Kuna umuhimu wa kuunda chama kipya cha upinzani?

IFAC

JF-Expert Member
Dec 12, 2021
3,632
9,159
Sote tunajua lengo kuu la Chama Cha Siasa ni kushika Dola.

Duniani kote vyama vinavyotarajia kushika dola huwa vinakuwa na ajenda, mipango na ratiba jinsi zitakavyo kwenda kushika dola.

Chama kilichotarajiwa na wengi Kutoa mawazo mbadala, kuonyesha mapungufu ya kimfumo na kiserikari.

Kuonyesha njia mbadala kunapokuwa na mkwamo wa kitaifa.

Kimeamua kuungana na mkoloni mweusi.

Je, kinafaa kuaminiwa?
Je, kinafaa kutumainiwa?
Je, kiendelee kushika ukamanda wa waamini mageuzi nchini?

Ukiwaza hapo juu, unagundua Sasa kinatoka kwenye misingi yake.

Ni vyema kusifu ila sio kuabudu maana Toka kipitishwe kwenye tanuri la moto badala ya kuuzidi kuwa kigumu kama chuma ila chenyewe kinazidi kulegea na viongozi wake wakizidi kuwa kupe na chawa.

Tukiamini hiki au tuunde kingine chenye kubeba maoni, mawazo na fikra za Tanzania mpya ya maendeleo Sasa na baadae?

View attachment 2542155
 
Huu muunganiko umeonekana kwenye nini? uliasisiwa lini?

Maridhiano sio muunganiko, ni makubaliano kwenye baadhi ya mambo, ukitaka muunganiko tazama ACT na CCM kule Zanzibar, hao wote wanaunda serikali moja.

Wengi wenu mnahitaji shule, thread mnazoleta huku ni za kiupotoshaji, au kwa maana nyingine mnawafundisha wasiojua ujinga.
 
Mnajisumbua bure Bila Katiba Mpya Bila Tume huru ya Uchaguzi hata Chama cha Democrat au REPUBLICAN kikishindana na Ccm vitashindwa ndio maana Chadema kinapigania hivyo Kwanza VIPATIKANE.

Tanzania kuna Utitiri wa Vyama vya Siasa kama unaona Chadema hakina uwezo wa kushika Dola je hivyo VYAMA vingine Vimeshindwa nini?

CCM imeshika Dola kwa sababu ya KATIBA iliyojiwekea na Tume iliyojiundia
Anzisheni hicho chama kipya ila kwa Katiba na Tume hii MNAJIDANGAYA
 
Unafikiri chama kinaota tu kama uyoga? Pamoja na ACT kuwachukua baadhi ya wanachama wa CUF bado kinapumulia mashine.

Kama huamini waende mikoani kama watapata wanachama. Tuwaachie wenye vyama vyao wafanye kile wanachoona kinawafaa maana wakipitia magumu hakuna anayewasaidia.
 
Pambania maisha yako na ya familia yako.

Wanasiasa wote wapo pale kwa manufaa yao binafsi na familia zao.

Hakuna mwanasiasa ana uchungu na wanyonge wala taifa.

Walau Magufuli kidogo alijitahidi, hawa wengine hakuna kitu. 😁
 
Nimekuwa mfuasi wa hiki chama tangu 2006, sio siri nilikipenda sana sababu kilikuwa na dhamira na dira fulani.

Leo hii sijui kinapigania jambo gani.. hakuna agenda mpaka sasa. Atleast baadhi ya wachache waliobaki kama Heche ndo wanatia matumaini.

Hapa katikakati kuna maamuzi ya kijinga yanafanyika bila vikao halali vya chama, personal nahisi Mbowe ni mfungwa huenda kuna order amepokea kutoka juu ndo anazotumia kuongoza chama.

Naunga mkono hoja kuna haja ya kuanzisha chama kipya cha siasa.
 
Sote tunajua lengo kuu la Chama Cha Siasa ni kushika Dola.

Duniani kote vyama vinavyotarajia kushika dola huwa vinakuwa na ajenda, mipango na ratiba jinsi zitakavyo kwenda kushika dola...
Ukianzisha chama Cha Upinzani leo, hesabu miaka 20 ndio ufikirie kuchukua dola. Waulize ACT walikuja na Moto Ila 2015 wakaamblia kiti kimoja Cha ubunge na kura elfu tisini za urais.
 
Huu muunganiko umeonekana kwenye nini? uliasisiwa lini?

Maridhiano sio muunganiko, ni makubaliano kwenye baadhi ya mambo, ukitaka muunganiko tazama ACT na CCM kule Zanzibar, hao wote wanaunda serikali moja.

Wengi wenu mnahitaji shule, thread mnazoleta huku ni za kiupotoshaji, au kwa maana nyingine mnawafundisha wasiojua ujinga.
Kuna kuungana kwa itikadi, sera, mtazamo au kimawazo.

Mawazo hayo yanaweza kuwa ya kiuchumi, kijamii, kisiasa au kifursa ikiwemo kulamba asali

Maridhiano hayatakiwi yakinyong'onyeshe bali yakiimalishe.

Je, kwa mtazamo wako ni upande upi utakao nufaika kisiasa?

Unafahamu kwenye wimbo wa sisi ndio M wanasemaga ndio Ile ile?

Maana yake linapokuja Swala la kushika dola hawana ajizi na utagundua hii yote ilikuwa komedi?

Je, ni mara ya kwanza hiki kutokea?
 
Unafikiri chama kinaota tu kama uyoga? Pamoja na ACT kuwachukua baadhi ya wanachama wa CUF bado kinapumulia mashine. Kama huamini waende mikoani kama watapata wanachama...
Kwani waliingia kwenye siasa kuvimbiwa matumbo yao au walikuwa na nia ya dhati kusogeza gurudumu la maendeleo la nchi hii.
 
Nimekuwa mfuasi wa hiki chama tangu 2006, sio siri nilikipenda sana sababu kilikuwa na dhamira na dira fulani...

Umesikiliza hotuba za Viongozi Leo kuanzia shariffa, Catherine na Mbowe? Tatizo hamtaki kusikiliza Viongozi wanaongea Nini, mnakuja na conclusion zenu.

Mbowe kaongelea CCM kuiba uchaguzi wa 2015 mbele ya Rais, kaongelea covid 19 na pia kaongelea Katiba mpya wewe ulitaka afanyeje?. Sharifaa na Ruge wameongelea matatizo ya wanawake na mfumuko wa Bei.
 
Hakuna umuhimi wowote ule.
Watu ni walewale, watu wapo kwa maslai binafsi, hakuna Uzalendo miaka hii.
 
Umesikiliza hotuba za Viongozi Leo kuanzia shariffa, Catherine na Mbowe? Tatizo hamtaki kusikiliza Viongozi wanaongea Nini, mnakuja na conclusion zenu. Mbowe kaongelea CCM kuiba uchaguzi wa 2015 mbele ya Rais, kaongelea covid 19 na pia kaongelea Katiba mpya wewe ulitaka afanyeje?. Sharifaa na Ruge wameongelea matatizo ya wanawake na mfumuko wa Bei.
Wameshikwa hakili hawa machawa.
 
Back
Top Bottom