Umuhimu wa kuanzisha chama cha ukombozi wa Mtanzania

carmel

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
2,837
262
Wana JF,

Baada ya kigugumizi kingi kinachopata CHADEMA kwa sasa, nidhahiri wengi wetu ambao tulikuwa tunadhani inaweza kututoa shimoni tumekata tamaa baada ya revelation mbalimbali zinazoendelea, inawezekana kuna agenda za siri nyingi sana tusizozijua na hivyo matokeo yake CCM itaendelea kutawala siku zote tusipofanya maamuzi ya busara ya kupata chama mbadala.

Sasa na-suggest tuanzishe chama cha watu wenye uchungu wa kweli na nchi hii, na tuweke malengo kwamba hadi 2025 lazima tubadilshe utawala, ni maoni tu!
 
Kwa hapa JF huwez kupata consensus nzuri sana, mi nashauri kama una wazo la namna hiyo, fanya kweli uraiani, JF itakusupport sana tu kama chama kitakuwa makini kulingana ndoto zako zinavyoelekeza.
 
Watanzania bwana, mkipigiwa ngoma hamchezi, mkiambiwa mpande mnashuka. Vyama sio suluhisho, kwani hata cha kwako utajitahidi kukiweka katika hali ambayo hutokuwa tayari mamluki wa ccm kuwemo ndani, matokeo yake ni bwack to square one.

Jambo la msingi ni kufahamu tu kuwa hakuna chama kibaya, sio CCM, CHADEMA CUF n.k. Vyote ni vizuri, tatizo ni watu kama mimi na wewe!

Dawa ni kujiunga na hivi vyama, tujenge nguvu ya kitaifa zaidi, hatimaye tutashinda. Ukitizama hadi leo, vyama vya siasa vya upinzani Tanzania vina mizizi mikubwa Kilimanjaro, Mara na Pemba! Tuunganishe nguvu ili tuweze kuwa na uwakilishi stahili, la sivyo tuaendelea kuwasema wale ni wapemba, wachaga n.k

Inshort kuanzhisha utitiri wa vyama sio suluhisho, ila kucheza ndani ya vilivyomo ndio tija.
 
Kuna chama karibu kitaanzishwa na hiki ni chama ambacho kitakuwa na lengo moja tu kuingoa ccm kupitia njia za mkato.
 
Kuna chama karibu kitaanzishwa na hiki ni chama ambacho kitakuwa na lengo moja tu kuingoa ccm kupitia njia za mkato.

Kuing'oa CCM kupitia njia za mkato ni kwa jeshi letu kuchukuwa nchi kwa kufanya mapinduzi. Je, mwenzetu unapendekeza jambo hilo?
 
carmel

Hilo ni shauri zuri, lakini we cannot afford kuweka malengo kama hayo hadi 2025. CCM ni lazima ing'oke sasa hivi - kama sio leo basi ni kesho. Hatuwezi kuendelea na umaskini kama huu ambao ni men-made wakati nchi yetu ni tajiri.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo ni kwamba baada ya ukombozi hao wakombozi watakuwa wabaya kuliko wale waliowaondoa madarakani. Mbona mfano mzuri tunao hapa Tanzania. Walioishi enzi za mkoloni wanasema kuwa maisha wakati ule yalikuwa safi sana.
 
Wazo si baya. Lakini kama umeona kasoro CHADEMA uliyodhani ni chama mbadala ukaamua kubadilisha na kuanzisha kingine means tutapata vyama vingi sana. Pia mawazo ya watu wote hayawezi kuwa sawa hata mara moja. Hivyo CHADEMA wamefanya kitu ambacho kwacho wewe umekwazika na kwa kuwa CHADEMA bado inakua ni vizuri kuwapa mawazo yako ili wayafanyie kazi kwa siku za mbele.

Ikiwa zinatokea kasoro tunakimbilia kuanzisha vyama tutafika wapi? Hata nyumbani mtoto akisosa unamrekebisha siyo kumtupa na kuzaa mwingine. Jaribu kurekebisha kasoro ulizoona otherwise tell me ulikuwa na wazo hilo si kwa kuwa CHADEMA wamefanya usiyoyakubali.
 
