Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,889
- Thread starter
- #41
TIBA YA TANO - Fanya makazi yako kuwa uwekezaji wenye faida.
"Iwapo mtu anatumia tisa ya kumi ya pato lake kwa mahitaji ya msingi na kufurahia maisha, na iwapo sehemu ya hii fedha anaweza kufanya uwekezaji wenye kuleta faida bila kuathiri maisha yake, hazina yake itakuwa kwa kasi sana." Hivyo ndivyo alivyoanza kuongea Arkad kwenye siku ya tano.
"Watu wengi hapa Babiloni hutunza familia zao kwenye nyumba za mbavu za mbwa na zilizo sehemu mbaya kabisa. Nyumba zisizofaa watu kuishi. Huko wanawalipa wenye nyumba kodi kubwa kwa nyumba ambazo hata nafasi ya kupanda maua ya kufurahisha moyo hakuna. Watoto wao hawana hata sehemu ya kucheza bali hucheza kwenye vichochoro vichafu.
"Hakuna familia inayoweza kufurahia maisha bila ya watoto kuwa na sehemu safi ya kucheza na eneo ambalo mke anaweza kupanda si tu maua bali pia mbogamboga kwa ajili ya familia yake.
"Inafurahisha mtu kula matunda kutoka kwenye mti wake na zabibu za bustani yake. Kumiliki makazi yake na kujivunia sehemu yake. Hilo litamfanya ajiamini na aweze kutimiza malengo yake mengine kwa moyo mmoja.
"Hivyo, napendekeza kila mtu amiliki nyumba kwaajili yake na familia yake.
"Kumiliki nyumba si jambo lisilowezekana kwa wale walio na nia. Je mfalme wetu hajatanua kuta za Babeli ili kuwe na eneo kubwa na sasa mtu anaweza kununua kiwanja kwa bei nafuu?
"Pia niwaeleze kitu kingine, wakopesha pesa hutafuta watu wanaokopa kwaajili ya kununua ardhi na ujenzi wa nyumba. Watakukopesha haraka ili umlipe mfyatua tofali na mjenzi, utahitaji tu kuonyesha kiasi kidogo ulichotenga kwaajili ya kazi hiyo.
"Ukishajenga nyumba unaweza kumlipa mkopeshaji kama ulivyokuwa unamlipa mwenye nyumba. Kila unaporejesha unakuwa unapunguza deni na baada ya miaka michache unakuwa umemaliza.
"Hapo utafurahi kuwa na nyumba yako mwenyewe na hutadaiwa na mtu zaidi ya kodi ya mfalme tu.
"Pia mkeo akienda mtoni kufua anaweza kurudi na maji ya kumwagilia bustani. Baraka nyingi huja kwa mtu anayemiliki nyumba yake mwenyewe. Pia hili hupunguza sana gharama za maisha. Pesa nyingi hubaki kwaajili ya kustarehe na kutimiza matamanio mengine. Hii ndiyo tiba ya tano ya pochi iliyo tupu.
Miliki nyumba yako mwenyewe.
TIBA YA SITA - Hakikisha wakati ujao utakuwa na kipato.
"Maisha ya kila mmoja huanzia utotoni hadi uzeeni. Hii ni njia ya maisha na mtu hawezi kuiepa isipokuwa miungu imemuita mapema. Hivyo ninasema kuwa ni muhimu kwa mtu kufanya maandalizi ili wakati ujao awe na kipato. Kipindi ambacho hatakuwa kijana tena. Pia anatakiwa kuweka maandalizi kwaajili ya familia yake ili isihangaike ikitokea Miungu imemuita mapema. Kwa hiyo nasema kuwa ni jambo la muhimu kwa mtu kufanya maandalizi ili aje kuwa na kipato uzeeni, nyakati ambazo hatakuwa kijana tena. Na pia kufanya maandalizi kwaajili ya familia yake iwapo atafariki. Somo hili linafundisha kuhakikisha pochi yako imetuna hata wakati ambapo huwezi kufanya kazi ya kuingiza kipato.
