Zanzibar 2020 Dkt. Hussein Mwinyi ni Mandela mpya wa Visiwa vya Zanzibar

Oct 1, 2019
79
150
DK. HUSSEIN MWINYI NI MANDELA MPYA WA VISIWA VYA ZANZIBAR

Deogratias Mutungi


Siasa imara ni zao la ustawi wa amani na maendeleo ya watu, Siasa ni chemichemi na kiungo cha utaifa wa mtu na mtu, Siasa mbovu ni chanzo cha matatizo na mifarakano inayo hatarisha utu na uhai wa binadamu aidha bila siasa safi ni vigumu kuwepo upendo na umoja wa kitaifa katika mifumo ya uzalishaji mali na kiuchumi, Siasa na amani ni uzao wa tumbo moja mtindo wa siasa unaojikita katika amani uzalisha misingi imara inayojenga tabaka la watu wanao heshimiana na kuishi kama ndugu hata kama wanatofautiana kiitikadi au wana mirengo tofauti, Siasa safi ni mawio na machweo ya mustakabari wa taifa la kizalendo lenye utu, heshima na maendeleo bora kwa wananchi wake wote bila ubaguzi wa aina yoyote ile

Historia inatufundisha na ipo wazi kabisa kuwa taifa linaloendesha siasa za chuki, ghiriba, ubabe, nongwa na hila uzalisha jamii yenye “gubu kisiasa,” ombwe la amani na utindio wa fikra za kimantiki katika kujenga jamii iliyo salama zaidi kwa watu wake na matokeo uwa ni mitafaruku ndani ya nchi baina ya mtu na mtu kikundi kwa kikundi, alama ya maendeleo na ustawi wa nchi ni matokeo ya amani, aidha ni wazi kuwa uhuru wa amani ndio sehemu kuu ya maisha ya binadamu hapa ulimwenguni kabla ya kitu chochote.

Andiko hili linapozungumzia gubu za kisiasa linamaanisha kuwa ni chuki ambazo upandikizwa na wanasiasa kwenda kwa wananchi wema wakiaminishwa amani si chochote bila uhuru na haki, Mantiki hapa ni kuwa huwezi kudai haki na uhuru bila amani, palipo na amani haki na uhuru utawala, baada ya wananchi kupotoshwa na wanasiasa uchwara uanza kujenga hoja za kuonewa na serikali bila kuonyesha ni kwa jinsi gani uonevu huo unatendeka, ndipo gubu ya kisiasa uanzia na amani kupotea.

Mathalani Libya walipotoshwa na wanasiasa wahuni wa Bengazi juu ya serikali ya Kanali Muamar Gaddaff, wakajaa upepo wa gubu la siasa na kuanza kudai uhuru wa kweli, kilichotokea Libya mpaka sasa ni aibu kwa Walibya wenyewe uhuru walioutaka umekuwa shubiri na nchi haikaliki sasa wanasaka amani ya kuishi salama Barani Ulaya, Watawaliwa tunalo jukumu la kupima kila tamko la kisiasa kutoka kwa wanasiasa kwa umakini wa hali ya juu.

Je huo ndio uhuru walioutaka wa Libya au walijazwa upepo na wanasiasa na wao wakajaa “kijua” bila kung’amua ukweli wa mambo, Zinapojengwa hoja na wanasiasa ambao wanataka kutumia amani yetu kama ngao yao ya kupata madaraka ni sharti tupambane nao kwa hoja na tusikubali kujaa upepo na kuwa bwana na bibi wa gubu za kisiasa.

Aidha huwezi ukajenga hoja ya demokrasia na uhuru wa kufanya utakalo bila kuwa na amani kisiasa,Wapo wanaobeza amani nafikri tuwaombee kwa maulana maana walitendalo hawalijui, lakini pia tuwaelimishe umuhimu wa taifa lililostawi kwa amani, Kwahiyo Makala haya yanatambua fika na bayana kuwa wapo wanasiasa wanaobeza amani ya taifa letu kwa kutoa kauli za hovyo za “liwalo na liwe” kauli za namna hii ni za wale wanasiasa wasiojua maana ya amani na wenye kutanguliza umimi kwenye siasa badala ya usisi.

Hata hivyo andiko hili linatambua uwepo wa vibaraka wa kisiasa wanaotumika kuinanga nchi na kuifarakanisha kwa maslahi ya watu wachache, historia ni mwalimu mzuri ukirejea Liberia, Sierraleone, DRC-Kongo, Libya na Niger mataifa yote haya yanaangamia kwa sababu ya wanasiasa vibaraka waliokosa maarifa na hivyo kuhatarisha amani ya nchi zao.

Ukweli upo wazi kuwa makala haya yanapozungumzia dhana ya siasa na amani ni ngumu sana kuwatenganisha watu hawa wawili Nelson Mandela rais wa zamani wa Afrika Kusini na mpigania uhuru wa taifa hilo, na mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Dk. Hussein Mwinyi, Mandela na Mwinyi wanajitambulisha kama viongozi waungwana wanao hubiri dhana ya amani kupitia mlango wa siasa, huu ni ufanano wenye vinasaba vya kisiasa kati ya watu hawa wawili ambao kwao amani kupitia mifumo ya siasa ni ngao na silaha ya ustawi wa watu na mali zao.