Humu ndani kuna watu uwezo wao ni mkubwa sana kuliko wengi niwaonao wanahangaika na siasa.

Nimebahatika kuongea na wanasiasa wengi hasa wabunge, uwezo wao wa kuchambua mambo ni mdogo mno ukilinganisha na wachambuzi wa mambo ya kisiasa na kijamii humu ndani.

Sasa kwanini tusikubali kuweka itikadi zetu pembeni na kuamua kutafuta ukombozi wa kweli wa taifa letu na tuanze kwa kuanzisha chama siasa?

Karibuni kwa mjadala
 
Ndugu yangu Chama cha siasa huanzishwa na kustawi endapo wanachama wake WANA ITIKATI sawa na wana malengo sawa. Sasa humu jamvini unajiridhisha kuwa kitu hiki kinawezekana? Tazama kwa makini mitizizamo yetu hata kwa masuala ambayo katika hali ya kawaida anagalau watu wangekubaliana.
 
Heri ya Mwaka mpya wana JF!

Nimekuwa nikifuatilia siasa za Tanzania ndani ya vyama mbalimbali nimekuja kungundua hakuna chama chochote hapa kwetu Tanzania chenye uwezo na nia ya kumkomboa mwananchi (Mtanzania) na kumpa maisha bora na yenye neema.

Si CUF na si CHADEMA na wala si hawa CCM walioshindwa kabisa toka uhuru! Vyama vyetu vimejaa nyufaa. Na ndani ya vyama vyetu vyote kuna matatizo makubwa ya mifumo, uongozi, ufisadi, rushwa, ukandamizaji, unyonyaji na tamaa mbaya ya madaraka.

Hakika si rahisi kuwa na chama kikamirifu kwa asilimia mia moja,Tokea uhuru tumekuwa na chama kilekile hadi leo kama ni mtu amezeeka sasa na anahitaji kupumzishwa. Lakin kwa kundi kubwa la vijana tuweni makini na tusikubali kundanganywa na mtu au chama chochote kile cha siasa na kukiamini kuwa ndo mkombozi wetu, kikubwa na cha kuamini ni kupunguziwa matatzo, kuonja malezi ya baba (Chama) kingine na wala siyo kumaliziwa matatizo yetu kwa asilimia mia moja hii ni tahadhali tu.
 
Badala ya kuhubiri kushindwa kwao bila wazo ya jinsi gani kuboresha, basi labda ungeinuka. Manake kazii hii inakuhusu pia. Unaonaje ukaanzisha chama chenye mtazamo wa kumkomboa mtanzania mzalendo na kuleta tangible results?
 
Heri ya Mwaka mpya wana JF!

Nimekuwa nikifuatilia siasa za Tanzania ndani ya vyama mbalimbali nimekuja kungundua hakuna chama chochote hapa kwetu Tanzania chenye uwezo na nia ya kumkomboa mwananchi (Mtanzania) na kumpa maisha bora na yenye neema.

Si CUF na si CHADEMA na wala si hawa CCM walioshindwa kabisa toka uhuru! Vyama vyetu vimejaa nyufaa. Na ndani ya vyama vyetu vyote kuna matatizo makubwa ya mifumo, uongozi, ufisadi, rushwa, ukandamizaji, unyonyaji na tamaa mbaya ya madaraka.

Hakika si rahisi kuwa na chama kikamirifu kwa asilimia mia moja,Tokea uhuru tumekuwa na chama kilekile hadi leo kama ni mtu amezeeka sasa na anahitaji kupumzishwa. Lakin kwa kundi kubwa la vijana tuweni makini na tusikubali kundanganywa na mtu au chama chochote kile cha siasa na kukiamini kuwa ndo mkombozi wetu, kikubwa na cha kuamini ni kupunguziwa matatzo, kuonja malezi ya baba (Chama) kingine na wala siyo kumaliziwa matatizo yetu kwa asilimia mia moja hii ni tahadhali tu.

Nina hakika wewe huishi Tanganyika. Maana nashindwa hata kukutafsiri.
 
Utayakaza macho yako na hautaona milele...tumia utashi na akili za bure kung'amua na utapata jawabu kuwa kipo,nacho ni M4C...
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom