rosemarie
JF-Expert Member
- Mar 22, 2011
- 6,887
- 3,412
AlhamduliLllah, magari sio gari.
Unaendeshwa au unaendesha?
AlhamduliLllah, magari sio gari.
Unaendeshwa au unaendesha?
Jamaa aliibiwa gari kutoka nje alipoona gari halipo akaanza kujisachi mfukoni...
Yes,OTIS, namshukuru mungu kwa sasa nimekua,
Wakati ule ilikuwa 2002 na sasa 2012,
Ila inapokuja ishu ya kuibiwa gari mmmh!hapo hakuna cha utoto wala ukubwa!
Huyo alikuwa Anaiba gari la Babake kwenda nalo Club hata Sie Tumefanya Sana Hadi Tukawa Tunaachiwa Funguo Ili Tusiibe haha... Ilikuwa kabla ya Kuliiba mnalisukuma hadi Nje ya Gate Mnaliwashia barabarani kabisa asije amka then hivyo hivyo wakati wa kurejea alfajili, Mnapima mafuta yaliishia wapi mnajazia tukikosea tu inakula kwetupoleni wote. aliyeiba ndo zaidi.
ulikuwa kidato cha ngapi?Haya mambo ya kuibiwa haya sio mazuri kbs,
Niliwahi kuibiwa simu enzi hiyo ya simems ile ya kidole gumba nikiwa natoka likizo narudi shule pale iringa stend,
Nilichanganyikwa nililia mpaka nafika bwenin usiku kucha sikulala kesho yake mapema nikapanda basi kurudi dar,
Nimefika huku watu wananishangaa niliingia hm kwa anko nakilio cha haja,wakanihurumia ila akaninunuliwa nyingine nikarudi shule,
Huwa wananikumbushaga na kunicheka sana!!
Nimewahi kuibiwa kipedo, nililia nikazimia mara 6.
Ndio matatizo ya kutembelea gari yenye 3rd part insurance, huwi na amani
ulikuwa kidato cha ngapi?
Unafanya mchezo na kufaulu kwenda 4m five!
Yani ilikuwa ndio zawadi baba alinihadi so nipofaulu tu mzee wangu akanikabidhi lol!
Aalafu hata sijafika shulen kwenyewe wakaniibia weeeeeee!
Mbona nilipagawa nikafunga safari!
Pole sana!
Loh! Hicho kipedo lazma kilikuwa na zindiko la babu wa mlingotini, bagamoyo! Sio bure!
hahahah we noma aisee!!
Mimi nilipaki gari kwenye mzunguko wa soko la Kariakoo nikaingia shimoni nilipotoka nikatokea upnade mwingine na ugeni wa soko kipindi hicho nilikuwa nakimbia kama mwizi around soko na kagari kenyewe ka mkopo hata mwezi nilikuwa sijamaliza.Ilinichukua kama nusu saa hivi kuipata hapa jasho lishanitoka sehemu zote za mwili.
Jamani nyi acheni yasije kuwakuta, july 20 mwaka huu baada ya kujibana sana nikaamua niingie ulimwengu wa blackberry, nimetoka kununua pale sapna nikaiweka kwenye gari na kuondoka mpaka kitega uchumi kumchek jamaa yangu ofisin kwake, ile narudi nikakuta kioo kimenyofolewa cha kushoto siti ya nyma na milango ikatolewa lock, jamaa walichukua simu mpya kwenye box, laptop mbil, binafsi na ya ofis na vitu vingine vidogovidogo, yaan nilikuwa kama nimedata, ikabid nitafutiwe dereva wa kunirudisha home maana ningegonga, chakula kilikuwa hakipiti, na hata job sikwenda karibu wiki, jamani haya mambo yasikie kwa mwenzako yakikukuta ni balaa, hadi niliwaza kwa nini nimemtembelea jamaa ofisin