Umuhimu wa chakula katika mapenzi/mahusiano

AshaDii

Platinum Member
Apr 16, 2011
16,190
18,080

Ladies and Gentle men, imani yangu ni kua woote wazima wa afya…. Na tutashirikiana katika mada hii nyingine tena ikilenga chakula na umuhimu wake katika mahusiano.

UMUHIMU WA CHAKULA KATIKA MAPENZI/MAHUSIANO

Chakula ni moja ya kitu ambayo huchukuliwa saana for granted katika maisha yetu ya kila siku… Kana kwamba hakina umuhimu wowote mpaka pale utaposikia njaa – However if you are lucky enough waweza jua/tambua kua with food… Great food at that you can do wonders katika mambo mengi, - mahusiano yakichukua kipengele chake pia. Hayo mahusiano yaweza kua mahusiano ya urafiki/undugu/ujamaa na la muhimu zaidi yanaweza kua ni Mahusiano ya Mapenzi ikienda hand in hand na tendo husika…

Najua na naamini kua usasa umetuingia na kututawala saana… tumefika wakati tunashindwa kujua kitu gani katika culture za watu (hasa magharibi) tuige na zipi tutupie mbali. Bahati mbaya saana katika jamii saizi sio ajabu kabisa kukuta mdada mtu mzima hajui kupika na ata admit kwa wazi kabisa kua hajui kupika… (sijui haoni aibu?? – lkn ngoja niachane na hawa niendelee na topic!) Na wengine akina mama anaendekeza binti yake asipike kwa sababu eti yuko busy na masomo, kuna msichana wa kazi or hata eti asisumbuliwe sababu binti mwenyewe hayuko interested….Sasa akiwa busy si ndo vizuri.. unamfundisha multitasking… Akina mama naomba mtafakari na mchukue hatua!

  1. Chakula na nafasi yake katika mahusiano ya Urafiki/Undugu na Jamaa.
Tokana na kasi ya maisha na majukumu kua mengi na magumu kumekua na taratibu saana ya watu kujiangalia wao wenyewe na familia zao ili kuweza kujikimu… Mahusiano na ushirikiano kwa Marafiki, Ndugu au Jamaa huendelea but out of obligation… Msaidie leo kesho atanisaidia… Mahusiano yanabaki ya kulipana. Kujenga uhusiano mzuri hasa kwa marafiki wa maana na karibu unaweza walau hata mara moja kwa miezi sita au hata mwaka (acha mambo ya sikukuu) waweza mkaribisha rafiki ama jamaa na mwenza wake (not necessarily but inapendeza) nyumbani kwako ukiwa umeandaa chakula kizuri kwa ajili yao. Kumbuka kua unapoandaa chakula kinacho matter ni jinsi gani umekiandaa wala si kutandaza Meza na kuweka kila aina (Personally naamini bora aina chache upate na ufurahie hio taste kuliko vikiwa viiiingi… labda in special cases kama sherehe).

  1. Chakula na nafasi yake katika mahusiano ya Mapenzi… (Wenza..)
Kitu kimoja wapo ambacho ni muhimu saaana katika mahusiano ni Chakula…. Ni wazi kua kaka/baba zetu wanapenda Sex, Great Food, Good Drinks mengine ndo hufuata… Wadada/wamama We love Good Life, Attention, Kujitambua then vitu kama Sex, Good Food and Good Drinks hufuata hapo… (sio woote kwa wasio kubali relax endelea kuto kubali…). Hivyo basi with Great Food you can say volume of words… Show the extent of your affection and Say the words I Love you… and this Dears is with food – Not only food, But Great Food… Chakula waweza onesha intensity ya mapenzi yako saa ingine kuliko maneno… It has that power.. angalia hii…

