Kuna siku nilipigiwa simu na mwanamke simfahamu na namba ngeni, akaniita jina fulani (Sio langu) nikamwambia umekosea namba, akakata simu. Wiki chache baadaye akapiga tena, mara hii akataja jina langu kabisa, ninapoishi na hata ninapofanyia kazi, akaniomba nikutane naye mahali kwa mazungumzo, hata nilipomwomba ajitambulishe na wapi alipopata simu yangu akakataa akidai "yote tutayajua tukikutana".
Nikamsisitizia kwamba kama asiposema amepata wapi simu yangu sitaweza kuonana naye hata iweje, alinibembeleza sana tuonane lakini nami nikakomaa, akapotea na hadi leo hatujaonana.
Nikawasimulia marafiki zangu wachache wakanionya kwamba nisikubali kuingia kwenye mtego kama huo. Kwamba kama ningekubali angejilengesha kimapemzi na tukiwa chumbani kuna watu watatuvamia mmoja akidai kwamba ni 'mume wake', na watanipiga picha na kudai kuzisambaza picha hizo mitandaoni hadi niwalipe fedha.
Je, nawe umewahi kukumbana na kisa chochote ambacho umenusurika? Labda umekwepa kutapeliwa? Umeepuka kuibiwa au umenusurika janga lolote? Tiririka hapa ili nasi tujifunze kutokana na kisa chako.