Umewahi kusoma kitabu, The Richest Man In Babylon? Ulijifunza nini? Kinasaidia?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,575
2,000
1618749998815.png

Muandishi: George S. Clason's, 1926.
Mtafsiri: Pictuss.

Email: pictuspublishers@gmail.com.

©Pictuss2021.

Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu yoyote ya tafsiri hii inayoweza kunakiliwa, kutolewa kivuli(photocopy), kuhamishwa, kurekodiwa au kutolewa kwa namna yeyote bila ya taarifa ya awali ya kimaandishi ya mtafsiri.

UTANGULIZI

YALIYOMO

Mtu aliyetamani dhahabu
Tajiri wa Babiloni
Tiba saba za pochi tupu
Kutana na Mungu wa bahati
Sheria tano za pesa
Mkopesha pesa wa Babiloni
Kuta za Babiloni
Mfanyabiashara ya ngamia wa Babiloni
Mabamba ya vigae
Mtu mwenye bahati zaidi katika Babiloni

Sasa unaweza kukisoma kitabu hiki bure ndani ya maktaba app(by pictuss). Install toka playstore.

MTU ALIYETAMANI DHAHABU
Bansir alikuwa ni mtengenezaji wa magari ya kukokotwa na farasi huko Babiloni. Alikuwa ni mtu ambaye hakuridhika na hali ya maisha yake. Siku hii alikuwa amekaa juu ya ukuta mfupi unaozunguka nyumba yake. Aliangalia kwa huzuni kajumba kake na eneo analofanyia kazi ambapo kulikuwa na gari la farasi ambalo halijaisha kutengenezwa.

Mara kwa mara mke wake alionekana mlangoni. Kwa jinsi alivyokuwa akimuangalia ilimkumbusha kuwa unga ulikuwa unakaribia kuisha hivyo anatakiwa kufanya kazi gari lile liishe. Agongelee, akate, apige msasa, apige rangi aweke matairi na kupamba kisha alipeleke kwa mteja wake ili apate pesa.

Hata hivyo mwili wake mnene na uliojengeka uliendelea kukaa kizembe juu ya ukuta. Akili yake nzito ilikuwa inahangaika kutatua tatizo ambalo hakuweza kupata jibu lake.

Joto na jua kali la kwenye bonde la mto Efrati lilikuwa likimpiga bila huruma. Matone ya jasho kama shanga yalimtoka kwenye paji la uso. Yalimtiririka mpaka kwenye kifua chake chenye vinyweleo vingi bila yeye mwenyewe kujua wala kutilia maanani.

Mbali na nyumba yake kulikuwa na jumba kubwa la mfalme lililokuwa limezungukwa na ukuta. Pembeni yake kulikuwa na jengo refu lililopakwa rangi, hekalu la Bel(bwana, Marduki). Katikati ya majengo makubwa na ya kifahari namna hiyo, kulikuwa na kajumba kake na tujumba tungine tuchafu zaidi.

Babiloni ulikuwa ni mji wa namna hiyo, mchanganyiko wa ufahari na uchafu. Utajiri mkubwa na umaskini wa kutupwa. Vilichanganyika na kujazana pamoja bila mpango ndani ya ukuta wa jiji.

Nyuma yake, japo hakuangalia kulikuwa na kelele za magari ya kukokotwa na farasi ya watu matajiri yakipita sambamba na wafanyabiashara waliovaa makubazi na ombaomba waliokuwa peku.

Matajiri walilazimika kupaki pembeni kupisha msafara mrefu wa watumwa waliobeba maji kwaajili ya kazi za mfalme. Kila mmoja wao alibeba mfuko mzito wa maji uliokuwa umetengenezwa kwa ngozi ya mbuzi. Walikuwa wanayapeleka kwenye bustani zinazoelea za Babiloni.

Bansir alikuwa amezama kwenye mawazo kuhusu shida zake wala hakukazia akili vurugu za mji. Alishtushwa na mlio wa kinubi ambao haukuwa mgeni kwake. Aligeuka na kukutana na uso unaotabasamu wa rafiki yake kipenzi, Kobbi, mwanamuziki.

"Baraka za Miungu ziwe nawe rafiki yangu" alisalimia Kobbi

"Inaonekana Miungu ni wema sana kwako hadi huna haja ya kufanya kazi! Nafurahia bahati yako maana na mimi naweza kufaidika nayo. Bila shaka mifuko yako imetuna, vinginevyo ungekuwa unapiga kazi saa hizi. Nikopeshe shekeli mbili, nitakulipa jioni baada ya karamu ya matajiri"

"Yaani ningekuwa na shekeli mbili nisingekukopesha" akajibu Bansir kwa unyonge. "Nisingekopesha mtu yeyote, hata wewe nisingekukopesha. Hizo ndizo zingekuwa kila kitu kwangu na mtu hawezi kukopesha kila kitu alichonacho, hata kwa rafiki yake kipenzi"
"Unasema!" Akashangaa Kobbi. "Inamaana hauna hata shekeli moja mfukoni lakini umekaa juu ya ukuta kama sanamu. Kwanini usimalizie hilo gari? Sasa utapataje mahitaji yako? Siyo kwa mtindo huo rafiki yangu. Nguvu zako za siku zote ziko wapi? Kuna kitu kimekukwaza, Miungu imekuletea matatizo?"

"Itakuwa ni mateso toka kwa Miungu" alikubali Bansir. "Ilianza kama ndoto, ndoto isiyo na maana. Ndani ya ndoto nilikuwa ni mtu wa maana. Kwenye mkanda wangu wa kiunoni ilining'inia pochi nzuri iliyojaa pesa. Kulikuwa na pesa nyingi kiasi kwamba ningeweza kugawia ombaomba bila kujali kuishiwa; nilikuwa na dhahabu zilizonifanya nijihisi salama hata kwa siku za usoni na wala sikuogopa kutumia pesa. Nilikuwa ni mtu niliyeridhika sana. Usingenijua kama ni mtu mwenye bidii ya kazi wala mke wangu usingemtambua. Uso wake haukuwa na makunyanzi na uling'ara kwa furaha, alikuwa mwanamwali tena, kama alivyokuwa mwanzo nilipomuoa."

"Ndoto tamu kweli" akasema Kobbi. "Lakini kwanini ndoto tamu hivyo ikufanye ukae juu ya ukuta kama sanamu?"

"Hilo ndilo swali! Nilipoamka na kukumbuka jinsi mifuko yangu ilivyo mitupu, hisia za uasi na kutojali zikaniingia. Ngoja tuongelee hilo suala pamoja. Kama mabaharia wasemavyo, mimi na wewe tupo ndani ya mtumbwi mmoja. Wakati tukiwa wavulana tulijifunza pamoja kwa kuhani. Tulipokuwa vijana tulifurahia maisha pamoja. Na katika utu uzima tumekuwa marafiki wa karibu.

Tumekuwa watu wa kuridhika. Tumeridhika kufanya kazi kwa masaa mengi na tunatumia mapato yetu kwa uhuru. Tumepata pesa nyingi kwa miaka yote tuliyofanya kazi lakini furaha ya utajiri tunaipata ndotoni tu. Bah! Tunatofauti gani na kondoo wasioelewa kitu? Tunaishi kwenye mji tajiri zaidi duniani. Wasafiri wanasema hakuna mji unaofanana nao kwa utajiri lakini sisi hatuna kitu. Baada ya kufanya kazi ngumu kwa nusu ya maisha yangu, mimi, wewe na rafiki zetu wengine, hatuna kitu,'

"Naweza kuazima shekeli mbili na nitakulipa jioni? Nilijibuje? Nilisema kuwa hii hapa? Hapana, nilikubali kuwa mifuko yangu haina kitu kama yako tu."

"Shida yetu nini? Kwanini hatuwezi kuwa na fedha na dhahabu zaidi ya zinazotosha nguo na chakula tu?"

"Fikiria kuhusu wana wetu" aliendelea Bansir. "Je, hawafuati hatua zetu? Si kwamba wao, familia zao, na familia za watoto wao wataishi katikati ya dhahabu na utajiri kama sisi lakini wataridhika na kunywa maziwa mgando ya mbuzi na uji tu?"
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,575
2,000
"Katika maisha yote ya urafiki wetu sijawahi ona ukiongea kama hivi Bansir" alishangaa Kobbi.
"Miaka yote hiyo sijawahi pata mawazo kama haya". Akajibu Bansir "Toka asubuhi hadi giza linapoingia nimekuwa nikitengeneza magari bora sana. Nilitegemea siku moja Miungu itaona kazi yangu nzuri na kunitunuku mafanikio.

Hawajawahi fanya hivyo na mwishowe nimegundua hawatakuja kufanya hivyo. Natamani kumiliki ardhi na ng'ombe. Kuwa na nguo nzuri na pesa mfukoni.

Niko tayari kufanya kazi kwa nguvu na akili zangu zote ili kupata vitu hivyo. Natamani kazi yangu inilipe ninavyostahili. Kwani tuna mkosi gani? Nikuulize tena! Kwanini hatuna vitu vizuri?"

"Unafikiri najua jibu?" Alijibu Kobbi. "Mimi ni kama wewe tu. Mapato kutokana na kinubi changu yanaisha haraka sana. Muda wote inanibidi niumize akili ili familia yangu isijepatwa na njaa. Pia moyoni mwangu natamani kupata kinubi kikubwa zaidi ili niweze kupiga muziki hasa. Kinubi kama hicho kinaweza kutoa muziki bora ambao hata mfalme hajawahi kuusikia. Na si mfalme tu, hata Miungu watashangazwa na muziki wake mzuri.

"Lakini nawezaje kupata kinubi bora ikiwa sote ni maskini kama watumwa wa mfalme tu? "Sikiliza kengele! Hao wanakuja," akaonyesha kwenye msafara mrefu wa watumwa waliotoka mtoni. Waliokuwa wamebeba maji huku wakiwa nusu uchi, jasho huku wakitembea kwa taabu kutoka mtoni. Walitembea watano watano huku wamebeba mifuko mizito ya ngozi ya mbuzi ikiwa imejaa maji."

"Anayewaongoza ana afya nzuri" akasema Kobbi huku akionyeshea kwa mtu aliyevaa kengele akiongoza mbele ya msafara aliyekuwa hana mzigo wowote. "Bila shaka ni mtu wa maana huko kwao, si unamuona?!" Akaendelea Kobbi.

"Watu wengi tu kwenye huo msafara wamejengeka vizuri" alisema Bansir. "Wako kama sisi tu. Warefu, weupe kutoka kaskazini, weusi kutoka kusini na wa kahawia kutoka nchi za jirani. Wote wanatembea kutoka mtoni hadi bustanini, kwenda na kurudi. Hawategemei furaha yoyote. Usiku kitanda cha nyasi kinawasubiri na chakula chao ni makande. Waonee huruma Kobbi!"

"Unawahurumia lakini mimi sioni tofauti yao na yetu japo tunajiita watu huru," akasema Kobbi.

"Hilo ni kweli Kobbi, ukweli mchungu. Hatujapenda kuishi kama watumwa miaka na miaka. Kufanya kazi kwa bidii bila kufika popote"akasema Bansir kwa unyonge. "Unaonaje na sisi tujue jinsi wenzetu wanavyopata mafanikio? Unaonaje na sisi tuwaige?" Akauliza Kobbi.

"Pengine kuna siri tunaweza kujifunza tukiuliza wale waliofanikiwa," akajibu Bansir kwa matumani.

"Huwezi amini, leo hii hii nimekutana na rafiki yetu wa zamani Arkad" akasema Kobbi. Alikuwa amepanda gari lake la dhahabu. Nilipomuona nikajisemea moyoni, hawezi kuniangalia mtu wa chini hivi, hana tofauti na matajiri wengine. Nikashangaa ananipungia mkono. Watu wote waliona tajiri mkubwa akimsalimia Kobbi mpiga kinubi kwa uchangamfu"
"Inasemekana ndiye tajiri kuliko wote hapa Babiloni" akasema Bansir kwa kustaajabu.