  • Chakula chaweza onesha or show intensity of your feelings… hasa when in love… ambapo Mwanamke (samahani nimezingatia katika jamii zetu za ki Africa sio Magharibi…) anapoamua kuandaa chakula maalum kwa ajili ya mpenzi wake… Kama nilivyosema sio lazima kutanda meza… Lah! Unaweza ukaanda vyakula concrete viwili kama Ugali Vs Ndizi OR Wali Vs Chapati… (Epuka saana vyakula kama chips, bites, hizo ni side food kwa most kaka zetu wa Kiswahili – huona tu soo kuadmit…); Kisha ukaanda na mboga yako kama Samaki, Nyama ya ng’ombe or Kuku… ikiambatana na veggies or salads. Of course bila kusahau Matunda na Home made fresh Juice – for vitu kama soda, wine, beer not recommended kuenda sambamba na food…

Baada ya kupika chakula chako hakikisha display mezani ni ya ukweli na Vyombo utumiavyo navyo hu matter katika presentation of your food…. In Short hakikisha kua the Food is of high quality katika kundaliwa.. (in the sense kua umepika kwa usafi, zingatia spices, cooking temp, ubora wenyewe wa ulicho pika i.e. Samaki aina gani na ina taste gani mdomoni and the like…) na pia hakikisha the Food has a quality display.. (Kama ni dinner, tumia candles, aina ya vyombo na clarity… sio glass ina michirizi ya maji yalokauka baada ya kuoshwa and the like…)… Andaa vyoote mezani that mkianza kula sio tena kunyanyuka nyanyuka mara umesahau kijiko mara chumvi… e. t. c. (alafu tupia kitu red ikiwezekana ili jamaa apate chakula kila mahala… macho, ubongo, tumbo - na… you know what I mean…)

  • Chakula chaweza tumika na wakaka kuweza msogeza the woman he has fallen for karibu… Kwa wale wachache ambao wamebahatika kua wapishi wazuri then they are in LUCK!.. Kama unakwako mkaribishe the Lady for an evening kwako… Pika whatever food you can cook best… kama ni chips, macaroni, rice… whatever for with food we ladies are not that complicated in choosing what to eat as long as it is good food. Take note kua siku ukimkaribisha akaja na ukampikia as much as utakua na usongo… don’t sleep with her siku hio – itafanya the lady apate a more lasting positive impression of how good a gentleman you are. Otherwise kama ni mpenzi wako ambae mmeshawahi kuvunja amri….Kwa wale wasio jua kupika waweza mtoa mdada out ukajikakamaa kidogo na kumpeleka sehemu nzuri ambayo kuna a good buffet and good music back ground… yaani sehemu ambayo imekaa kaa ki kuwaweka wepenzi/wenza karibu…

  • Chakula pia kinaweza haribu mahusiano hasa kati ya wenza/wapenzi… Hii hutokea saana pale mdada/mmama mapishi nyumbani kwake yamemshinda kabisaa… In short hajui kupika… wakaka/baba wengine hawana makuu na huvumilia na kuona sawa tu… (ni wachache by the way…) BUT Issue ni kwa wale ambao kalelewa katika familia ambayo they are Great Cooks… yaani kazoea chakula kizuri na kitamu pia… yaani hata kama kala tu Ugali na dagaa… huo ugali ni ugali umesongwa hasa!… na hizo dagaa mazagazaga yoote from kitunguu saumu, nazi, nyanya/hoho/carrot/vitunguu, curry powder to perfection. (Huyu akipata nyumba ndogo anajua wajibu wake katika sector ya chakula usishangae ukitangaziwa mke mdogo….)

  • Na kwa wale ambao ni busy wifes in the sense kua kazi yake haimpi kabisa nafasi ya kupika… kila unapopata msaidizi walau msimamie mpaka ajue… na hata akijua ni vizuri once a week hasa kama Sunday unaandaa chakula mwenyewe kwa mkono wako from breakfast ya ukweli (walau hapa epuka vitafunwa vya kununua unashtulia kidogo vitu kama maandazi/chapatti/kalmati/ sambusa and the like..); Lunch ya uhakika… to a light dinner. Ni vizuri dinner ikiwa light sababu ni usiku haipendezi kula vitu vizito hivyo lunch ni vizuri kikapikwa kizito na cha kueleweka.

