Umoja wa Afrika (AU) Waridhia kumuunga mkono Dkt. Tulia kuwa mgombea pekee kutoka Afrika nafasi ya Urais wa Jumuiya ya Mabunge Duniani

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Umoja wa Afrika (AU) umeridhia kumuunga mkono Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) kuwa Mgombea pekee kutoka Bara la Afrika wa nafasi ya Urais wa Jumuiya ya
Mabunge Duniani (Inter-Parliamentary Union-IPU).

Uamuzi huo ulifikiwa katika Mkutano wa 43 wa Baraza la Mawaziri la Umoia wa Afrika uliofanyika Jijini Nairobi, Kenya tarehe 13 hadi 14 Julai, 2023 baada ya Baraza hilo kupokea na kuridhia ombi la Seriali ya Tanzania la kumuunga
mkono Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) katika kugombea nafasi hiyo.

Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) tayari ameungwa mkono na Bunge la Afrika (PAP), Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) na Jukwaa la Mabunge ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC PF) katika kugombea nafasi hiyo. Uchaguzi wa Rais wa Jumuiya ya Mabunge Duniani (Inter-Parliamentary Union-IPU) unatarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 chini Angola.

Screenshot 2023-07-19 at 13.40.02.png
 
Hongera Sana Dr.Tulia Ackson, Mungu akujalie Mtanzania Mwenzangu bila kujali itikadi wala tofauti ya Namna yoyote Ile upate Ushindi wa Kishindo na Tanzania izidi kupaa kwenye medani za siasa za kimataifa.

Nakuombea Kwa Mungu jambo hili likawe heri kwako na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ukishinda unikumbuke Mtanzania mwenzako wa kawaida sana huenda ukawa muujiza kwenye maisha yangu pia. Amen
 
Yaani Waafrika utumwa ni jadi na mnastahili kuendelea nao! Huyu kiazi asiye na hata chembe ya demokrasia! Nina wasiwasi hata phd ni ya chupi tu stupid! Kwa jinsi nilivyofuatilia DP word ratification HUYU ni tumbili tu!
 
Watanzania sijui lini tutajitambua, hivi kweli mtu anapata nafasi ya kuwakilisha taifa, halafu tunakuwa mstari wa mbele kutoa kejeli na dharau kwa walioona ana sifa, vigezo na uwezo wa kuwa mgombea wa nafasi tajwa! Hakika mungu ni mkubwa na ndiye atakayeamua nani awe kwenye nafasi hiyo, chuki zenu sana sana zinazidi kumpaisha kimataifa! Hongera Mheshimiwa daktari Tulia Akson!
 
Ila ametuangusha sana pale Bungeni.

Hatuna Imani na Bunge letu kwa sababu yake.
 
Yaani watu wa humu jf, badala ya angalau kunyamaza kama hupendi mafanikio yake, wewe unaleta vitu vya ajabu.

Hizi roho mbaya ndiyo hata Mwenyezi Mungu hakupi baraka wewe unaemuombea mwenzako vibaya.
 
Back
Top Bottom