bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 750
- 1,743
Kuna kiwango cha ufahamu ukifika, unashindwa kujibu swali la umri sababu umri unaozungumzwa ni umri wa mwili siyo wako. Wewe mwenyewe umri wako huujui maana hujui kitu kinachoitwa muda. Huwezi tena kusema asili yako ni wapi kwa kuwa unajua kuwa asili yako ni ulimwengu. Wewe na ulimwengu ni kitu kimoja.
Unafika hatua mtu akikuuliza swali "tukifa tunaenda wapi?", unatamani kumzaba makofi. Kwani kabla ya kufa ulikuwa wapi. Unagundua kwamba wajinga wanaotaka uwaze unaenda wapi, ni watu ambao hawajawahi kuishi lakini wanaogopa kufa. Wanaogopa hali ambayo tayari wapo. Kifo siyo kuvua mwili ila ni kufika ukomo wa ufahamu. Unakufa pale ufahamu wako unaposhika breki. Aliyevua mwili hajafa bali amebadili dimension. Huyu yupo juu zaidi kuliko mtu anayepumua lakini kaamua kuwa zombie.
Zombie ni kiumbe mwenye mwili na umbile la mtu lakini ana ufahamu wa mnyama. Iwapo wewe ni mtu lakini umekuwa programed kufikiri katika mzingo mdogo huku ukionywa kwamba kufikiri au kuhoji zaidi utakufuru, sasa tofauti yako na zombie ni nini? Ukiambiwa kitu unakimbilia kwenye kijitabu kuchomoa mstari. Unatamani umzibue mtu kofi, ili brain ifanye reset. Any way nakutakia siku njema.
Mimi siyo adui yako, ni mpinzani wa ulichoaminishwa.