Umewahi Kuchunguza kwanini Nyoka hamdhuru Mtoto!?

Umewahi Kuchunguza kwanini Nyoka hamdhuru Mtoto!?

Inasemekana adrenaline hormone inayozalishwa pale mtu anaposhtuka kwa kumuona nyoka ndio inasababisha ang'atwe kwani nyoka anahisi hatari inayomkabili na anajihami mapema. Na ndio maana inasemekana kama hujamuona nyoka na yeye kakuona hawezi kukudhuru, kwa kuwa hakuna adrenaline inayozalishwa. Wataalamu wanasema nyoka inahisi adrenaline inayozalishwa katika mwili wa binadamu.
Kwa watoto nadhani hiyo ishu ya adrenaline hormone ina-apply, kwa sababu hawajui hatari ya nyoka.

umejibu kitaharamu sana,safi sana
 
Angalau leo nimelewa sababu. Natumai kuna ukweli. Nasikia na paka wako hivyo hufeel mtu mwpga na ndie anaemfuata.
 
Kwa kweli there're somethings which are exeptional, mimi nimemshuhudia mtu mzima kabisa mwenye wajukuu hadhuriwi na nyoka wa aina yoyote ile, Yule mzee alikuwa pacha na inasemekana tangu utotoni walikuwa na hiyo hali na nyoka, Yeye nyoka akimuona anakuwa mpole kama nini anashindwa hata ku move, Kuna incident moja tulienda kuvuna mahindi shambani kwake, wakati wa kula kule shambani mzee alivua saa yake akaiweka juu ya kisiki akaisahau akakumbuka tumefika nyumbani, akawasha pikipiki tukairudia tukakuta bonge la nyoka aina ya kifutu ameizunguka ile saa, mzee akamchukua nyoka akamning'iniza shingoni akawasha pikipiki baada ya umbali flani akamtua na kumwacha aende zake, Kwa wale waliokuwa wanamfahamu amefanya kazi kama afisa elimu takwimu Mbozi baadae.Mbarali in late 1990s now ni Marehemu. Hii makitu ipo ingawa nimekuwa impressed na maelezo ya kibailojia about Adrenaline hormone.

Jf raha sana
 
Watu wametoa maelezo mazuri lakini kuna wanyama ni wakorofi tu kama FISI!

Fisi acha kabisa yule hata uwe usingizini anakupitia.Nimecheka juzi nikiangalia NAT Geo. FISI wakimshambulia SIMBA mkubwa tena dume hadi wakamla mpaka mifupa!!
 
The answer is simple: Law of Love applies. When you act lovely towards anything the reaction you receive is love. Unapomwona nyoka ukahamaki the impression he receives is that you've considered him a threat therefore anakuona wewe ni threat kwake vile vile, lazima ajihami.

lugha ilikuja kwa meli hii!
 
Inasemekana adrenaline hormone inayozalishwa pale mtu anaposhtuka kwa kumuona nyoka ndio inasababisha ang'atwe kwani nyoka anahisi hatari inayomkabili na anajihami mapema. Na ndio maana inasemekana kama hujamuona nyoka na yeye kakuona hawezi kukudhuru, kwa kuwa hakuna adrenaline inayozalishwa. Wataalamu wanasema nyoka inahisi adrenaline inayozalishwa katika mwili wa binadamu.
Kwa watoto nadhani hiyo ishu ya adrenaline hormone ina-apply, kwa sababu hawajui hatari ya nyoka.

Na kama ni hivo, iweje amgonge mtoto baada ya kustuliwa na mwingine? Adrenaline hormone aihisi kwa mstukaji, kugonga agongwe mtoto. INAKUWAJE???
 
Vipi kuhusu watu wenye sura za kitoto(baby face),nao hawapati madhara?
 
wanyama ni wanyama tu hata binadamu ni sehemu yao ndio maana wewe ukiona mtoto wa simba,chui, nyati nk aliezaliwa jana yuko peke yake wala hukimbii tena waweza kumchukua eti ukamfuge kwako.
 
Nshawah tembelewa na tandu mwilini bila kujijua wala hakunidhuru tena ni wale wekundu wenyesumu nilipogundua ni tandu niliogopa sana ila alikuwa tayari amesha shuka miguuni kwangu hiyo fact its kinda true.
 
Naomba mtu anielezee ilikuwa kuwaje hadi chatu akawaua hao wavulana.

mzee umeshaambia kuwa watoto , yani wale wasioelewa baya na jema mara nyingi hata kutembea wanakuwa bado. sasa wewe vijana wa miaka saba na tano hao ni watot wasiotambua madhara ya nyoka? huoni hapo adrenaline hormone itazalishwa kwani hiyo adrenaline hormone inazalishwa na hofu ya mtu na kwa matinki hiyo hao watot walikuwa na hofu
 
Haya mambo yapo sanaa,mimi ilinitokea mwanangu mdogo...kwa mara ya kwanza nimempeleka na mke wangu kuwasalimu wazee kijijini,mchana fulani tukiwa ndani tulisikia mtoto nje akicheka kicheko kikubwa sanaaaa,mke alikuwa kalala na mtoto alikuwa nje na bibi yake,bahat mbaya au nzuri,mama yangu alishuka bondeni mtoni..mtoto akabaki peke yake kama dk 10 hivi.
Kicheko cha mtoto ndio kilistua,alikuwa anacheeeka sana,kuchungulia..hamad!!!mtoto anajiviringisha na nyoka,nyoka anapanda,anamzunguka shingoni..mara ajiviringishe mkononi,haraka nikamuita mama watoto...ile kuona tu na ka...ji...ko...jo..le,mara huyo kadondoka...mimi nimesimama kimyaaa...kimba inagonga pichu...natetemeka balaa,kilichonishangaza ni kuwa nyoka akitaka kuondoka mtoto analia sana...nyoka anarudi,walicheza around 45''...kwa kweli nilitetemeka sana...kumbe Mama yangu anaiona movie yote,ila kajificha kweenye vitindi vya ulanzi,woga wake ni sisi kupanic na kupiga kelele kitu ambacho nyoka angemdhuru mtoto.
Kama baaada ya dakika 45 hivi nyoka akaanza kuondoka,mtoto nae akatambaa kumfuata nyoka machakani...nyoka akaenda baadae akasimama,mtoto akamshikashika...nyoka huyoooo akapotelea..mtoto akashindwa kuingia machakani akaanza kulia,tukajua labda kamuuma kwa kile kilio,kumbe wapi.
Nilitimua mbio kumnyakua mtoto kama mwewe,haya mambo yapo sana...kwaa kweli mi sitasahau...mke wangu ndio alipata kiwewe sana ukizingatia ni wale waliokulia kimjini mjini,Nimeona watu wametoa maelezo ya “kibaolojia/kisayansi“,japo kimila hii mambo ina tafsiri yake pia.
 
Ni kwasababu ya sense of INNOCENCE: Nitaeleza

Kwa kawaida mtu anapopata mstuko huexcrete hormones ambazo humfanya ajihami na kuwa tayari kushambulia wakati wowote. Kimsingi hutoa adrenaline, hii huongeza hasira, nguvu na mambo mengine kama hayo. Sasa.......... adrenaline hutoa harufu au hujenga muunganiko (Nashindwa kuuelezea kibiolojia) na kile kitu ambacho kitashambuliwa. Mfano mtu anapokasirika kama amemkasirikia mwingine, ile hormone humvuta na kumjenga yule anayekasirikiwa na hatimaye naye huanza kujihami. Ndo maana mtu akikukasirikia utajikuta na wewe unamkasirikia (We become suggestible to other people's emotions) au kulia unapomuona mwingine analia hata kama hujui ni kwanini analia.

Back to the topic: Kwa vile mtoto ana sense of innocence, akimuona nyoka, wala hatastuka na adrenaline haitakuwa excreted na hivyo kutomjengea hali wa kujihami. Jambo hili halitamfanya Nyoka naye kujihami so anaweza "kucheza" na mtoto bila shida na bila kumdhuru. But akitokea mtu mzima ghafla na anastuka na kuexcrete adrenaline, then huyo nyoka anaweza kumng'ata mtoto kwasababu ya "mistaken identity" (kama ulivoambiwa ukimstua nyoka atatema SUMU kwenye mbege)

Nimejibu kwa maelezo ya kawaida (a layman's knowledge)
Museme na aina ya nyoka jamani aje chatu amwone mtoto hata awe kazaliwa sasa hivi kwake ni lunch made easy!
 
Kwa hiyo na sisi ni MALAIKA TULIOZEEKA?

Afadhali tungekuwa malaika tuliozeeka tu, tuliasi na kumezeeeka katika uasi. Pia hatutaki kamwe kuweka silaha chini. Yote kwa yote, majibi sahihi yametolewa na kuungwa mkono.
 
Jamani kweli JF ni darasa tosha, nimepata maarifa ya kutosha juu ya results of reaction connected to this topic. ni kweli the Law of Love or the sense of innocence linked to Adrenaline hormone ndicho chanzo. nimeamini kweli pasipo maarifa ni majanga tu na hii nadhani ni applicable kila kona ya maisha.
 
mzee umeshaambia kuwa watoto , yani wale wasioelewa baya na jema mara nyingi hata kutembea wanakuwa bado. sasa wewe vijana wa miaka saba na tano hao ni watot wasiotambua madhara ya nyoka? huoni hapo adrenaline hormone itazalishwa kwani hiyo adrenaline hormone inazalishwa na hofu ya mtu na kwa matinki hiyo hao watot walikuwa na hofu

Kwa hiyo mtoto wa miaka mitano au saba siyo mtoto? Wapi katika hii mada umri wa mtoto umekuwa specified au defined?

Naomba nionyeshe kama kuna mahali kwenye hii mada ambapo umri umekuwa specified, tafadhali.

Na huyu wa miaka 2 naye si mtoto?

A 2-year-old Florida girl died after being strangled by a pet python that escaped from its aquarium and attacked her in her crib, police said.
 
Back
Top Bottom