Umoja wa Ulaya (EU) ujue Tanzania ni Taifa huru kwa 100%

goodluck5

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
4,433
2,000
Badala uwalaumu watawala (mabwana zako wanaokulisha) kwa kutozingatia utawala bora na demokrasia nchini unawalaumu watu wanaokutaka uzingatie vigezo vigezo hivyo kwa raia unawaongoza ili kupata misaada hiyo?

Kama tz ni nchi huru kama unavyojitapa si ingekuwa inaikataa hiyo misaada toka zamani, misaada (yenye masharti) ya nn sasa wakati wewe ni nchi huru?
 
Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
2,113
2,000
Zitto Kabwe, na Tundu Lissu wanadhani Wanawakomoa Watanzania, wanajikomoa wawo wenyewe maana wameisha waonesha Watanzania kuwa kumbe walikuwa wametumwa ili kutuletea machafuko nchini ili Watanzania tuwe na hofu.

Watanzania tuliiisha amua hatutaki upumbafu wao na hatuna hofu (Elimu tunayo, Ardhi tunayo, Fedha tunazo, siasa tunazo, na Watanzania tupo kwa ajili ya kufanya kazi. )

Ushauri: Serikali ikithibitisha Janja ya EU imfukuze nchini Balozi wa EU, Marekani na Ujerumani na Dunia itangaziwe kwamba kwasasa hatuna shughuli nao na Maeneo yao ya ubalozi Yajengwe Mazizi ya kufugia Samaki, Ngedele, na Nguruwe. Na Watangaziwe wazi.
Habari za asubui mh pole×2.
 
Matrix19

JF-Expert Member
Feb 24, 2020
866
1,000
Mbona hujaandika pia waache kupokea Madawa na chanjo za misaada,miradi ya kilimo , ujenzi wa mashule na zana za kufundishia na kadhalika?
 
jogoo wa maajabu

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
308
500
Hatuwezi ishi bila misaada? Ama kweli wazungu wamekuoa
Hatuwezi kuishi bila misaada ya EU na EU inaweza kuishi bila biashara na chochote kutoka Tanzania.

Jiandae kuandika uzi mwingine maana kuna list ya Icc itakuja siku si nyingi kilaza wa Lumumba wewe
 
Kilawo

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
786
1,000
Zitto Kabwe, na Tundu Lissu wanadhani Wanawakomoa Watanzania, wanajikomoa wawo wenyewe maana wameisha waonesha Watanzania kuwa kumbe walikuwa wametumwa ili kutuletea machafuko nchini ili Watanzania tuwe na hofu.
Watanzania tuliiisha amua hatutaki upumbafu wao na hatuna hofu (Elimu tunayo, Ardhi tunayo, Fedha tunazo, siasa tunazo, na Watanzania tupo kwa ajili ya kufanya kazi. )
Ushauri: Serikali ikithibitisha Janja ya EU imfukuze nchini Balozi wa EU, Marekani na Ujerumani na Dunia itangaziwe kwamba kwasasa hatuna shughuli nao na Maeneo yao ya ubalozi Yajengwe Mazizi ya kufugia Samaki, Ngedele, na Nguruwe. Na Watangaziwe wazi.
Eti pesa tunazo
 
yomboo

JF-Expert Member
May 9, 2015
6,235
2,000
Na Mwandishi Wetu

Zipo taarifa zinasambaa kwamba bunge la Jumuiya ya ulaya limeazimia kuifutia Tanzania misaada inayokadiriwa kufikia shilingi trillion 1.6 kwa muda wa miaka 6 kutoka 2014-2020 ambazo ni wastani wa shilingi bilion 267 kwa mwaka. Kiwango hiki cha fedha ni kidogo mno kulika heshima ya uhuru wetu kama nchi.

