Je, umewahi kupatwa na hali hii au unapitia kwenye hali hii?

Samson Ernest

JF-Expert Member
Aug 28, 2014
404
651
Hali hii ya mgandamizo, yaani unakuwa mzito, wasiwasi mwingi, maswali mengi, unajiuliza hivi nikiondolewa hapa nitaenda wapi?

Mtu anafanya kazi mahali fulani ila haoni kabisa kitu kingine cha kufanya kwenye maisha yake isipokuwa hiyo kazi anayoifanya.

Nikiwa na maana ofisi aliopo, haoni kitu kingine cha kufanya, haoni mahali pengine pa kuajiriwa, amejikuta anaishi kwa mashaka kiasi hata ile nguvu ya kuthubutu kufanya kitu kingine cha kumsaidia kesho anashindwa.

Anaweza kutamani na kupanga kabisa kufanya mambo makubwa ila ndani yake anasikia kelele nyingi, inafika mahali kelele hizo zinamshinda kuendelea kubaki kupanga kutekeleza.

Unaweza kuchukulia kawaida, ila ni hali ambayo sio ya kawaida kabisa, hali hii inawafanya wengine kuwa na msongo wa mawazo na kuwa watumwa ndani yao.

Wakati mwingine mazingira ya kazi au tunayoishi yanatufanya ufahamu wetu ufungwe, kusudi tuendelee kubaki katika hali dhaifu na zisizokuwa na matokeo makubwa.

Kuondoka kwenye hali hii, kuwa mtu wa maombi, Omba Mungu sana juu ya maisha yako, kuna mipaka hutovuka hadi Mungu akutoe.

Mathayo 17:21 NEN
[21] Lakini hali kama hii haitoki ila kwa kuomba na kufungua.]”

Jambo lingine unapaswa kujifunza sana, soma sana neno la Mungu, soma sana vitabu vya kukujenga, hudhuria sana semina na mafunzo ya neno la Mungu.

Kuna maeneo huvuki bila maarifa sahihi, maarifa yanaondoa ujinga mwingi sana kichwani, maangamizo mengi tunakutana nayo kwa sababu ya kukosa maarifa.

Hos 4:6 SUV
[6] Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.

Hakuna laana yeyote anayekutesa kwa umempokea Kristo ndani yako, sababu huna neno ndani yako, kukosa kwako neno kunakufanya ujione bado umefungwa na laana za ukoo.

chukua hatua, hakikisha unakua kiroho, tafuta kwa bidii kuwa na maarifa mengi ndani yako, isiwe ilimradi maarifa, yako ni maarifa sahihi.

Nakukaribisha kwenye group la kusoma biblia kila siku na kutafakari, wasiliana nasi kwa wasap namba +255759808081 ili uunganishwe kwenye group hili zuri la kukuza kiroho.

Mwisho, nikukaribishe kwenye chaneli yangu ya wasap kupata maarifa mbalimbali kama haya kwa mtiririko mzuri, bonyeza kiungo kujiunga na=>>Samson Ernest

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
+255759808081
 
Back
Top Bottom