Ukirejea historia ya gwiji huyu wa siasa za Kiafrika Mandela amani kwake ilikuwa ndio silaha kubwa kuliko zote ndani ya mifumo ya kisiasa, alitambua bila amani maendeleo ya Afrika ni ubatili mtupu, huwezi kujenga nchi kiuchumi na kisayansi kama taifa lipo kwenye ombwe la amani, Ulimwenguni kote amani ni ufunguo wa maendeleo ya watu na vitu, heshima ya Mandela inayoendelea kuishi kwa nyakati zote katika dunia hii ni kutokana na amani kwake kuwa ndio kitu kikubwa kuliko kingine, kwa ufupi Mandela alikuwa mwanaamani, alihubiri amani kwa vitendo na aliweza kuwa kiongozi imara na shupavu miongoni mwa viongozi wa Kiafrika waliopigania uhuru wa mtu mweusi na kutanguliza falsafa za amani katika ukombozi wa bara letu kutoka mikononi mwa wakoloni.

Kwa nukta hiyo makala haya yanasema hapa Tanzania tumempata Mandela mwingine ambaye ni Dk. Hussein Mwinyi mgombea wa nafasi ya urais kwa upande wa Zanzibar, Mwinyi amani kwake kisiasa ni chaguo la kwanza, kwenye hotuba na mazungummzo yake yote katika kipindi hiki cha shughuli na harakati za uchaguzi amekuwa mwanasiasa tofauti na wanasiasa wengine akijitambulisha kwa kuinadi amani zaidi kuliko kitu kingine, Mwinyi amechagua falsafa ya amani kuongoza mapambano yake kisiasa, Mwinyi anafikri ili tufikie malengo yetu kisiasa na kiuchumi lazima amani itamalaki, hakika hajakosea na historia itamtambulisha kwa vizazi vijavyo.

Ni nadra sana kiongozi kutumia amani kama sera na njia ya kufikia hatua muhimu za kimaendeleo wengi utumia ubabe na vitisho lakini kwa Mwinyi imekuwa tofauti kabisa, Inawezekana wengi wasielewe lakini mantiki ya Mwinyi ni ustawishaji wa nchi iliyotulia inayotoa fursa kwa kila mwananchi na mgeni kufanya shughuli zake za uwajibikaji bila hofu ya aina yoyote, Kisiasa hii ni hoja yenye mashiko zaidi na inayompaisha mwanasiasa kufikia malengo yake anayoyataka, Mandela alipata tuzo ya Nobel kwa sababu ya falsafa zake za amani katika kutatua mikwamo ya kisiasa ndani na nje ya Afrika Kusini, Mandela aliweza kuleta amani na usawa kwa wote licha ya historia ya makaburu kuwabagua watu weusi.

Kwa muktadha huo andiko hili linaamini Mwinyi atafikia malengo yake kisiasa kama ataendelea kuamini na kutumia falsafa za imani katika kuwatumikia watu kisiasa, aidha heshima iliyotukuka aliyoipata Mandela inaweza ikajitokeza pia kwa Dk. Hussein Mwinyi kwa sababu alichokiishi Mandela ndicho anachokiishi kwa sasa Mwinyi.

Kwa mantiki ya uchambuzi huu Unaweza ukaona uwezo wa mwanasiasa huyu kuwa ni kiongozi bora anayetanguliza fikra za utu, upendo na uungwana kama silaha ya kuwaunganisha Wazanzibari kuliko jambo lolote lile akiwa na lengo kuu la kuwaletea maendeleo ya tija kifalsafa, maana bila amani hakuna maendeleo ya kweli katika taifa lolote lile ndani ya dunia hii, pengine tusijue kwenye sayari nyinginezo huko juu Mungu tu ndo anajua.

Kwa Afrika ni mara chache kuwa na watu mithili ya Dk. Hussein Mwinyi wenye fikra na mitizamo ya kisiasa inayojikita kwenye kuhubiri nidhamu ya amani kuliko kitu chochote, viongozi wenye tabia na heshima hii kama wapo hapa Afrika na Tanzania kwa ujumla basi wanahesabika, Tunao ukosefu wa viongozi wenye kariba kama ya Mwinyi kwa sababu ya uwepo wa mfumo wa vyama vingi ambao wanasiasa wengi wanaoshiriki kwenye siasa za kutaka kuishika dola wanasukumwa na tamaa na uchu wa madaraka, Uwepo wa siasa za vyama vingi Afrika umechochea maendeleo kusonga mbele lakini kwa asilimia kubwa baadhi ya vyama vya upinzani vimekuwa mwiba na chachu ya kuwafarakanisha wananchi kwa kile kinachoitwa kunyimwa haki na vyama tawala.

Inawezekana kweli wanaminywa na vyama tawala, je suluhisho la kumaliza tatizo hilo ni nini? Wapo wanasiasa wanaojenga hoja za ili kupata muafaka ni sharti “Pachimbike” wakiwa na maana ni bora kupoteza amani kuliko kuminywa kisiasa, Andiko hili halioni mantiki ya dhana ya kupoteza amani kwa sababu ya madaraka zaidi ya kutafuta muafaka kisiasa juu ya mukwamo wa aina yoyote ile, lakini kwa bahati mbaya wanasiasa wengi tulio nao ni uchawara fikra za namna hii kwao ni adimu sana ni heri shari kuliko maridhiano ya amani kana kwamba wao na koo zao wanaishi kwenye sayari ya Pluto tofauti na dunia, kisiasa huu ni huayawani uliopitiliza.

Kwa nukta hiyo andiko hili likiri wazi kuwa Zanzibar na Wanazanzibari kwa ujumla wake wanaweza kuwa wamepata Mandela mpya atakayewaongoza kwa miiko na maadili ya kuitangaza amani na kuilinda kwa gharama yoyote ile kwasababu anajua umuhimu wa amani, endapo Wazanzibari watampa ridhaa ya kuwa rais wao kwa kipindi cha miaka mitano, hii inatokana na tunachokiona kwa sasa kutoka kwa Dk. Hussein Mwinyi juu ya falsafa zake za kisiasa na amani.dmutungid@yahoo.com

0717-718619
 

Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
17,374
2,000
Hakuna mzanzibari hata mmoja anaweza kumpigia kura mwinyi kibaraka wa tanganyika......

Alafu baba yake amesema anataka mwanae atawale milele......

aendelee kula pensheni ya baba yake zanzibar ni ya wazanzibari na kiongozi wa wazanzibari ni Maalim Seif
 
Aug 31, 2020
31
125
Hii naomba wapinzania hususa Maalim Seif aisome kwa kutulia au asomewe kwa utarabiti ili aelewe Dk. Mwinyi ni mutu ya aina gani wa Wazanzibar maana tunaona kabisa akili yake haijatulia kuelewa hili na wakati hoja za kama hzi zipo ili kumuelewesha

2020-2025 Zanzibar ni zamu ya Dkt MWINYI kuwa Rais wa Zanzibar na yule mzee wa kukosa atambue pia anaenda kukosa tena kama kawaida yake.
 

Reykijaviki

JF-Expert Member
Aug 25, 2020
359
1,000
Hii naomba wapinzania hususa Maalim Seif aisome kwa kutulia au asomewe kwa utarabiti ili aelewe Dk. Mwinyi ni mutu ya aina gani wa Wazanzibar maana tunaona kabisa akili yake haijatulia kuelewa hili na wakati hoja za kama hzi zipo ili kumuelewesha

2020-2025 Zanzibar ni zamu ya Dkt MWINYI kuwa Rais wa Zanzibar na yule mzee wa kukosa atambue pia anaenda kukosa tena kama kawaida yake.
Kumbe wanasiasa waongo huwa wanasema Maalim huwa anaishinda ccm ktk chaguzi zote kisha wanampora! Kumbe huwa anakosa ushindi japokuwa kashinda!!! Duh Dunia haijawahi kuwa na usawa.
 

Falconer

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
821
500
Hheheheheehh, Leo, aliekuwa mgombea uraisi na waziri kiongozi mstaafau wa Zenji, Bw. Nahoda amechukuliwa na usalama wa taifa bara kwa kuwa hampigiii debe hussein. Pili, si wazanzibari tushaema hatumtaki.

Mumeiba majimbo ya ubunge 7 tayari na bado hamushindi. Lilioko ni kuwa mutalazimisha awe raisi . Kwa kura hapati kitu ndio mumeweka siku mbili za kupiga kura kusudi muibe kura zetu.

Hesabu na tathmini tumekwisha fanya. Tunawapiga vizuri sana ndio munatafuta kila kisababu cha kuiba.

Unatumia jina la Mzee Mandela kimakosa kabisa. Mungu akusamehe. Vyenginevo utakosa pumzi ghafla. Kusoma nakala yako ni upuuzi mtupu. Mtu usie na fikira.
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,822
2,000
Mkuu pamoja na kujipinda kote huku na kuleta maelezo marefu sana ktk mada yako. Kwa kifupi sana naweza kutoa ushauri. Mwinyi inampasa akapambane na hali yake tu. Wazanzibari wanamuona tu kama kibaraka kutoka Bara na wala si vinginevyo.
 

Reykijaviki

JF-Expert Member
Aug 25, 2020
359
1,000
Ila Shemsi vai Nahodha yule jamaa ana misimamo unajua hajakubaliana na matokeo alitaka kufanya kama Lowasa kuikimbia Ccm ila naona wamembana,hahahahah mmoja wa mpambe wake alilia machozi Dodoma Mara baada ya uteuzi wa Mwinyi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom