The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 836
Viongozi wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya wanaokutana katika mkutano wa kilele mjini Brussels, wamekubali kurefusha vikwazo vyao dhidi ya Urusi kwa muda wa miezi sita, kwa mujibu wa duru za kidiplomasia.EU tayari imepitisha "vifurushi" 17 vya vikwazo tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 24, 2022. Vikwazo hivi lazima viongezwe upya kwa kauli moja na nchi 27 wanachama wa EU kila baada ya miezi sita, na Hungary, nchi iliyo na uhusiano wa karibu na Urusi katika Umoja wa Ulaya, inatishia kuvipinga mara kwa mara.
Mnamo mwezi Januari, Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban aliendelea kuonyesha msimamo wake hadi dakika ya mwisho, kabla ya kutoa idhni yake.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya pia wamejadili siku ya Alhamisi kifurushi cha 18 cha vikwazo, vilivyopendekezwa wiki mbili zilizopita na Tume ya Ulaya, lakini hakuna uamuzi ambao unaweza kufanywa, wakati huu kutokana na kura ya turufu ya Slovakia.