaifa kwani hakina ukanda wala udini, Vuta subira kama hilo litafanikiwa uje uchukue mrejesho.

Kihistoria Chama Cha Konde ndio kilipewa kazi hiyo ya kuwa backup ya ccm kuelekea uchaguzi wa 2014, chama hicho kilianzishwa na genge la Maembe, Migulu,mnamo January, Napea kutoka msoga, lakini Daktari John Pombe Magufuli alipoingia madarakani 2015 aliamua kuacha mikakati yote ya gengeni ikiwemo ya kisiasa,toka wakati huo dhambarau ikapotea.Daktari John Pombe Magufuli yeye alikuwa hapambani kwa mikakati ya kisiasa, na hapo ndio ukamuona Mwami kuwa mpinzani wa kweli baada ya Chama chake Cha Konde kufinyangwa finyangwa na kutupwa kule na Mwanaume.

Kwa sasa Genge linarudi tena lakini Watanzania wameshawajua,kwamba awa si Wazalendo kitu kidogo tu kwa wazungu,sasa tukiwapa nchi si watampa mzungu,tuache utani tumpe nchi kibaraka wa mzungu,hapana bora tuanzishe Chama kingine kitakachobeba Uzalendo, Tanzania kwanza na rasilimali ziwanufaishe Watanzania,wanaojaribu kusogeza dhambarau karibu, wakisema hakitakiwi kususia uchaguzi hata kama tume ya uchaguzi sio huru. Upepo utakavyovuma ndio utaamua hicho chama kipya kianzishwe maana mipango imeshakamilika, Tatizo Chama Cha Konde kupewa nafasi hiyo limekuja kutokana na wao kuungana na Wapemba Kinyume na hapo, hata Konde wasingekuwepo.

@CHAKAT#
 
MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,863
2,000
Policcm wataacha kudhibiti Chama kipya kutoka Ccm au itakuwa tawi la CCM

Acheni KUJITOA ufahamu

Makada embu tafuteni hoja zenye ushawishi kwa wananchi...hamjiamini..mnategenea police mpaka kichefu chefu
 
mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
9,731

Chadema inawatesa watawala,
 
Nipo huru

JF-Expert Member
Jul 20, 2021
1,328
2,000
CCM itaendelea kutawala hadi wachoke wenyewe kwa sababu vyama vilivyopo vimeacha lengo lao halisi vimekubali kuingia kwenye mtego wa CCM wa kuwagombanisha wenyewe kwa wenyewe,kuna watu wanajiona wao ndio wapinzani wa kweli na wengine sio wapinzani.
 
kedrick

JF-Expert Member
Apr 25, 2015
4,805
2,000
Iko chama kilitakiwa kuanzishwa na Hayati JPM waliobakia wote Hamna kitu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom