Umoja wa Mataifa (UN) walaani Utawala wa Mali kufungia vyombo vya habari

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu amekosoa uamuzi wa Mali wa kupiga marufuku vyombo vya habari vya Ufaransa na kuwataka watawala wake wa kijeshi kubadili uamuzi wao.

"Tumesikitishwa sana na uamuzi wa Mdhibiti wa Vyombo vya Habari wa Mali kuifungia Radio France International [RFI] na France24," anasema Kamishna Mkuu wa UN, Michelle Bachelet na kuongeza:

"Hatua hiyo ni mwendelezo wa vitendo vya kuminya uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza Nchini Mali, vinafanyika wakati uhuru ukiwa unahitajika kwa kiwango cha juu."

Viongozi wa kijeshi wa Mali kwa mara ya kwanza walisimamisha kazi vyombo hivyo vya habari Machi 16, 2022 wakishutumu kwa kupeperusha madai ya uwongo kuhusu ripoti za ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanya na Jeshi la Mali.

Jumatano Aprili 27, 2022, Mamlaka ya Juu ya Mawasiliano ilitangaza juu ya maamuzi ya kusimamisha matangazo ya vyombo hivyo.

Vyama vya waandishi wa habari vimeshutumu ongezeko la mashambulizi na kampeni za kupaka matope dhidi ya waandishi wa habari katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, hasa dhidi ya wawakilishi wa vyombo vya habari vya Ufaransa.

Waandishi wa habari wa kigeni na wa ndani wanaoripoti Mali wameshutumu kuzorota kwa wataalamu wa vyombo vya habari nchini humo.


Source: Aljazeera
 
Back
Top Bottom