  1. Chakula katika tendo lenyewe la 6/6
Kuna vyakula hutumika kabla tu ya tendo, wakati wa tendo na baada ya tendo lenyewe la 6/6… Jinsi na namna gani hutumika naomba nisiende in detail for uzi wangu usije ukarushwa jukwaa lile lingine na sina access… In short kwa kiasi kikubwa naamini kua wengi twatambua… Vyakula husaidia saana kuhamasisha hasa kwa wale ambao ni wagumu kuamka hamu/ ambao hupanga wavunje hio amri siku nziima, au wale ambao wako honey moon e. t. c. Utumiaji wa vitu kama asali.. matunda kama ndizi/ strawberries/passions.. ice creams… vinywaji… ice cubes … chocolates.. pili pili (mmh! This is exteme but hutumika na wachache…) na vinginevyo vyaweza spice up your relationship/sex life and intensify your feelings

DISCLAIMER…

Sio lazima kua ukifanya the above kuhusu chakula kua waweza kujenga uhusiano mzuri zaidi … (tumeumbwa tofauti… wanaume/wanawake wengine are so selfish and fail to appreciate the little yet incredible things their love ones do for them). Ila naamini kwa asilimia zaidi ya 80% it works!!! Na naamini ukifanya hivyo kwa a person who is appreciative and loves Great Food and Sex… itajenga zaidi….

Pamoja saana.

AshaDii

The above post is sorely my observation and analysis… Tafadhali JF member(s) toa mawazo/challenges/maswali kuhusu Mada... na mtazamo wako....
 
Hapo Ashadii,umenigusa ndipo,manake sikuizi kazi tumeziweka mbele time hakuna lakini Inshallah japo hata wala na mchuzi wa chuku chuku nipike.
 
Hapo Ashadii,umenigusa ndipo,manake sikuizi kazi tumeziweka mbele time hakuna lakini Inshallah japo hata wala na mchuzi wa chuku chuku nipike.

Nafurahi umekubaliana na mimi na ni wazi utafanyia kazi walau siku moja moja....
Umenifurahisha wali na chuku chuku... wapi na wapi, si bora hata ukaange mayai faster??
 
ashadii, hapo umemaliza, mwenye masikio atasikia.
1 good quality food with a good layout will melt a stony heart!
2 ile tabia ya kizamani ya vyombo vizuri ni vya wageni tuiache kabisa!live today,umenunua vyombo vyako,let ur family enjoy them.wageni watakachobahatisha ndo size yao!
3 kubadilisha vyombo vya kutengea chakula kila mara hufanya kikawa more interesting! sipendi kunywa chai na kikombe cheupe kila siku, ama wali na sahani ya bluu maisha yote! sahani ya dinner iwe tofauti na ya lunch (mchina katusaidia vyote vunapatikana kwa bei rahisi,lol)
 
Wifi ni dhahiri kakangu kapata.... Dah! nimefurahishwa....
 
wifi mtarajiwa, wali na mayai tena kama tuko shule? bora chuku chuku bana, talaka itanukia,lol

ha ha ha.... siwezi kabisa chuku chuku na wali... unanishinda....lol
but kama mhusika ni kakako... mbona mda unakuwepo, yaani hata
haiwi chuku chuku.... inakua mlo ulokamilika....
 
patia picha chukuchuku hii ya kuku wa kienyeji, beef, mbuzi au bata: imo viazi ulaya kidogo, kitunguu maji, karoti,hoho,koli flower. green beans, zuchini na vile vitunguu vyeupe vya supu! yaani hata mchuzi haupitilizi chini ya wali wifi! inabidi wknd ijayo uje aisee,lol!
ha ha ha.... siwezi kabisa chuku chuku na wali... unanishinda....lolbut kama mhusika ni kakako... mbona mda unakuwepo, yaani hatahaiwi chuku chuku.... inakua mlo ulokamilika....
 
