GE2025 Ummy Mwalimu: Siwezi kususa, naipambania CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu, amehudhuria uzinduzi wa kampeni za kumnadi na kumuombea kura ya ndiyo Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mgombea Ubunge wa CCM katika Jimbo la Tanga, Kassim Amar M’baraka (Makubel), katika mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Majengo, Jijini Tanga.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo, Ummy Mwalimu amesema hana sababu ya kususa baada ya kutopitishwa tena kuwania ubunge, kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemheshimu na kumpa nafasi za juu katika uongozi kwa muda mrefu.

Soma pia

Ameeleza kuwa amehudumu kama Mbunge kwa miaka 15 na pia ameshika nyadhifa mbalimbali za Uwaziri kwa kipindi cha miaka 14, hivyo hana sababu ya kuwa na hasira au kukasirika, kwani kufanya hivyo ni sawa na kumkosea Mungu

“Siwezi kususa, nimsusie nani? CCM imeniheshimu sana mimi mtoto wa Kidogo. Nimehudumu kama Mbunge kwa miaka 15 na nimepewa dhamana ya kuwa Waziri kwa miaka 14. Nikikasirika, nitakuwa namkosea Mungu,” amesema Ummy Mwalimu kwa msisitizo.

Aidha, alisifu uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, akisema umetekeleza mambo makubwa na ya kihistoria yanayostahili kuendelezwa kwa maslahi ya Taifa.

Mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Jiji la Tanga waliokusanyika kusikiliza sera na mikakati ya wagombea wa CCM kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
View attachment 3467336
Source: Clouds
Odo wewe wa kumsema boss wako kuwa anapiga ugimbi hadi anazima? Kweli domo ponza kichwa, ila umesaidia umma kujua wanaongozwa na kichwa cha namna gani.
 
Wivu sina ila roho inauma
Sasa jiulize roho inauma vip wakati huna wivu
 
Teuzi pendwa anazohangaikia Lucas msandambwa mpaka visigino vimeisha bado zipo, acha abahatishe
 
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu, amehudhuria uzinduzi wa kampeni za kumnadi na kumuombea kura ya ndiyo Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mgombea Ubunge wa CCM katika Jimbo la Tanga, Kassim Amar M’baraka (Makubel), katika mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Majengo, Jijini Tanga.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo, Ummy Mwalimu amesema hana sababu ya kususa baada ya kutopitishwa tena kuwania ubunge, kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemheshimu na kumpa nafasi za juu katika uongozi kwa muda mrefu.

Soma pia

Ameeleza kuwa amehudumu kama Mbunge kwa miaka 15 na pia ameshika nyadhifa mbalimbali za Uwaziri kwa kipindi cha miaka 14, hivyo hana sababu ya kuwa na hasira au kukasirika, kwani kufanya hivyo ni sawa na kumkosea Mungu

“Siwezi kususa, nimsusie nani? CCM imeniheshimu sana mimi mtoto wa Kidogo. Nimehudumu kama Mbunge kwa miaka 15 na nimepewa dhamana ya kuwa Waziri kwa miaka 14. Nikikasirika, nitakuwa namkosea Mungu,” amesema Ummy Mwalimu kwa msisitizo.

Aidha, alisifu uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, akisema umetekeleza mambo makubwa na ya kihistoria yanayostahili kuendelezwa kwa maslahi ya Taifa.

Mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Jiji la Tanga waliokusanyika kusikiliza sera na mikakati ya wagombea wa CCM kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
View attachment 3467336
Source: Clouds

Bddo ana matumaini ya kurudishwa huko mbeleni kipitia milango ya nyuma.

Ila siku hizi wakikutema ni ngumu sana kurudi unless mtandao wako umefanikiwa. Apitie kwa Adul kumuomba Maza msamaha maana inaelekea ana kinyongo naye kikubwa. Sijui alifanya nini....!?
 
Hawa walioanguka ubunge wana altenative ya kutunukiwa madaraka tena na maisha yao ya kisiasa yakaendelea kama kawaida, ndio maana wanakipepelea chama chao, wanakiona ni mgodi wa ajira zao
 
Ila jinsi alivyokua anaongea, ni km vile kalazimishwa, au laah kujikosha tyuuh.

Hayuko sawa kabisaa, Lol 😂😂😂😂😂😂
 
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Tanga mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Ummy Mwalimu amesema katu hawezi kususa eti kwa sababu hakuteuliwa na chama hicho kupeperusha bendera katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu (2025) licha ya kuwa aliongoza kwenye mchakato wa awali wa kura za maoni, badala yake amesema atasimama kidete kuhakikisha chama chake kinapata ushindi wa kishindo kwa nafasi zote jimboni humo

"Nawaomba sana ndugu zangu, tarehe 29 tunakwenda kufanya maamuzi makubwa kuhusu amani ya Tanzania, maendeleo ya Tanzania, amani ya Tanga, maendeleo ya Tanga na ustawi wa watu wa Tanga, tusifanye makosa kura zote za ndio kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan" -Ummy

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Tanga mjini kupitia CCM Kassim Makubeli, Ummy amesema kwa nyakati tofauti amebahatika kufanya kazi chini ya Marais watatu tofauti wa Tanzania hata hivyo amemtaja Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa kiongozi wa kipekee kwani anajali na kuumizwa na changamoto zinazowakabili Watanzania

Soma pia: Ummy Mwalimu adondokea pua jimbo la Tanga Mjini, nafasi yake yachukuliwa Kassim Baraka

Back
Top Bottom