"Ni tajiri hadi inasemekana mfalme huomba msaada wa kifedha kwake" akasema Kobbi. "Tajiri sana" Bansir akamkatiza" ninaogopa siku nikikutana naye kwenye giza naweza kumpora".

"Acha ujinga" akamzodoa Kobbi. "Mtu hatembei na utajiri wake mfukoni. Mifuko huwa mitupu iwapo hakuna namna ya kuijaza tena. Arkad ana kipato ambacho kinafanya mifuko yake itune muda wote, haijalishi ana matumizi ya kiasi gani."

"Kipato, hicho ndiyo muhimu" akasema Bansir kwa furaha. "Natamani kuwa na kipato ambacho kitakuwa kinaingia hata nikisafiri nchi za mbali au nikikaa juu ukutani kama sanamu. Arkad atakuwa anajua jinsi ya kuwa tajiri. Unafikiri anaweza kunielewesha mtu mwenye akili nzito kama mimi?"

"Nafikiri inawezekana, mbona aliweza kumfundisha mtoto wake Nomasir" akajibu Kobbi "nilisika watu wakisema kuwa kijana wake alienda Ninawi, na bila msaada wa baba yake, amekuwa mmoja wa watu matajiri huko Ninawi"

"Kobbi umenipa wazo" akasema Bansir akasema Bansir huku macho yake yaking'aa kama mtu aliyegundua jambo. "Haitupunguzii kitu kupata ushauri kwa rafiki, na Arkad ni rafiki mzuri. Tusijali kuwa mifuko yetu ni mitupu kama kiota cha mwaka jana cha kipanga.

Twende tusiogope. Tumechoka kuwa maskini katikati ya utajiri mwingi. Kama tumedhamiria kuwa watu wa maana na twende kwa Arkad tumuulize cha kufanya ili na sisi tuwe na kipato cha kueleweka."
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,575
2,000
"Umeongea kweli tupu Bansir. Umenifungua akili. Umenifanya nielewe kuwa, sababu ya kutokuwa na utajiri ni sababu hatujautafuta. Umefanya kazi kwa bidii kutengeneza magari bora, kwa hilo umefanikiwa. Mimi nimefanya bidii kuwa mpiga kinubi hodari na nimefanikiwa katika hili. Kwa kila jambo tulilotia bidii na kutumia akili zetu zote tulifanikiwa. Miungu ilitubariki.

Sasa tumeona mwanga, kama mwanga wa jua linalochomoza. Inatubidi kujifunza zaidi ili kufanikiwa zaidi. Tukiwa na maarifa tunaweza kupata njia bora za kutimiza matamanio yetu."

"Twende zetu kwa Arkad leo hii hii" akasema Bansir. "Pia tuwapitie rafiki zetu wengine ambao hali zao ni kama sisi wajiunge nasi kupata maarifa ya Arkad."
"Hilo ni jambo zuri Bansir!, Kuwaza kuhusu rafiki zako. Kama ulivyosema, twende tuwapitie na twende kwa Arkad leo hii hii."

Mwisho wa sura ya kwanza
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,575
2,000
TAJIRI WA BABILONI

Hapo zamani, kwenye mji wa Babiloni aliishi mtu mmoja tajiri sana aliyeitwa Arkad. Utajiri wake ulisifika hadi nchi za mbali sana. Pia alisifika kwa utoaji wake. Alikuwa na roho ya utoaji, hakuwa na choyo kwa familia yake na kwa watu baki pia. Wala hakuwa mbahili kwenye matumizi. Pamoja na hayo, kila mwaka utajiri wake uliongezeka kwa kasi kuliko alivyoutumia.

"Siku moja rafiki zake wa utotoni walimuijia na kusema, "Arkad wewe umebarikiwa kuliko sisi. Umekuwa mtu tajiri kuzidi wote katika Babiloni wakati sisi ni watu wa kubangaiza tu. Unaweza vaa nguo bora kabisa na kula chakula kizuri wakati sisi tunavalisha familia zetu kile kinachopatikana na tunakula kile tunachoweza pata."

"Zamani tulikuwa sawa. Tulisoma wote chini ya mkufunzi mmoja. Tulicheza michezo pamoja. Na si katika masomo wala michezo kwamba ulikuwa bora kutuzidi. Na kwa miaka mingi baada ya hapo ulikuwa raia wa kawaida kama sisi tu. Na si kwamba unafanya kazi kwa bidii kuliko sisi au ni muaminifu kutuzidi. Sasa kwanini bahati ikuchague wewe tu kufurahia vitu vizuri vya maisha na kutuacha sisi ihali kila kitu tunafanana?"

Hapo Arkad akapinga na kusema "kama hamjafanikiwa kupata zaidi ya mahitaji ya kuwafanya muishi toka tulipokuwa vijana, ni kwasababu mmeshindwa kujifunza sheria zinazoongoza ujengaji wa utajiri au mmeshindwa kuzitambua."

"Bahati ni Mungu katili ambaye hawezi kumletea mtu mafanikio ya kudumu. Kinyume chake huleta maangamizi kwa karibu kila mtu anayempatia dhahabu. Anafanya wawe watumiaji wabaya ambao baada ya muda mfupi hubaki bila kitu bali matamanio wasiyoweza timiza. Wengine huwafanya wawe mabahili wanaoogopa kutumia utajiri walionao. Wakijua hawana uwezo wa kupata tena iwapo watatumia. Hawa hupatwa na uoga juu ya majambazi na huishia kuishi maisha ya usiri, kujitenga na wasiwasi mwingi.

"Wapo pia ambao huchukua dhahabu waliyofanikiwa kuipata kwa bahati na kuifanya iongezeke. Hawa huwa na furaha na kuridhika. Lakini wa aina hii ni wachache sana. Mi sijawahi ona bali nawasikia tu. Hebu fikirieni kuhusu watu waliopata utajiri kwa kurithi na muone kama ninalosema lina ukweli."

Rafiki zake wakakubali kuwa kwa watu waliowajua kuwa wamerithi utajiri maneno yake ni kweli. Wakamuomba awaeleze ni jinsi gani ameweza kuwa na mafanikio makubwa kiasi kile.

Arkad akaendelea kusema, "katika ujana wangu niliangalia na kuona vitu vingi vizuri vinavyoweza kuleta furaha na kuridhika. Nikagundua kuwa, utajiri hufanya vyote hivyo vipatikane. Utajiri ni nguvu, hufanya vitu vingi viwezekane."

"Mtu anaweza kupamba nyumba yake kwa vitu vya gharama. Kusafiri bahari za mbali na kula vyakula adimu kutoka nchi za mbali'''

"Anaweza kununua mapambo kutoka kwa sonara wa dhahabu au kwa mchonga mawe ya vito. Mwingine anaweza hata kujenga mahekalu makubwa kwaajili ya Miungu."

"Mtu anaweza kufanya hivi na vingine vingi vya kuridhisha nafsi yake."
"Nilipogundua hili nikaamua kuwa nitahakikisha na mimi napata sehemu ya vitu vizuri maishani. Sitakuwa kati ya wale wanaosimama pembeni na kuangalia kwa kutamani wengine wakifurahia maisha. Sitaridhika na kuvaa midabwada. Sitaridhika na vitu vya kimaskini. Nitajitahidi niwe mshiriki wa karamu ya vitu vizuri.

"Kama mnavyojua, mimi ni mtoto wa mfanyabiashara wa kawaida tu. Familia yetu ilikuwa kubwa sana kwa hiyo sikuwa na matumaini ya urithi. Pia kama mlivyosema, sikuwa na akili sana wala vipaji vyovyote kuwazidi. Niligundua kuwa ili kufikia malengo yangu nilihitaji kujifunza na kutumia muda vizuri."

"Kuhusu muda, watu wote tuna muda wa kutosha. Hata nyinyi mlikuwa na muda wa kutosha kuwafanya kuwa matajiri, lakini mmesema wenyewe kuwa hamna kitu zaidi ya familia zenu. Ndiyo kitu pekee mnachojivunia."

"Kuhusu kujifunza, je, mwalimu wetu hakutufunza kuwa kujifunza kupo kwa aina mbili? Aina ya kwanza ni juu ya vitu tunavyofundishwa na kujua. Aina ya pili ni mafunzo yanayotufundisha jinsi ya kutafiti na kuelewa vitu tusivyoelewa."

"Kwa hiyo nikaamua kujifunza jinsi ya kuwa tajiri na kufanyia kazi niliyojifunza kikamilifu. Hamuoni kuwa ni busara kufurahia maisha ingali tupo hai kabla ya kuingia kwenye giza la kifo?"

"Nilipata kazi kama muandishi kwenye jumba la kumbukumbu. Nilifanya kazi masaa mengi nikiandika kwenye mabamba ya vigae. Wiki baada ya wiki na miezi baada ya miezi nilifanya kazi. Hata hivyo sikuwa na chochote cha kuonyesha kwa kazi yangu hiyo ngumu.

Pesa yangu yote iliishia kwenye chakula, nguo, sadaka na vitu vingine vidogovidogo. Lakini sikukata tamaa kuhusu lengo langu.
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,575
2,000
"Siku moja, Aligamishi, tajiri mkopesha pesa, alikuja kwa msimamizi wa mji na kuomba apate nakala ya sheria ya tisa. Alisema kuwa anataka kazi yake ikamilike ndani ya siku mbili. Niliambiwa nikifanikiwa kufanya kazi hiyo kwa siku mbili nitapewa zawadi ya sarafu mbili za shaba."

"Nilifanya kazi kwa bidii lakini sheria ya tisa ilikuwa ndefu sana. Algamishi alipokuja na kukuta kazi yake haijaisha alikasirika sana. Kama ningekuwa mtumwa wake hakika angenipiga. Lakini kwa kujua kuwa msimamizi wa mji asingemruhusu anipige, sikuogopa, nikamwambia "'Aligamishi wewe ni tajiri sana. Niambie jinsi ya kuwa tajiri nami nitafanya kazi yako usiku kucha, asubuhi itakuwa tayari.'

"Akatabasamu na kusema, 'we mjanja sana, basi na iwe hivyo'

"'Usiku kucha nilikesha nikiandika, japo mgongo uliuma na harufu ya utambi iliniumiza kichwa na hadi macho yakawa hayaoni vizuri. Alipofika asubuhi kazi yake ikawa tayari."

"Hapo nikamwambia, 'niambie ulichoniahidi'

"Kijana wangu umefanya sehemu yako kwa ukamili,' aliniambia kwa upole. 'Sasa ngoja nami nitimize sehemu yangu. Nitakwaambia ujuzi huo kwasababu nimezeeka na ulimi wa wazee hupenda kuongea Vijana wanapoomba ushauri kutoka kwa wazee, hupata hekima ya miaka mingi. Lakini mara nyingi vijana hufikiri kuwa hekima ya wazee imepitwa na wakati, hilo linafanya wakose kufaidika.

"Kumbuka hili jambo, jua lililowaka wakati wa baba yangu ndilo hilo hilo litakalokuwa linawaka mjukuu wangu wa mwisho atakapokufa.

"Mawazo ya ujana,' akaendelea kusema, 'ni kama mwanga mkali wa kimondo kinachopita angani kwa kasi. Lakini hekima za wazee ni kama nyota inayoangaza siku zote kiasi kwamba mabaharia huitegemea kuwaongoza.

"Nisikilize kwa makini nitayokueleza na uelewe, vinginevyo kazi yako ya usiku kucha itakuwa ni kazi bure.

"Hapo aliniangalia kwa makini kwa macho yake yaliyokuwa yamefunikwa na makunyanzi, kwa sauti ya chini lakini thabiti, akaniambia.

'''Niliipata njia ya kwenda kwenye utajiri nilipoamua kwamba sehemu ya kumi ya kipato changu ni yangu, na wewe unatakiwa ufanye namna hiyo."

"Hapo akaendelea kuniangalia kwa macho ambayo nilihisi kuchomwa lakini hakuendelea kuongea.

"Ni hilo tu?' nikamuuliza.
"Hilo liliweza kubadilisha mchunga kondoo kuwa mkopesha pesa,' akanijibu.

