Umewahi kujiuliza hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umewahi kujiuliza hili?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by WomanOfSubstance, Aug 9, 2010.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Maisha ya mwanadamu hayazidi miaka 70 wachache kuenda hadi 100 kwa wale waliojaaliwa kuishi umri mkubwa, achilia mbali life expectancy ambayo kwa Watanzania kufuatia UKIMWI kuwa tishio na magonjwa mengine kama shinikizo la damu, cancer etc,hayazidi miaka 50.

  Chukulia kuwa toka kuzaliwa hadi uweze kusimama kwa miguu yako mwenyewe kimaisha, ukijumlisha na miaka ya kusoma hadi chuo ni miaka 25. Halafu ongezea miaka mingine kama 15 ya kujijenga kimaisha ( kuanzisha familia yako na kujiweka sawa kiuchumi) kwa walio wengi ukiondoa wachache wenye kukuta wazazi wamewawekea kila kitu au labda waliorithi, au kubahatisha kupata mali upesi kwa njia halali au labda zisizohalali! Hapo tayari ni miaka 40. Ongezea hapo miaka mingine 20 ya consolidation na kustaafu = 60.

  Baada ya hapo ni mtu kupumzika na ama kula jasho lake au kuanza msoto mkali wa kutafuta riziki baada ya kustaafu, ilhali mwili na hata akili vimeanza kuchoka kwa miaka 10 = 70 ambapo ndio umri mrefu wa wastani wa binadamu kuishi.

  Huwa najiuliza, hivi binadamu tuna raha gani ya maisha? Je wewe mwenzangu huwa unajiuliza maswali gani ya kifilosofia juu ya maisha?
   
 2. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  mh hii kweli imetulia manake nami nimekuwa najiuliza hichi kitu bado sijaona raha ya maisha manake kwa huu mchakato ulivyo kwenye dunia yetu ni kumshukuru mungu kwa neema na kila hali tulizonazo,tuendelee tu kuishi kwa matumaini na tufanye kazi kwa kama hatufi leo au kesho kisha tufanyiane mema na kusaidiana kama tutakufa muda huu.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Aug 9, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Huwa najiuliza sana hayo maswali mimi. Ila raha ya maisha ipo bana. Nikianza kurodhesha raha za maisha nitajaza ukurasa. Vivyo hivyo kwa karaha.

  Kama hatima yetu sote ni mauti, ya nini kuhangaika na kufanya mambo kama kusoma? Ukiamua kusoma hadi ngazi za juu kabisa huenda ukaishia kutumia muda mwingi wa maisha yako kusoma kuliko kutumia ujuzi ambao unausomea. Sasa shida yote hiyo ya nini wakati hayo makaratasi ya shahada utayaacha duniani? Kwa nini tu usile raha kwa mtindo wa full kujiachia....si maisha mafupi bana?

  Kuna raha gani kukesha usiku kucha na kukariri na kusoma maneno ya kwenye mavitabu?
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Aug 9, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Pia ushawahi kujiuliza usawa wa binadamu uko kwenye jambo lipi? Maana binadamu tumetofautiana sana - tumetofautiana rangi, mwonekano, akili, busara, hekima, sauti, hulka, haiba, mahitaji, matakwa, mapenzi, tajiriba, n.k. n.k.

  Je, ni kipi ambacho kinatufanya sote tuwe sawa?
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kobe, kweli hili la kuishi kwa matumaini nadhani ndilo haswa linatusukuma kuendelea kuchacharika kama hakuna kufa!
  NN, Nimekupata .Nilivyosema hakuna raha ya maisha nilitumia msemo huo kwa wepesi zaidi lol. Ni kweli raha zipo na haijalishi uko tajiri au maskini maana zipo za kila aina na gharama zake ni hivyo hivyo.
  Mimi la kusoma halinipi shida sana maana kweli kusoma ni kuongeza maarifa kutegemeana na mtu unataka maarifa kwa kiwango gani. Kinachonipa kuwaza sana ni shughuli tunazozifanya almost 16 hours kati ya masaa 24 yaliyoko kwenye siku moja.Tunahangaika mno! Wapo pia ambao hawajishughulishi kivile lakini hawa nao ndio wale wanaosubiria fainali ngumu uzeeni kama Mungu kawajalia maisha marefu.
   
 6. M

  Malunde JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Job 7:7 ¶ O remember that my life is wind: mine eye shall no more see good. {shall...: Heb. shall not return}. Job 10:12 Thou hast granted me life and favour, and thy visitation hath preserved my spirit. Compare and contrast the two bible verses you might get your answer
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Aug 9, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Wewe nawe bana...biblia ni fiction tu. Haijibu chochote as far as real life is concerned....
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hili nalo ni la msingi kabisa.Ni swali lenye kuzungusha kichwa na kufanya mtu ufikiri hadi kushindwa kufikiri tena. Ukiangalia binadamu tulivyoumbwa tuko tofauti kabisa kwa kila hali kama ulivyoainisha hapo juu. Na wakati mwingine unaweza kutaka hata kuuliza kwanini kuna tofauti zote hizi ilhali tunaambiwa na vitabu vya dini kuwa tuliumbwa kwa mfano wa Mungu ambaye ana upendo na haki.......lakini unaweza kuona hatuko sawa kwa namna tulivyoumbwa.Ila kuna kitu kinatufanya tuwe sawa - sote ni binadamu, wenye roho, wenye kuvuta hewa ya oxygen ili tuishi, na kwa vigezo hivi pengine kwa urahisi twawezasema tuko sawa.

  Ila bado tutajiuliza zaidi, mbona kuna tofauti sana miongoni mwetu? Mbona wengine wamejaaliwa kuliko wengine? Kuna wenye kufanya kazi kwa bidii na hawafanikiwi sana.Kuna wenye kuweka juhudi kidogo sana lakini mambo yao yako supa!
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Aug 9, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Dah...WoS leo umenirudisha kwenye darasa langu la Philosophy 101, Advanced Philosophy, Truth and Knowledge, Epistemology, Mind, Language, and Logic, Existentialism and Phenomenology, etc.

  Damn I was good in that class....Lol
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  tell us!
   
 11. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #11
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndio maana sometimes mtu ukipata kijichance cha kujirusha, jirushe sawasawa, huwezi jua kama kesho itakuwaje. Life is too short to take it siriazzz...
   
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sisi ambao wenye kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu tunaamini kuwa tumeumbwa kwa maumbo, tabia, tofauti za rangi, mwonekano, akili, busara, hekima, sauti, hulka, haiba, hurka, jamii na tofauti zingine ili tupate kujuana (Kufahamiana). Vile vile Utajili na umasikini pamoja na ufukara ni mtihani Anaowapa Mola waja wake, katika mitihani ya kila aina iliyomo katika maisha ya binaadamu, mitihani mizuri na mibaya yote ni mitihani. Mfano, binaadamu anapopewa mali basi ajue kuwa ni mtihani huo kuwa vipi ataitumia mali yake, akijaaliwa kupewa elimu atajaribiwa pia kuwa vipi ataitumia elimu yake, akipewa akili na siha, vyote atajaribiwa navyo kuwa vipi atatumia neema hizo.

  Mitihani mibaya kama kufiwa, maafa, ufukara, magonjwa na kadhalika yote ni mitihani anayopewa mwanaadam kutazamwa kama atasubiri au atakufuru.
   
 13. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  haya.... tuendelee
   
 14. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ukifikiria kwa undani kabisa hayo uliyoandika, unaweza kujiuliza hivi kwanini mtu aamue kuwa mwizi na kufisadi jamii kubwa wakati maisha yenyewe ni mafupi sana? Hivi kuhodhi mabilioni ya pesa kwa wizi, ghiriba na udanganyifu ni sahihi wakati kuna watu wanataabika? Kwakweli kila mtu akifikiria kuwa maisha ni muda mchache nadhani dhana hiyo inatosha kabisa kuacha ujambazi na kuishi katika misingi inayokabalika.
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hili neno!
   
 16. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  WOS we have been told that raha tunayo itaka siye haipatikani hapa duniani..ndo maana mtu usijishughulishe saaaaaaaana na mambo ya dunia....we have been told also that GOD has said that he has created us to test us, to see which of us is best in deeds. He is not testing us to know, in the sense that he doesn't already know, but this world is a test for us in order that we can grow spiritually.

  We cannot develop this spiritual characteristic of generosity unless some of us have more then others and then we are required to give of the wealth we have. When we give, we grow. Similarly, if we were not in a position where others had more than us then we wouldn't have the ability to develop the higher spiritual quality of contentment, patience, satisfaction in what God has given us.

  So it is all there in order to bring out the higher spiritual qualities, which enable us to attain the state, which makes us suitable and eligible to return to paradise. The paradise from which we were created, we were created in paradise and for paradise. Through our choices we have left, in this life, a field of testing, where we can grow to a state where we deserve paradise.

  This life is a test. A test for us, will we worship GOD, or will we forget Him....
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Aug 10, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  WOS mie huwa nawaza nachoka namwachia mungu nadhani ukiwaza sana unaweza kuchanganyikiwa...
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Aug 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kwani wew WOS raha kwako ni nini ?

  maana mie naona raha zimejaa kila kona ya dunia hii, raha ndogo ndogo na kubwa kubwa....................
   
 19. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #19
  Aug 10, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  G nadhani ukifanya kazi 16 hours u wouldnt call tht raha...plus raha ya hapa duniani huwezi kuipata kama hujapata tabu kwanza..there's no such thing as a free lunch
   
 20. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #20
  Aug 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Maisha ni safari sio kituo: Duniani tunapita!
   
Loading...