Rais Dkt. Mwinyi akutana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa EU

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Naibu Mkurugenzi Mkuu Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Martin Seychell na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe 7 Desemba 2023.

Katika mazungumzo yao wamegusia uhusiano uliopo kati ya Zanzibar na Umoja wa Ulaya katika kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo elimu, nishati, afya, maji na miundombinu nchini.

Pia sekta ya utalii, uchumi wa buluu hususani uvuvi na kilimo cha mwani.

Kwa upande mwingine Rais Dk. Mwinyi amewashukuru Uongozi wa bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) kwa kufanyia vikao vyao Zanzibar ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika nje ya Bara la ulaya na Amerika pamoja na kuisadia Zanzibar hususani katika sekta ya elimu.

IMG-20231207-WA0013.jpg
IMG-20231207-WA0012.jpg
IMG-20231207-WA0011.jpg
IMG-20231207-WA0015.jpg
IMG-20231207-WA0016.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom