Umiliki wa mali baada ya ndoa: Naomba kuelewa hii sheria. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umiliki wa mali baada ya ndoa: Naomba kuelewa hii sheria.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Pretty, Apr 24, 2009.

 1. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Kama msichana umeolewa na mwanaume ambaye tayari umemkuta na vitu vyake, I mean may be umemkuta na mali kama Nyumba, magari na vitu kama hivyo, na kila kitu kipo kwenye jina lake. je kwa kisheria hivyo vitu vitahesabika vya wote kama mmeoana? Au kuna uwezekano wa yy kubadili jina hati zote na kuandika jina lake na mkewe?
  Nahitaji kujua kama hii sheria ipo.
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ...Nilipigana vikumbo juzi na Invisible kwenye korido za sheria ameshika makabrasha kibao. Naamini atakuja hapa na vipengele kadhaa ktk kukusaidia kupata jibu

  Ila kiufupi ni kwamba hapo huna chako labda aamue kukujumuisha kwa hiari yake. ila since day one mnapaswa pia kukubaliana kipi cha nani na kipi si cha nani. Pia SI lazima kwa kuhamisha umiliki wa mali ulizokuta kwa mumeo/mkeo. Bali kumbuka kama ni mali zenu wote basi majina yote yatokee ktk hati za umiliki au la utashangaa jamaa au mama anakopa mahala bila kumjulisha mwenza halafu antumia mali yenu ya umma kisha mwishowe mnapoteza yote kwa uzembe wa....
  Zingatia kwenye mirathi lazma zile mali zenu nyote mlizomiliki pamoja mnatolea maamuzi yanayowiana baada ya mmoja kutangulia ili kupunguza kesi za mashemeji na ndugu wa kiumeni kukamia mali endapo baba atagoshora mapema.

  Nahisi Pretty unataka kuhamisha umiliki wa mali za yule mshikaji aliye keko mgawa RAV4 nyekundu ili akitoka ajikute segerea ya uraiani haha(joke)
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  sheria ipo na angalia sheria ya ndoa na sheria ya mikataba inaonesha hayo....
   
 4. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Ahsante Msanii kwa ufafanuzi wako.
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nitajaribu kukujibu kwa kifupi kama ifuatavyo:
  Sheria ya Ndoa ya 1971( LMA/Act no.5/1971) inaweka utaratibu wa kuwa na mali baina ya wanandoa kama ifuatavyo:- mali ya pamoja kwa maana wote wamechangia kuipata na wana haki nayo.Vilevile inaruhusu wanandoa kuwa na mali binafsi - kwa maana mtu anaweza kuwa na mali aliyoipata kabla, au aliyorithishwa n.k. in short siyo joint property.Uthibitisho wa mali ni pamoja na hati yenye jina la mhusika.KUOANA HAKUBADILI AUTOMATICALLY HIZO MALI NA KUZIFANYA JOINT UNLESS MUWE NA MAKUBALIANO YA HIVYO.Huu ndiyo msimamo wa kisheria.
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kwa kuongezea, labda kama umeongezea thamani katika mali husika basi utakuwa na haki kwa kiwango kile cha mchango wako.Uamuzi wa uwiano wa haki katika mali hiyo utaamuliwa na mahakama pale kutakapokuwa na shauri kwa misingi labda unadai talaka na mgawanyo wa mali.Na wewe unayedai utatakiwa uthibitishe mchango wako katika mali hiyo unayodai on a balance of probability.
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  1. Hivi mkifunga ndoa: baada ya wiki 2 ikavunjika na mmali yote ni ya baba na mke amekuwa tu mama wa nyumbani, je hapo ina maana mke hatapewa chochote kisheria?