Hivyo ndivyo alivyoanza kusema Arkad katika siku ya sita.
"Mtu ambaye anajua kanuni za utajiri na akaweza kujipatia utajiri ni muhimu akafikiria kuhusu wakati ujao. Anatakiwa kuwekeza kwenye miradi ambayo ni salama na inadumu kwa miaka mingi. Laki mapato kutokana na miradi hiyo yanatakiwa kupatikana kirahisi mara yatakapohitajika.
"Kuna njia nyingi ambazo mtu anaweza kuhakikisha kuwa wakati ujao atakuwa salama. Anaweza kuwa na sehemu ya siri na kufukia hazina yake hapo. Lakini hata afiche namna gani lazima siku moja wezi wataipata. Kwa hiyo sishauri kufanya hivyo.
"Mtu anaweza kununua nyumba au ardhi kwaajili ya wakati ujao. Kama amechaguwa vizuri na kuna uwezekano wa kupanda thamani huko mbeleni, hivi ni vitu vyenye thamani ya kudumu. Mapato yake au mapato kutokana na kuviuza yanaweza kufaa kwa ajili ya wakati ujao.
"Pia anaweza kukopesha pesa zake huku akiziongeza mara kwa mara. Riba inayoongezwa kwenye pesa hiyo itafanya pesa yake ikue haraka sana. Minamfahamu mtengenezaji wa makubazi mmoja anayeitwa Ansam. Ansam aliniambia kuwa kila wiki huweka vipande viwili vya fedha kwa mkopesha pesa. Amekuwa anafanya hivyo kwa muda wa miaka minne sasa. Hivi karibuni ameenda kuona akiba yake na imemfurahisha sana. Pesa yake, ukichanganya na riba ya moja ya nne kwa kila miaka minne imefikia jumla ya vipande elfu moja na arobaini vya fedha.
"Kwa ujuzi wangu wa masuala ya fedha nilimhamasisha kuendelea kuweka kwa kumuonyesha kuwa; akiendelea hivyo kwa miaka kumi na miwili mingine atakuwa anamdai mkopesha pesa vipande elfu nne vya fedha. Kiasi kitakachomtosha maisha yake yote.
"Kiasi kidogo hivyo kikiwekezwa kwa ukawaida huwa kikubwa sana. Hakuna mtu ambaye hawezi kuweka akiba kwaajili ya uzee wake na kwaajili ya wakati ujao wa familia yake. Hilo halijalishi biashara yake ni kubwa kiasi gani au ana miradi gani.
Nategemea siku moja watu wenye akili watabuni bima ya kifo. Watu wengi eaweke pesa kidogokidogo na kisha mmoja wao anapokufa basi familia yake wapewe kiasi fulani. Hili naona kama litakuwa jambo zuri na napendekeza lifanyike. Lakini hili kwa sasa ni gumu kufanyika kwa sababu ni jambo linalofanyika baada ya ya maisha ya mtu au ushirika wowote wa kibiashara. Ila ili ufanye kazi unatakiwa kuwa imara kama kiti cha ufalme.
Lakini siku moja nafikiri hilo litawezekana na kuleta baraka kwa watu wengi. Hata pesa ndogo iliyowekezwa itafanya familia ya marehemu kulipwa pesa za kutosha.
Lakini kwa sababu tunaishi katika siku hizi, basi tunatakiwa kutumia njia zilizopo. Kwa hiyo basi nashauri watu wote kutumia njia zilizothibitika kuwa ni bora ili kujiandaa kwa ajili ya miaka ya uzeeni. Mtu asiye na kitu na hawezi kufanya kazi au familia iliyoondokewa na kichwa cha familia na kuachwa bila kitu ni janga kubwa sana.
Hii ndiyo tiba ya sita, hakikisha una kipato kwajili ya uzee wako, na kwaajili ya ulinzi wa familia yako.