Umoja wa Ulaya (EU) ujue Tanzania ni Taifa huru kwa 100%

Ni taifa huru lisilotaka raia wake wawe huru, ni taifa huru lisilotoa haki kwa raia wake, ni taifa huru linalo lazimisha raia wake kuongozwa na viongozi ambao hawakuwachagua, ni taifa huru ambalo hata kura ya mgombea wa upinzani aliyejipigia kura kura yake inabadilikia ndani ya sanduku la kura na kuonyesha kuwa alimpigia mgombea wa CCM.
 
Umeandika utopolo ukijua hii ni HIPC nation
Na Mwandishi Wetu

Zipo taarifa zinasambaa kwamba bunge la Jumuiya ya ulaya limeazimia kuifutia Tanzania misaada inayokadiriwa kufikia shilingi trillion 1.6 kwa muda wa miaka 6 kutoka 2014-2020 ambazo ni wastani wa shilingi bilion 267 kwa mwaka. Kiwango hiki cha fedha ni kidogo mno kulika heshima ya uhuru wetu kama nchi.

Ni muhimu jumuiya ya ulaya ikajua:-

1) Haki na Demokrasia:

Kama ambavyo Tanzania haina mamlaka ya kuwatafsiria watu wa Ulaya haki na demokrasia zao, halikadhalika watu wa Ulaya hawana madaraka ya kuwatafsiria Watanzania haki na demokrasia zao. Tanzania ni Taifa huru kama ilivyo hizo nchi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya.

2) Hiyo inayodaiwa kuwa ni misaada haikuwa misaada:

Mtu akikupora shilingi 1,000 kwa mfano, halafu akaamua kukurudishia shilingi 250, hapo hajakupa msaada wowote.

Kwa miaka nenda rudi mataifa na mashirika ya Ulaya na nchi zingine zinazojiita zilizoendelea, walilazimisha Tanzania na nchi za Afrika kwa ujumla kuwapa wawekezaji wao kitu kilichoitwa "tax holidays" yaani misamaha ya kulipa kodi. Na hii ilikuwa ni uhalalishaji wa wizi, "tax holidays are a legal fraud."

Kampuni moja imewahi kufanya biashara Tanzania kwa miaka 18 bila kulipa kodi kwa madai ya kuwa ilikuwa haipati faida. Hiyo kweli inaingia akilini? Kwa nini kampuni ya kibiashara iendelee kufanya biashara miaka 18 wakati ilikuwa haipati faida?

Ukweli ni huu: Makampuni na mataifa ya Ulaya yamekuwa yanatuibia kupitia ukwepaji na misamaha ya kodi. Hivyo basi, hizo £626 milioni ambazo wamekuwa wanatupa tangu hiyo 2014, haikuwa ni msaada bali fedha zetu ambazo walitakiwa watulipe kama kodi.

Marekani, mathalani, bajeti yake yote ya Ulinzi inakuwa - "covered by corporate tax". Kodi za makampuni ni mipesa mingi sana. Halafu wao (the developed countries) wanalazimisha makampuni yao yasilipe kodi yanapowekeza nje ya nchi zao. What a con?

3) Jumuiya ya Ulaya haina demokrasia:

Kama kuna Jumuiya hapa duniani ambayo haina demokrasia na inaminya uhuru wa raia wake, basi ni Jumuiya ya Ulaya. 'Structure' ya Umoja wa Ulaya ni ya kitapeli ' per se.' Kwa nini ninasema hivyo:
Umoja wa Ulaya una mihimili mitatu.

(a) Bunge la Umoja wa Ulaya: Hili lina wabunge waliopigiwa kura na raia wa nchi wanazotoka.

(b) Halmashauri au 'Council'. Hapa kuna wajumbe walioteuliwa na Serikali za nchi wanachama.

(c) Kuna 'Commission' au Kamisheni. Wajumbe wa hii Commission wamejichagua wenyewe - ni 'self-appointed clique.' Hawapigiwi kura; na raia wa Jumuiya ya Ulaya hawana njia ya kuwatoa hawa watu kwenye nyadhifa zao.

Utapeli mkubwa zaidi unakuja kwenye mgao wa madaraka. Hii Commission ndiyo inayotunga sheria na kuzipeleka Bungeni. Na hao wabunge hawaruhusiwi kubadili sentensi, neno hata nukta au koma kwenye mswaada. Wabunge kazi yao ni kupiga kura ya "ndiyo" au "hapana."

Jamani hivi, hiyo ndiyo demokrasia ya rangi gani? Umoja wa Ulaya kweli wana miguu ya kusimamia na kutukosoa Watanzania?

4) Soko la Umoja wa Ulaya.

Umoja wa Ulaya, ni asilimia kumi na mbili tu (12%) ya Soko la Dunia. Hata kama wakitutenga, Tanzania au Afrika itakuwa na asilimia 88 (88%) ya soko la dunia la kufanya nalo biashara.

Ushauri Wangu.

Serikali ya Tanzania isitishike na maamuzi ya kikoloni yaliyotolewa na Umoja wa Ulaya. Tanzania siyo koloni, ni Taifa huru; na tupo huru milele (we are free forever."

Cha Kufanya:
  • Tanzania ifute misamaha yote ya kodi kwa makampuni ya nje.
  • Tanzania iendelee kukusanya kodi kwa dhati kama inavyofanya.

Matokeo yatakuwa ni Taifa kunufaika kwa sababu mirija ya waliokuwa wanatunyonya tutakuwa tumeikata.

Tanzania ilipata kuwa kisiwa wakati wa vita vya kulikomboa bara la Afrika; kwa maana ya kuwa hakuna nchi ambayo ilijitolea kwenye masuala ya ukombozi kwa upeo ambao Tanzania ilifanya - ndiyo kusema zama hizo tulikuwa ni kisiwa. Leo, tusihofu kuwa kisiwa tena kwenye vita hii ya kujikomboa kiuchumi. Hivyo,basi tutake tusitake tutakuwa ni kisiwa kwa sababu hakuna atatupigania, zaidi ya sisi wenyewe.

Kwa hiyo kauli za 'hatuwezi kujifanya kisiwa ni za kipuuzi sana.'
Hawa, yaani Umoja wa Ulaya inawauma kuona kuwa taifa ambalo walisadiki kuwa ni duni, si duni tena.

mkali@.co.uk
19/11/2020View attachment 1630297
 
Nimeogopa kusikia kwa mwaka watu 72,000 wanaambukizwa HIV na ARV kwa mwezi ni $150-170 kwa mgonjwa mmoja na wazungu wanatununulia ...Waimba mapambio endeleeni tu ..mtanzania mnyonge anaweza kutumia 400,000 kununua ARV kwa mwezi ..Twafaaaa
 
hera za ARV ?? kama tumeweza kununua mandege makubwa sembusee hvyo vipipi vya kumeza anko mbona hutumii ubongo...tz ni matajiri.
Kama hauamini utaona Kabudi soon anapanda ndege kwenda kuwabembeleza wazungu bajeti ya nchi mpaka Mabeberu wachangie, hela ya ARV Mabeberu umesahau tuliletewa vyandarua toka marekani?
Kama upo Dsm barabara ya kutoka Kwa Kakobe kwenda Sinza Mori financer ni World Bank pita usome ubao wa project pale.
 
Hahahhha wanakuhitaji kwa nini wewe fukara ambaye kila siku unawatembezea bakuli kuwaomba hela??? Na rudisheni Euro Mil 27 za watu. Na bado tena. Kuna list ya ICC inakuja ndo mtapoteana kabisaaaa
euro mil 27 za watu?? hivyo ni vijisenti kwa taifa langu la tz na wakitaka tutawaludishiaa wasitutishee
 
Huwezi kusema Tanzania ni taifa huru wakati zaidi ya 90% ya wananchi wake hawapo huru.

Huwezi kusema Tanzania ni taifa huru wakati karibu 40% ya bajeti ya kuendesha nchi inategemea misaada ya wahisani.
 
Huwezi kusema Tanzania ni taifa huru wakati zaidi ya 90% ya wananchi wake hawapo huru.

Huwezi kusema Tanzania ni taifa huru wakati karibu 40% ya bajeti ya kuendesha nchi inategemea misaada ya wahisani.
Sio 40% ya bajeti ndugu. Achana na takwimu za Ccm izo ni almost 60%
 
Nieleze kimaandiko kidogo Ufunuo 17:18 "na yule mwanamke uliyemwona in mji ule mkubwa wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi" Hapa duniani kazima ukubali kabisa Mungu anatoa uwezotofauti wa akili,uchumi na hekma.Kunafalme zenye nguvu kupita Tanzania lazima tujue namna ya kuishi nao ilitusiumize raia wetu,tatizo tunaonesha kiburi wakati hatuna lolote.Viongozi tutumie hekima sana
 
Back
Top Bottom