"Lakini mbona kila ninachopata ni changu mwenyewe?' nikahoji'

"Unajidanganya,' akasema, 'je humlipi mshona nguo? Humlipi mtengeneza makubazi? Haulipii vitu unavyokula? Unaweza kuishi Babiloni bila kutumia pesa? Una nini cha kuonyesha kutokana na kipato chako cha mwezi uliopita? Vipi mwaka uliopita? Unalipa watu wote, kasoro wewe mwenyewe. Usiye na akili! Unafanyia wengine kazi. Ni sawa tu na kuwa mtumwa na kufanya kazi kwa yule anayekupa chakula na mavazi.

"Iwapo ungetunza sehemu ya kumi ya pato lako, ungekuwa na kiasi gani kwa miaka kumi?'
"Hesabu bado zilikuwa zinachaji kichwani mwangu, 'itakuwa sawa na pato langu la mwaka mmoja', nikajibu

"Kwa kiasi fulani upo sahihi' akasema. 'Kila kipande cha dhahabu ulichojilipa ni mtumwa wa kukufanyia kazi. Kila senti unayopata ni mtoto anayetakiwa kukuzalishia. Ili kuwa tajiri, kile unachotunza kinatakiwa kikuzalishie, na watoto wake wakuzalishie pia. Hilo ndilo linaweza kukufanya ufikie matamanio yako ya kuwa na mali.'

"Unaweza dhani nakudanganya na umekesha bure, lakini ninachokupa kina thamani mara elfu ya kazi uliyofanya. Unatakiwa tu kuwa na akili ya kuelewa.'

'''Lazima ujilipe sehemu fulani ya pato lako. Haitakiwi kuwa chini ya sehemu ya kumi ya pato lako hata kama pato lako ni dogo kiasi gani. Lakini inaweza kuwa zaidi ya hapo kulingana na uwezo wako. Lazima ujilipe kwanza na panga matumizi yako vizuri, usinunue nguo na viatu kwa pesa nyingi hadi ukakosa pesa ya kutoa misaada na sadaka.

"Utajiri ni kama mti, unakua kutoka kwenye mbegu ndogo sana. Pesa kidogo unayoanza kutunza ndiyo mbegu ya mti wa utajiri wako. Unavyopanda mapema ndivyo na mti utakua mapema. Na kadri unavyotunza mti wako kwa kuumwagilia kwa kutunza pesa ndivyo utakavyokaa na kufurahia kivuli chake mapema,'

"Baada ya kusema hayo, alichukua mabamba yake na kuondoka."

"Nilifikiria kwa makini kile alichokuwa ameniambia na nikaona kinapatana na akili, nikaazimia kukifanyia kazi. Kila mara nilipolipwa, nilichukua sehemu ya kumi ya pato na kuitunza. Jambo la ajabu ni kwamba sikupata shida yoyote ya mahitaji yangu. Tofauti ilikuwa ndogo sana na baadaye nikazoea.

Akiba yangu ilipoanza kukua nikaanza kupata kishawishi cha kuitumia. Nilitamani kununua vitu vizuri vilivyoletwa na meli na ngamia kutoka kwa wafoenike lakini nikajizuia'

"Baada ya miezi 12 toka Algamish aondoke, akarudi tena. Akaniuliza 'kijana, ulifanikiwa kujilipa sehemu ya kumi ya pato lako kwa mwaka uliopita?'

"Ndiyo mkuu, niliweza," nilijibu kwa kujidai.

'''vema sana,' akajibu akiwa kafurahi, 'umefanyia nini?'

'''Nimempatia Azmur, mfyatua matofali. Aliniambia atafanya safari kwenda nchi za mbali na akifika Tiro ataninunulia vito adimu kutoka kwa wafoenike. Akirudi tutauza kwa bei kubwa na kugawana faida,'

'''Kila mpumbavu anatakiwa kujifunza,' alifoka Algamish, 'kwanini umemuamini mfyatua matofali kwa jambo linalohusu vito? Unaweza kwenda kwa muoka mikate kuuliza kuhusu mambo ya nyota? Hapana! Utaenda kwa mnajimu iwapo una akili. Akiba yako imeshapotea, umeng'oa mti wako wa utajiri. Lakini unaweza panda upya. Jaribu tena na wakati mwingine ukitaka habari za vito nenda kwa sonara. Ukitaka kujua kuhusu kondoo, nenda kwa mfuga kondoo.