  2. Watoto/Mke wa nyumba ndogo je atakuwa na sauti gani gatika mali ya familia?
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  1.kwanza kisheria hamwezi kuvunja ndoa kwa talaka ya kimahakama kama hamjakaa miaka miwili minimum.( Unless kuwe na sababu kubwa sana kama non-consumation of marriage na hii itafanya hiyo ndoa iwe batili tangia mwanzo.Kwa msingi huo hakuna cha kugawana mali.. labda mgawane zile zawadi mlizopewa wakati wa harusi ( tena za send-off zinaweza kuwa za bibi harusi mwenyewe..bwana harusi hazimhusu).
  2.Nyumba ndogo kisheria siyo mke bali ni paramour ( hawara/mwizi tu) na anaweza kushtakiwa na kutakiwa kulipa fidia kwa mke wa ndoa! hivyo hana chake.
  3. Watoto wa nje ya ndoa - kila mtoto ana haki kutunzwa na wazazi wake wote wawili.Ila kwa vile mtoto huyo kazaliwa nje ya ndoa, basi ni juu ya mama mtoto kudai matunzo hayo mahakamani.Atalazimika kuthibitisha kuwa huyo ndo baba( putative father) miaka ya nyuma hili lilikuwa gumu kidogo, ila sasa kuna vipimo vya DNA.Ikishathibitika kuwa huyo ni baba, mahakama itaamuru kiwango atakachotoa baba, kwa mkupuo au kwa mwezi kama utashi na busara za mahakama zitakavyoelezeka.Sheria ya Affiliation ilikuwa imeweka kiwango kidogo sana lakini mahakama inaweza kuweka kiwango reasonable kuendana na kipato cha baba mhusika.
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  WOS
  nakuja kusoma sheria kwako
  ila nina vijiasignment fulni naomba unisaidie maana nipo majalala hapa sana tu. je upo tayari kunsaidia?
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Anytime Msanii.Uskonde wala nini..just shoot!
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  please can you measure
  Cicero's advise vis-a-vis provisions of the LAND ACT on DISPOSITIONS

  unayo introduction
  of the philosophical conception of 'DUTY' or 'OBLIGATION' and why the
  moral obligation to DUTY overrides EXPEDIENCE [Utility] yake?
  kama huna niputumie kwenye PM
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  You can PM
   
 13. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #13
  Apr 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,233
  Likes Received: 5,619
  Trophy Points: 280
  Hivi mkifunga ndoa: baada ya wiki 2 ikavunjika na mmali yote ni ya baba na mke amekuwa tu mama wa nyumbani, je hapo ina maana mke hatapewa chochote kisheria?

  2. Watoto/Mke wa nyumba ndogo je atakuwa na sauti gani gatika mali ya familia?
  __________________
  WE MZALENDO HALISI UANHIMIZA UZINZi HEEE????NDOA YA WIKI MBILI MTOTO WAMPATIE WAPI UNLESS WALIZAA KABLA YA HARUSI NA KA HIVYO HAWAKUOANA HAO WALIBARIKI NDOA ...KWA UPANDE WA NDUGU ZETU WAKRISTO....
   
 14. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Ahsante WoS kwa maelezo yako ya kisheria.
   
 15. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu WomenofSubstanc,

  Nadhani sheria inasema unaweza kudai talaka mahakama ndani ya miaka miwili ya ndoa kama utaona ndoa inakupa "shida za kipekee." Sio lazima ihusiane na "sababu kubwa sana kama non-consummation."

  Mwanamke akiona, kwa mfano, anatwangwa makonde toka siku ya kwanza, au analetewa udhia wa vimada humo ndani kiasi cha kuleta ugumu usio kifani katika ndoa basi nadhani anaweza akadai kumuacha huyo mume ndani ya miaka miwili. Na ataweza kuondoka na thamani yake ya mali walizochuma pamoja katika hiyo ndoa yao.

  Nadhani ni muhimu kwa wanawake kujua kwamba sio lazima wakae kwenye ndoa ambayo haiwezekaniki eti kwa vile wanasubiri miaka ya kuchukua hatua ifike. Wanaweza kuchelewa, wakadhuriwa jumla jumla.
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  May 2, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ndio uzuri wa kuwa katika forum kama hii. Tafadhali mwenye copy ya sheria ya ndoa atuwekee hapa tuisome wote na kuichambua!
   
Loading...