Haya mambo yapo sanaa,mimi ilinitokea mwanangu mdogo...kwa mara ya kwanza nimempeleka na mke wangu kuwasalimu wazee kijijini,mchana fulani tukiwa ndani tulisikia mtoto nje akicheka kicheko kikubwa sanaaaa,mke alikuwa kalala na mtoto alikuwa nje na bibi yake,bahat mbaya au nzuri,mama yangu alishuka bondeni mtoni..mtoto akabaki peke yake kama dk 10 hivi.
Kicheko cha mtoto ndio kilistua,alikuwa anacheeeka sana,kuchungulia..hamad!!!mtoto anajiviringisha na nyoka,nyoka anapanda,anamzunguka shingoni..mara ajiviringishe mkononi,haraka nikamuita mama watoto...ile kuona tu na ka...ji...ko...jo..le,mara huyo kadondoka...mimi nimesimama kimyaaa...kimba inagonga pichu...natetemeka balaa,kilichonishangaza ni kuwa nyoka akitaka kuondoka mtoto analia sana...nyoka anarudi,walicheza around 45''...kwa kweli nilitetemeka sana...kumbe Mama yangu anaiona movie yote,ila kajificha kweenye vitindi vya ulanzi,woga wake ni sisi kupanic na kupiga kelele kitu ambacho nyoka angemdhuru mtoto.
Kama baaada ya dakika 45 hivi nyoka akaanza kuondoka,mtoto nae akatambaa kumfuata nyoka machakani...nyoka akaenda baadae akasimama,mtoto akamshikashika...nyoka huyoooo akapotelea..mtoto akashindwa kuingia machakani akaanza kulia,tukajua labda kamuuma kwa kile kilio,kumbe wapi.
Nilitimua mbio kumnyakua mtoto kama mwewe,haya mambo yapo sana...kwaa kweli mi sitasahau...mke wangu ndio alipata kiwewe sana ukizingatia ni wale waliokulia kimjini mjini,Nimeona watu wametoa maelezo ya kibaolojia/kisayansi,japo kimila hii mambo ina tafsiri yake pia.