Umuhimu wa DPP Biswalo na Plea-bargaining unaonekana kwenye hukumu kama hizi

Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
715
1,774
Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imemhukumu kwenda jela miaka 4 au kulipa faini ya tsh mil 12 aliyekuwa mkurugenzi wa mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania David Mattaka na wenzie kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka, kughushi nyaraka na kuisababishia serikali hasara ya tsh bil 71.

Huu ni ujuha na matokeo ya rushwa katika mihimili ya haki
 
Badilisheni sheria

Watumishi wengi wa uma watatamani waibe ili watajirike.

Sheria ikiwa dhaifu huchochea maadili mabaya katika jamii.

Kuna haja ya kufanya maboresho katika sheria hii.
 
Unaamini huo uzushi toka kwa Rais wako? Utakuja kusikia alidanganywa na wasaidizi wake ngoja hiyo kauli ije imgeuke utasikia
Sasa unataka tukuamnini wewe tusiyekujua hata jina?

Yule dikteta alikuwa muuaji, mwizi na mporaji. Akawa anawalazimisha watu kukiri makosa ya kubambikiziwa halafu anawatoza pesa na kuzificha kwenye akaunti binafsi kule China.

Bora kafa mapema (majitu ya hovyo hufa mapema).
 
Kama alivyotufanya jpm kwamba hela za makinikia kila mmoja atanunuliwa Noah. Baadae kabudi akasema zile kauli za jpm alikuwa ni kanyaboya
 
Watumishi wengi wauma watatamani waibe ili watajirike.

Sheria ikiwa dhaifu huchochea maadili mabaya katika jamii.

Kuna haja ya kufanya maboresho katika sheria hii.
Wakumbuke maisha yetu siyo ya hapa duniani hapa tunapita tu. Itakufaidia Nini kuipata ulimwengu wote huku ukiicha nafsi yako iangamie kwa moto usiozimika wa milele
 
Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imemhukumu kwenda jela miaka 4 au kulipa faini ya tsh mil 12 aliyekuwa mkurugenzi wa mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania David Mattaka na wenzie kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka, kughushi nyaraka na kuisababishia serikali hasara ya tsh bil 71.

Huu ni ujuha na matokeo ya rushwa katika mihimili ya haki
Mtu ameondoka na shs bil. 71 za umma unamuhukumu kulipa shs m 12. Mbona ni biashara ya faida kupindukia kupindukia. Hiyo kesi ni ya siku nyingi. Wamehonga hadi jpm hayuko imemalizwa. Watu wanaopambana ili rushwa itawale walaaniwe wote.
 
Watumishi wengi wauma watatamani waibe ili watajirike.

Sheria ikiwa dhaifu huchochea maadili mabaya katika jamii.

Kuna haja ya kufanya maboresho katika sheria hii.
Mimi nadhani sheria siyo dhaifu isipo kuwa wasimamizi wa vyombo vya kutoa haki
 
Unaamini huo uzushi toka kwa Rais wako? Utakuja kusikia alidanganywa na wasaidizi wake ngoja hiyo kauli ije imgeuke utasikia
Kilichotokea kimetokea Sasa swala la kusubiri hata Yesu Masihi tunamsubiri. How many years now? Unawezaje kusema Rais Ni Mzushi? Serious na bado uko kwenye nchi inayoongozwa na Rais Mzushi? Hebu wewe unayejua ukweli tuambie zile fedha ziko wapi Sasa!
 
Sasa unataka tukuamnini wewe tusiyekujua hata jina?

Yule dikteta alikuwa muuaji, mwizi na mporaji. Akawa anawalazimisha watu kukiri makosa ya kubambikiziwa halafu anawatoza pesa na kuzificha kwenye akaunti binafsi kule China.

Bora kafa mapema (majitu ya hovyo hufa mapema).
Kwani wewe kwenu watu hawafi?ata Mtangazaji wa Channel ten Daud Mwangosi aliuwawa kinyama na Polisi wakati wa utawala wa JK na Mabomu ya Mbagala yaliua watu kibao kwa uzembe wa utawala wa JK!
Watanzania hawajaanza kufa wakati wa JPM.Au ulikuwa kachalii enzi hizo?
 
Naomba saaana nikochini ya miguu ya mwishiwa jaji, mimi niko tayari nikamtumikie hiyo miaka 4 huko jela kisha nikitoka anipige kabilioni kamoja kwenye hizo 71 au robo tuu ya kabilioni kamoja...
 
Back
Top Bottom