Ni muhimu jumuiya ya ulaya ikajua:-

1) Haki na Demokrasia:

Kama ambavyo Tanzania haina mamlaka ya kuwatafsiria watu wa Ulaya haki na demokrasia zao, halikadhalika watu wa Ulaya hawana madaraka ya kuwatafsiria Watanzania haki na demokrasia zao. Tanzania ni Taifa huru kama ilivyo hizo nchi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya.

2) Hiyo inayodaiwa kuwa ni misaada haikuwa misaada:

Mtu akikupora shilingi 1,000 kwa mfano, halafu akaamua kukurudishia shilingi 250, hapo hajakupa msaada wowote.

Kwa miaka nenda rudi mataifa na mashirika ya Ulaya na nchi zingine zinazojiita zilizoendelea, walilazimisha Tanzania na nchi za Afrika kwa ujumla kuwapa wawekezaji wao kitu kilichoitwa "tax holidays" yaani misamaha ya kulipa kodi. Na hii ilikuwa ni uhalalishaji wa wizi, "tax holidays are a legal fraud."

Kampuni moja imewahi kufanya biashara Tanzania kwa miaka 18 bila kulipa kodi kwa madai ya kuwa ilikuwa haipati faida. Hiyo kweli inaingia akilini? Kwa nini kampuni ya kibiashara iendelee kufanya biashara miaka 18 wakati ilikuwa haipati faida?

Ukweli ni huu: Makampuni na mataifa ya Ulaya yamekuwa yanatuibia kupitia ukwepaji na misamaha ya kodi. Hivyo basi, hizo £626 milioni ambazo wamekuwa wanatupa tangu hiyo 2014, haikuwa ni msaada bali fedha zetu ambazo walitakiwa watulipe kama kodi.

Marekani, mathalani, bajeti yake yote ya Ulinzi inakuwa - "covered by corporate tax". Kodi za makampuni ni mipesa mingi sana. Halafu wao (the developed countries) wanalazimisha makampuni yao yasilipe kodi yanapowekeza nje ya nchi zao. What a con?

3) Jumuiya ya Ulaya haina demokrasia:

Kama kuna Jumuiya hapa duniani ambayo haina demokrasia na inaminya uhuru wa raia wake, basi ni Jumuiya ya Ulaya. 'Structure' ya Umoja wa Ulaya ni ya kitapeli ' per se.' Kwa nini ninasema hivyo:
Umoja wa Ulaya una mihimili mitatu.

(a) Bunge la Umoja wa Ulaya: Hili lina wabunge waliopigiwa kura na raia wa nchi wanazotoka.

(b) Halmashauri au 'Council'. Hapa kuna wajumbe walioteuliwa na Serikali za nchi wanachama.

(c) Kuna 'Commission' au Kamisheni. Wajumbe wa hii Commission wamejichagua wenyewe - ni 'self-appointed clique.' Hawapigiwi kura; na raia wa Jumuiya ya Ulaya hawana njia ya kuwatoa hawa watu kwenye nyadhifa zao.

Utapeli mkubwa zaidi unakuja kwenye mgao wa madaraka. Hii Commission ndiyo inayotunga sheria na kuzipeleka Bungeni. Na hao wabunge hawaruhusiwi kubadili sentensi, neno hata nukta au koma kwenye mswaada. Wabunge kazi yao ni kupiga kura ya "ndiyo" au "hapana."

Jamani hivi, hiyo ndiyo demokrasia ya rangi gani? Umoja wa Ulaya kweli wana miguu ya kusimamia na kutukosoa Watanzania?

4) Soko la Umoja wa Ulaya.

Umoja wa Ulaya, ni asilimia kumi na mbili tu (12%) ya Soko la Dunia. Hata kama wakitutenga, Tanzania au Afrika itakuwa na asilimia 88 (88%) ya soko la dunia la kufanya nalo biashara.

Ushauri Wangu.

Serikali ya Tanzania isitishike na maamuzi ya kikoloni yaliyotolewa na Umoja wa Ulaya. Tanzania siyo koloni, ni Taifa huru; na tupo huru milele (we are free forever."

Cha Kufanya:
  • Tanzania ifute misamaha yote ya kodi kwa makampuni ya nje.
  • Tanzania iendelee kukusanya kodi kwa dhati kama inavyofanya.

Matokeo yatakuwa ni Taifa kunufaika kwa sababu mirija ya waliokuwa wanatunyonya tutakuwa tumeikata.

Tanzania ilipata kuwa kisiwa wakati wa vita vya kulikomboa bara la Afrika; kwa maana ya kuwa hakuna nchi ambayo ilijitolea kwenye masuala ya ukombozi kwa upeo ambao Tanzania ilifanya - ndiyo kusema zama hizo tulikuwa ni kisiwa. Leo, tusihofu kuwa kisiwa tena kwenye vita hii ya kujikomboa kiuchumi. Hivyo,basi tutake tusitake tutakuwa ni kisiwa kwa sababu hakuna atatupigania, zaidi ya sisi wenyewe.

Kwa hiyo kauli za 'hatuwezi kujifanya kisiwa ni za kipuuzi sana.'
Hawa, yaani Umoja wa Ulaya inawauma kuona kuwa taifa ambalo walisadiki kuwa ni duni, si duni tena.

mkali@.co.uk
19/11/2020 View attachment 1630297
Dah yaani umeandika ujinga huwa unawaza kwa kutumia mku.ndu ww..

By the way 27m Euro zirudishwe kwa wenyewe hayo mengine hayanihusu

Taifa la wajinga na matakataka ninyi
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
11,973
2,000
Hii serikali dhalimu ina watetezi wa kiwango cha chini sana. Kwa hoja tatu kati ya lundo la utopolo ulloweka;
1.Tanzania ina aina yake ya demokrasia, ni sawa. Hii ya kuingiza mabegi kura zimeshapigwa mlikubaliana na nani? Mbona upande wa pili haukupewa nafasi ya kuingiza mabegi ya kura kama CCM? Hata vituo vya kujumlishia kura tu watu walikamatwa?
2.Hamtaki misaada yao maana mnawapa 1000/- wao wanawapa 250/-. Hizi hesabu sijui umezitoa kwa nani? Mbona mnapopata misaada hiyo media zote za chama chenu na kuwaita haohao marafiki wa maendeleo/Wanaume? Wakiwakosoa wanabadilika kuwa Mabeberu, sijui Beberu ni jike?
3.Soko la Ulaya ni 12% tu ya soko la Dunia. Hiki ni kichekesho. Hivi kama ABDALLA ananunua 10% ya mpunga kijijini lakini mpunga wako wewe ananunua 80%, huyo kwako bado ni 10%?
Mnapokubali kupokea kuweni waungwana, mnapokosea kubalini kukosolewa maana kwa utashi wenu mlisaini mikataba ya kimataifa ambayo Leo mnaivunja makusudi.
 
Papy ndombe

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
3,451
2,000
Watoto sio wa jirani ni wa Jamii nzima thus hata Kama ni wako ukiwatesa ukiwanyima haki zao lazima Jamii itachukua hatua. Maana haki ikipotea Jamii ndio itaingia gharama za kuwahudumia.
 
Papy ndombe

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
3,451
2,000
Wenzetu ukiwa uncivilized, uneducated and not matured enough upewi lesseni ya kuendesha gari ili kuepuka migogoro
 
uttoh2002

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
5,554
2,000
Na Mwandishi Wetu

Zipo taarifa zinasambaa kwamba bunge la Jumuiya ya ulaya limeazimia kuifutia Tanzania misaada inayokadiriwa kufikia shilingi trillion 1.6 kwa muda wa miaka 6 kutoka 2014-2020 ambazo ni wastani wa shilingi bilion 267 kwa mwaka. Kiwango hiki cha fedha ni kidogo mno kulika heshima ya uhuru wetu kama nchi.

Ni muhimu jumuiya ya ulaya ikajua:-

1) Haki na Demokrasia:

Kama ambavyo Tanzania haina mamlaka ya kuwatafsiria watu wa Ulaya haki na demokrasia zao, halikadhalika watu wa Ulaya hawana madaraka ya kuwatafsiria Watanzania haki na demokrasia zao. Tanzania ni Taifa huru kama ilivyo hizo nchi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya.

2) Hiyo inayodaiwa kuwa ni misaada haikuwa misaada:

Mtu akikupora shilingi 1,000 kwa mfano, halafu akaamua kukurudishia shilingi 250, hapo hajakupa msaada wowote.

Kwa miaka nenda rudi mataifa na mashirika ya Ulaya na nchi zingine zinazojiita zilizoendelea, walilazimisha Tanzania na nchi za Afrika kwa ujumla kuwapa wawekezaji wao kitu kilichoitwa "tax holidays" yaani misamaha ya kulipa kodi. Na hii ilikuwa ni uhalalishaji wa wizi, "tax holidays are a legal fraud."

Kampuni moja imewahi kufanya biashara Tanzania kwa miaka 18 bila kulipa kodi kwa madai ya kuwa ilikuwa haipati faida. Hiyo kweli inaingia akilini? Kwa nini kampuni ya kibiashara iendelee kufanya biashara miaka 18 wakati ilikuwa haipati faida?

Ukweli ni huu: Makampuni na mataifa ya Ulaya yamekuwa yanatuibia kupitia ukwepaji na misamaha ya kodi. Hivyo basi, hizo £626 milioni ambazo wamekuwa wanatupa tangu hiyo 2014, haikuwa ni msaada bali fedha zetu ambazo walitakiwa watulipe kama kodi.

Marekani, mathalani, bajeti yake yote ya Ulinzi inakuwa - "covered by corporate tax". Kodi za makampuni ni mipesa mingi sana. Halafu wao (the developed countries) wanalazimisha makampuni yao yasilipe kodi yanapowekeza nje ya nchi zao. What a con?

3) Jumuiya ya Ulaya haina demokrasia:

Kama kuna Jumuiya hapa duniani ambayo haina demokrasia na inaminya uhuru wa raia wake, basi ni Jumuiya ya Ulaya. 'Structure' ya Umoja wa Ulaya ni ya kitapeli ' per se.' Kwa nini ninasema hivyo:
Umoja wa Ulaya una mihimili mitatu.

(a) Bunge la Umoja wa Ulaya: Hili lina wabunge waliopigiwa kura na raia wa nchi wanazotoka.

(b) Halmashauri au 'Council'. Hapa kuna wajumbe walioteuliwa na Serikali za nchi wanachama.

(c) Kuna 'Commission' au Kamisheni. Wajumbe wa hii Commission wamejichagua wenyewe - ni 'self-appointed clique.' Hawapigiwi kura; na raia wa Jumuiya ya Ulaya hawana njia ya kuwatoa hawa watu kwenye nyadhifa zao.

Utapeli mkubwa zaidi unakuja kwenye mgao wa madaraka. Hii Commission ndiyo inayotunga sheria na kuzipeleka Bungeni. Na hao wabunge hawaruhusiwi kubadili sentensi, neno hata nukta au koma kwenye mswaada. Wabunge kazi yao ni kupiga kura ya "ndiyo" au "hapana."

Jamani hivi, hiyo ndiyo demokrasia ya rangi gani? Umoja wa Ulaya kweli wana miguu ya kusimamia na kutukosoa Watanzania?

4) Soko la Umoja wa Ulaya.

Umoja wa Ulaya, ni asilimia kumi na mbili tu (12%) ya Soko la Dunia. Hata kama wakitutenga, Tanzania au Afrika itakuwa na asilimia 88 (88%) ya soko la dunia la kufanya nalo biashara.

Ushauri Wangu.

Serikali ya Tanzania isitishike na maamuzi ya kikoloni yaliyotolewa na Umoja wa Ulaya. Tanzania siyo koloni, ni Taifa huru; na tupo huru milele (we are free forever."

Cha Kufanya:
  • Tanzania ifute misamaha yote ya kodi kwa makampuni ya nje.
  • Tanzania iendelee kukusanya kodi kwa dhati kama inavyofanya.

Matokeo yatakuwa ni Taifa kunufaika kwa sababu mirija ya waliokuwa wanatunyonya tutakuwa tumeikata.

Tanzania ilipata kuwa kisiwa wakati wa vita vya kulikomboa bara la Afrika; kwa maana ya kuwa hakuna nchi ambayo ilijitolea kwenye masuala ya ukombozi kwa upeo ambao Tanzania ilifanya - ndiyo kusema zama hizo tulikuwa ni kisiwa. Leo, tusihofu kuwa kisiwa tena kwenye vita hii ya kujikomboa kiuchumi. Hivyo,basi tutake tusitake tutakuwa ni kisiwa kwa sababu hakuna atatupigania, zaidi ya sisi wenyewe.

Kwa hiyo kauli za 'hatuwezi kujifanya kisiwa ni za kipuuzi sana.'
Hawa, yaani Umoja wa Ulaya inawauma kuona kuwa taifa ambalo walisadiki kuwa ni duni, si duni tena.

mkali@.co.uk
19/11/2020 View attachment 1630297

Kaka uhuru unaanzia kwenye kujimudu ki uchumi, Yani wewe mwenyewe kama hauna hela na unategemea mke wako ujue uhuru hauna!

September hii tumekula euro za watu na wanatusimanga nazo, huo uhuru tunatoka nao wapi sasa? Kuwahi na akili nyie watu na mjitahidi kuficha ujinga wenu utawasaidia baadaye!

Pesa una nguvu, uhuru sio kutembea mtaa ni, Uhuru ni kumtegemea mtu bila fedha, we cant move an inch bila Hawa wazungu mbali watu kana; Yani wakifunga tu bidhaa Zao tunaanza tafutana huku!
 
Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
6,015
2,000
Zitto Kabwe, na Tundu Lissu wanadhani Wanawakomoa Watanzania, wanajikomoa wawo wenyewe maana wameisha waonesha Watanzania kuwa kumbe walikuwa wametumwa ili kutuletea machafuko nchini ili Watanzania tuwe na hofu.
Watanzania tuliiisha amua hatutaki upumbafu wao na hatuna hofu (Elimu tunayo, Ardhi tunayo, Fedha tunazo, siasa tunazo, na Watanzania tupo kwa ajili ya kufanya kazi. )
Ushauri: Serikali ikithibitisha Janja ya EU imfukuze nchini Balozi wa EU, Marekani na Ujerumani na Dunia itangaziwe kwamba kwasasa hatuna shughuli nao na Maeneo yao ya ubalozi Yajengwe Mazizi ya kufugia Samaki, Ngedele, na Nguruwe. Na Watangaziwe wazi.
Rudisheni pesa za Covid,si hakuna covid hapa nchini?mnajifanya wajanja wakati mnatembeza bakuli tena kwa sababu za uongo uongo
 
MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,134
2,000
Ni sawa ulivyoeleza ila nami najiuliza kwanini tuna mwakilishi wao hapa nchini huku tukijua ni taasisi ya Kitapeli. Pili matapeli wanawezaje wakatupatia misaada ikiwemo zile Euro za Covid-19 ambazo hazijulikani zilipo.
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
13,621
2,000
Hatuwezi kuishi bila misaada ya EU na EU inaweza kuishi bila biashara na chochote kutoka Tanzania.

Jiandae kuandika uzi mwingine maana kuna list ya Icc itakuja siku si nyingi kilaza wa Lumumba wewe
Familia yako ndio inaweza kuishi bila misaada ya EU.

Kwanza chadema hamuoni aibu kulilia misaada?

Mnatuaibisha wanaume
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom