Umetutoka Mandela,mambo haya matano ni msingi wa siasa zetu vijana

Dr. Mwigulu Nchemba

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
416
2,037
1474622_186180934917476_369947093_n.jpg

R.I.P Mzee Nelson Rolihlahla Mandela. Tutakukumbuka kwa Mengi Mazuri. Kama mwanasiasa kijana nayaona mambo matano (5) kati ya mengi
(1) Mandela had a VISION and MISSION in his Struggle. Hakuwa na uroho wa madaraka, alipokamilisha aliachia madaraka. KUNA WANASIASA WA KIAFRIKA MALENGO NI MADARAKA, AKISHIKA MADARAKA MPAKA AFE TU. Tumewaona kwa Tanzania hata kwa madaraka madogo ya Tasisi ndogo akishika mpaka afe azikwe kwanza ndio wengine mfikirie nafasi aliyokuwa nayo.

(2) Mandela WALKED THE TALK, Alisimamia, alitenda na aliishi sawasawa na anayosema. Hakuyafanya aliyokuwa hayapendi wakoloni wayafanye walipokuwa madarakani. Kwa Tanzania kuna viongozi wanadhani jambo ni baya likifanywa na chama tawala tu, au serikali tu au na viongozi wa serikali tu ila wakifanya wao ni jema. Wanakemea likifanywa na serikali ila wao wanafanya hayohayo hata bila ya kuwa na serikali.

(3) Mandela alisamehe na Kuanza ukurasa mpya. Alipokea mamlaka akaongoza Taifa wakiwemo na waliomtesa. Kwa kiongozi kusamehe ni jambo la msingi. Sio busara kutafuta madaraka na kwenda kufanya kazi moja tu, KULIPA VISASI.

(4) Mandela alikuwa mwadilifu, mzalendo wa kweli aliyeweka maslahi ya Taifa mbele. Alikuwa mtaifa.
(5)Mandela hakuwa Mtu wa kukata tamaa,He was the last Person to give up.

R.I.P NELSON MANDELA
 
Kama hayo unayoyasema ndiyo unayotaka kumaanisha, jibu maswali yafuatayo:-
  1. Mbona nafasi ya M/Kiti wenu huwa haigombewi na wanachama wengi?
  2. Kama kuachia madaraka kwa amani ndio desturi yenu, mbona mmeng'ang'ania madaraka kwa zaidi ya nusu karne na hata pale mnaposhindwa kwenye chaguzi huwa mnachakachua kura?
  3. Wee gamba gumu, kwanini chama chako kimejaa mafisadi wa kutisha, wezi, wauaji na wabakaji lakini hayo huyaoni, wewe akili yako inaona yanayofanywa na wapinzani tu?
  4. Hivi ile falsafa ya M/Kiti wenu Dr. KIWETE ya kujivua gamba iliishia wapi?
  5. Hivi ile miezi 6 ya Mangula haijaisha tu?
Hizi siyo zama za kudanganya Watz, rudi ukajipange upya muuaji mkubwa wewe!
 
Mandela help save the souls of many people for their crimes against humanity, that's not easy to live with. But thanks to Mandela he gave them away to get over their fears and hatred, and learn to act as decent people toward all. At the same time he lead his own people to not be resentful and seek revenge. That deserves world recognition.
 
Mandela hakuwa akiua watu kwenye mikutano ya wapinzani wake kisiasa kwa kutumia mabomu ya Kichina kama alivyofanya Mwigulu huko Arusha

Lakini ushahidi wameukalia Mbowe na Lema kwa kisingizio kwamba mpaka iundwe tume halafu wanajiita wazalendo.Hii ni kejeli kwa wahanga wa tukio la bomu Arusha.
 
Mandela hakuwai kamatwa gest na mke wa mtu kama we ulivokamatwa igunga

Rejea ya Hotel 56 Dodoma babu alipochomokea dirishani akiwa kama alivyozaliwa huku akijistiri kwa pazia la hotel na kutokomea kusikojulikana.
 
Punguza font size, it's too much kwa habari nzima kuwa na font hiyo.

Back to topic, na nyie jifunzeni ku-walk the talk, sio kumaliza tembo wetu tu.
 
Mimi nnajiuliza siku nikifa ntakumbukw kwa kitu gani au ni mchango gani nimefanya kugusa maisha ya watu.
Na wewe Mwigulu Nchemba unajiuliza hayo maswali? na kama unajiuliza hayo maswali na ni mkweli kwa nafsi yako, unajisikiaje?
 
Last edited by a moderator:
Hayo mengine yanzishie mada yake tupo na migulu apa ambae anakila aina ya uchafu
Rejea ya Hotel 56 Dodoma babu alipochomokea dirishani akiwa kama alivyozaliwa huku akijistiri kwa pazia la hotel na kutokomea kusikojulikana.
 
Kujaribu kutumia kifo cha Nelson Mandela kuhalalisha hizi siasa uchwara na maji taka ni kumvunjia heshma Mandela. Mwacheni Mzee wa watu apumzike kwa amani.
 
Maneno haya yangekuwa na maana yangesemwa au kuandikwa na mtu mwenye moyo safi na dhamira ya.kweli. je kwenye kinywa kilekile kunaweza kutoka baraka na laana? Mtu hujulikana kwa matunda yake na siyo kwa maneno yake.

'Mtawajua kwa matunda yao'.
 
Na kwa hakika kitu kimoja ambacho kinanifanya nimtpfautishe Mandela na viongozi wengine wala sio harakati zake za kupambana na ubaguzi na kuhakikisha SA huru bali ile hatua yake ya kuanzania Kamati ya Mapatano na Maridhiano.

Hakuna mwanadamu ambae angependa kutawaliwa na kudhalilishwa milele hivyo hata kama Mandela asingetokea bado wangetokea wengine wakapigana dhidi ya ubaguzi.

Lakini linapokuja suala la mapatano na maridhiano, ni very exceptional issue. Inawezekana kabisa kwamba kiongozi mwingine yeyote ambae angekuwa ni first Black President SA nae asingependa suala la visasi kutokea lakini sidhani kama angefanya kama alivyofanya Mandela; kwamba watu(tena wazito) wanajitokeza hadharani, mbele ya TV na kukiri makosa yao bila kujali kwamba wewe ni Kaburu au Mwafrika wa ANC; provided ulihusika kwa namna moja au nyingine, lazima uhojiwe.....haikuwa ni kamati dhidi ya Makaburu peke yao bali hata manguli wa ANC kwavile Mandela alifahamu kwamba wakati wanapinga ubaguzi hata wana-ANC nao walifanya mambo kadhaa yasiyo ya kibinadamu!! Hakumuachwa hata mke wake anayeheshimika sana, Winnnie Mandela....wote wakahojiwa mbele ya tume huku mahojiano yakirushwa Live; very impressive!

Mandela alifahamu wazi kwamba kama angewataka watu wasemeheane kwa kauli tu kutoka Ikulu, basi watu wasingesameheana; lazima visasi vingekuwepo!

Rest In Peace Madiba!
 
mandela hakuamini katika udini,ukanda wala siasa za maji taka
 
Mandela, hakuwahi kuwa na ushahidi wa Mbinguni na Duniani, na utashindwa hatua za awali Duniani.
 
Na wewe uache siasa zako za kijasusi!! kijana mdogo mambo yako kama Savimbi kunywa damu za watu.
 
Back
Top Bottom