gemmanuel265
JF-Expert Member
- Feb 16, 2016
- 8,485
- 18,053
Duuuh naona Waziri kakumbana na hasira ya umma !
We...Tumaini..sasa umeandika nini?Waziri Ummi alipo simama nakutaka baruwa toka kwa familia ilikuwa ni msg nzuri kuwafumbua macho wanachama na wapenzi wa chadema kile chama chao wanakifanya nakuwa tahadharisha wasitoe michango isio kuwa na muhasibu wala muhadhini.
Kiufupi kufa kufaana kitu kimefanyika na mpaka serikali imeingilia kati ni kundi la wajanja ndani ya chadema ndani na nje kujipatia mtonyo kwa njia iso sawa upo msemo unasema mali bila daftari hupotea. Msemo huu unaendana sana na akaunti nyingi kwenye mablog ndani na nje kujifanya watu wachangie Lisu. Jambo lakutisha pesa hazifiki hata 300m mpaka sasa wakati watu wamejitoa. Jambo lingine hakuna udhibiti wakuchangia kila mtu kawa mchangishaji jambo serikali imewatahadharisha sana watanzania kwa nia njema wawe makini na matapeli ambao kwao shida za wengine ni fursa ya mtaji kwao..
Swala la msingi kwa wananchi na wanachama kujiuliza whyhawa jamaa wanatembeza bakuli kwenye taasisi nje ya nchi nakuichafuwa serikali nini kimejificha.
Je nikweli kuna uwazi wa kile kinafanyiwa na pesa yao?
Ummi mwalimu ameutahadharisha umma nakwahakika tusipo jiongeza wanachama basi tusije laumu.
Tuwaambie chadema wafuwate utaratibu Lisu apate haki yake otherwise mtafika mahali mlaumiane amini usiamni Ruzuku ikiingia mtaambiwa imeenda mtibu Lisu na huyo lisu akijuwa ukweli atalia nakujuwa kweli kufa kufaana na uwenda vile wanaiwazia serikali ni uongo at that time itakuwa muda hakuna.
Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas amefunguka na kusema kuwa hakuna masharti yoyote serikali imeweka ili Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu apatiwe matibabu na kusema wanasubiri maombi ili waweze kugharamia matibabu ya Lissu.
![]()
Msemaji wa serikali amesema hayo jana kupitia mtandao wake wa twitter siku moja baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kusema kuwa alipata taarifa kutoka kwa wasaidizi wa Spika wa Bunge kuwa wapo tayari kugharamia matibabu ya Tundu Lissu kwa masharti ya kuwa mgonjwa lazima apelekwe India, wapate barua ya maombi na kupata ripoti ya madaktari jambo ambalo Mbowe anasema alilikataa na kusema hawezi kufanya hivyo.
Kufuatia kuwepo kwa taarifa hizo ndipo Msemaji wa Serikali ameibuka na kusema kuwa hakuna masharti yoyote ambayo wameyaweka na kusema serikali ipo tayari kugharamia matibabu ya Tundu Lissu na kuwa wao wanasubiri barua kujua gharama za matibabu.
"Hakuna sharti lolote, tunasisitiza tena na bado tunasubiri, leteni barua rasmi tujue gharama na itifaki nyingine za tiba. Tutagharamia" alisema Dkt. Abbas
Aidha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu aliendelea pia kufafanua jambo hilo kuwa Mbunge Tundu Lissu aliondolewa kwenye utaratibu wa serikali alipopelekwa nchini Kenya hivyo anadai ili serikali iweze kuingia katika gharama za kulipia matibabu lazima wapate ridhaa ya familia.
"Mgonjwa alitolewa kwenye utaratibu wa Serikali alipopelekwa NRB. Sasa gharama/tiba zaid yahitajika. Serikali inaingiaje bila ridhaa ya familia? Mgonjwa ni Mbunge, anahitaji matibabu zaidi. Lakini kwa kuwa sasa yupo nje ya utaratibu wa Serikali, Serikali kushiriki ni lazima yawepo maombi" alisisitiza Ummy Mwalimu
Familia imesha sema haita omba. Nadhani serikali waache kuendela kutoa matamkoHebu muacheni huyo Baba wa watu angalau augulie majeraha yake ili apone ni muhimu kwake na Familia yake!