patia picha chukuchuku hii ya kuku wa kienyeji, beef, mbuzi au bata: imo viazi ulaya kidogo, kitunguu maji, karoti,hoho,koli flower. green beans, zuchini na vile vitunguu vyeupe vya supu! yaani hata mchuzi haupitilizi chini ya wali wifi! inabidi wknd ijayo uje aisee,lol!

aiseee.... who am i to resist?? nakuja haraka!! naruhusiwa kumleta wa ndani wangu??
 
Asha haya mambo yako ya misosi na maandalizi yake, sisi huku kwetu uswahilini hatuna ustaarabu kama huu.........
nahisi imekula kwangu hii....lol.....
 
Asha haya mambo yako ya misosi na maandalizi yake, sisi huku kwetu uswahilini hatuna ustaarabu kama huu.........
nahisi imekula kwangu hii....lol.....

Sio kweli Bacha.. acha visingizio, hakuna kitu hapo kinachoashiria
haitakiwi uswahilini... mbona mie nipo uswahilini pia??

Mzima wewe??
 
  1. Chakula na nafasi yake katika mahusiano ya Mapenzi… (Wenza..)
Kitu kimoja wapo ambacho ni muhimu saaana katika mahusiano ni Chakula…. Ni wazi kua kaka/baba zetu wanapenda Sex, Great Food, Good Drinks mengine ndo hufuata… Wadada/wamama We love Good Life, Attention, Kujitambua then vitu kama Sex, Good Food and Good Drinks hufuata hapo… (sio woote kwa wasio kubali relax endelea kuto kubali…). Hivyo basi with Great Food you can say volume of words… Show the extent of your affection and Say the words I Love you… and this Dears is with food – Not only food, But Great Food… Chakula waweza onesha intensity ya mapenzi yako saa ingine kuliko maneno… It has that power.. angalia hii…

Nisaidie recipe moja ya wiki nzima nianze kuchangamsha majambo hapa jikoni..............................au labda kwanza nikimbilie sokoni kukusanya mavituzi................
 
Nisaidie recipe moja ya wiki nzima nianze kuchangamsha majambo hapa jikoni..............................au labda kwanza nikimbilie sokoni kukusanya mavituzi................

ha ha ha Rutah... ukirudi tuarifiane basi...
 
Asha haya mambo yako ya misosi na maandalizi yake, sisi huku kwetu uswahilini hatuna ustaarabu kama huu.........<BR>nahisi imekula kwangu hii....lol.....
 
Asha haya mambo yako ya misosi na maandalizi yake, sisi huku kwetu uswahilini hatuna ustaarabu kama huu.........<BR>nahisi imekula kwangu hii....lol.....

Bacha uko uswahilini mnalia chini? je unaishi nje ya chumba? hamli?
inatakiwa kila mtu aishi kwa level yake... hata kama mtu chumba ni kimoja
(natolea mfano for i know it does not apply kwako...) lazima kuna mpangilio
kua kona hii kitanda, upand huu ni kochi/sofa meza na stools hata mbili, yaani
hio hio ya level yako you have to make the best of it.... Hivyo nasisitiza
tena... acha visingizio...
 
Asha sie kwetu huku uswahilini tunakula kwa pamoja,
si unakumbuka ule mchezo wa kitoto wa kula mbakishie baba...............?
hatuna mambo sijui ya sahani kila mtu na yake, sijui kuwasha candle,
ukiona mshumaa umewashwa basi ni mpaka TANESCO wamechukua kilicho chao,
Matunda sijui, ndo hivo tena kuyala mpaka baba afurahi au ujue kuna mgonjwa hapo home..................
mmmh, wewe Asha karibu kwetu ujionee mwenyewe, kila kukicha afadhali ya jana lol..........
 
Back
Top Bottom