Ushauri mara nyingi ni kitu ambacho hutolewa bure lakini kuwa makini na hakikisha unachukua ule unaofaa tu. Anayechukua ushauri kuhusu akiba yake kutoka kwa mtu ambaye hana uzoefu ataipoteza kwanza ndipo atajua kuwa haufanyi kazi'. Baada ya kusema hayo akaondoka.
 
nyalujama

Senior Member
Sep 4, 2020
112
250

Thanks tuko pamoja
 
Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,575
2,000
"Kama alivyokuwa amesema Algamishi, wafoenike walimtapeli Azmur. Walimuuzia vioo vilivyoonekana kama vito. Lakini kama Algamish alivyonihimiza, nikaanza kutunza tena kila sehemu ya kumi ya pato langu. Kwa vile nilikuwa nimeshazoea, haikuwa kazi ngumu.

"Baada ya miezi 12 Algamish alirudi tena, alinitafuta na kuniuliza, 'umefikia wapi toka tulipoonana?'
'''Nimejilipa kwa uaminifu', nilijibu, 'akiba yangu nimempatia Agger mtengeneza ngao, alienda kununua shaba na kila baada ya miezi minne ananilipa.
'''Vyema sana. Na hiyo pesa anayokulipa umeifanyia nini?'

'''Nimefanya karamu kubwa ikiwa na asali, divai na keki zenye viungo. Pia nimenunua kanzu ya rangi nyekundu-angavu na nina mpango wa kununua punda wa kutembelea.'

"Aliposikia hivyo Algamish alicheka, kisha akasema 'unakula watoto wa akiba yako. Sasa unategemea watakufanyiaje kazi? Na watawezaje kuwa na watoto ambao watatakiwa kukufanyia kazi?

Tengeneza kwanza jeshi la watumwa wa dhahabu na utafurahia karamu nyingi bila wasiwasi?
Baada ya kusema hayo aliondoka tena.
"Sikumuona tena kwa miaka miwili. Aliporudi alikuwa amezeeka sana, akaniambia, 'Arkad, umefanikiwa kupata utajiri ulioutaka?' "Sijafanikiwa lengo bado lakini nilicho nacho kinazalisha na kilichozalishwa nacho kinazalisha," nilijibu

'''Bado unachukua ushauri kutoka kwa wafyatua matofali?'
'''Labda kuhusu matofali, hapo wanatoa ushauri mzuri sana,' nikajibu.

'''Umejifunza somo hili vizuri sana Arkad. Kwanza ulijifunza kuishi chini ya kipato chako. Kisha ukajifunza kupata ushauri kwa wale wenye uzoefu na mwisho umejifunza kufanya fedha ikufanyie kazi.

'''Umejifunza jinsi ya kupata pesa, jinsi ya kuitunza na jinsi ya kuitumia. Sasa upo tayari kwa majukumu makubwa zaidi. Mimi sasa nimekuwa mzee na wana wangu wanafikiria kutumia pesa tu, hawawazi namna ya kujiongezea kipato. Miradi yangu ni mingi na nina wasiwasi sitaweza kuisimamia vizuri. Kama utaweza kwenda Nippur na kusimamia miradi yangu nitakufanya kuwa mshirika wangu na utakuwa na hisa kwenye mali zangu.'

"Kwahiyo nikaenda Nippur na kusimamia mali zake, alikuwa na mali nyingi sana. Kwa sababu nilikuwa ni mtu mwenye malengo na sasa nilikuwa nimejifunza zile sheria tatu za jinsi ya kusimamia utajiri niliweza kukuza sana mali zake.

Nilitajirika sana. Algamish alipokufa nilibaki na hisa zangu kwenye mali ile kama alivyoandaa kwenye mkataba." Hayo ndiyo aliyozungumza Arkad.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom