Dr. Mwigulu Nchemba
JF-Expert Member
- Feb 25, 2012
- 416
- 2,037
(1) Mandela had a VISION and MISSION in his Struggle. Hakuwa na uroho wa madaraka, alipokamilisha aliachia madaraka. KUNA WANASIASA WA KIAFRIKA MALENGO NI MADARAKA, AKISHIKA MADARAKA MPAKA AFE TU. Tumewaona kwa Tanzania hata kwa madaraka madogo ya Tasisi ndogo akishika mpaka afe azikwe kwanza ndio wengine mfikirie nafasi aliyokuwa nayo.
(2) Mandela WALKED THE TALK, Alisimamia, alitenda na aliishi sawasawa na anayosema. Hakuyafanya aliyokuwa hayapendi wakoloni wayafanye walipokuwa madarakani. Kwa Tanzania kuna viongozi wanadhani jambo ni baya likifanywa na chama tawala tu, au serikali tu au na viongozi wa serikali tu ila wakifanya wao ni jema. Wanakemea likifanywa na serikali ila wao wanafanya hayohayo hata bila ya kuwa na serikali.
(3) Mandela alisamehe na Kuanza ukurasa mpya. Alipokea mamlaka akaongoza Taifa wakiwemo na waliomtesa. Kwa kiongozi kusamehe ni jambo la msingi. Sio busara kutafuta madaraka na kwenda kufanya kazi moja tu, KULIPA VISASI.
(4) Mandela alikuwa mwadilifu, mzalendo wa kweli aliyeweka maslahi ya Taifa mbele. Alikuwa mtaifa.
(5)Mandela hakuwa Mtu wa kukata tamaa,He was the last Person to give up.
R.I.P NELSON MANDELA