Hivi ni kwanini Mandela baada ya kutoka jela na kuwa Rais wa Afrika Kusini hakulipa kisasi?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,479
30,144
Hebu tujikumbushe kidogo historia

Shujaa wetu wa ukombozi wa Bara hili la Afrika ndiye aliyefungwa miaka mingi jela kuliko mwafrika mwingine yeyote kwa sababu za kisiasa

Mnamo mwaka 1964 alihukumiwa kifungo cha maisha jela na mahakama za enzi hizo za kikaburu, kwa kile kilichoitwa na makaburu hizo za Afrika Kusini kuwa ametenda kosa la uhaini

Hata hivyo baada ya nchi hiyo kutengwa na kuwekewa vikwazo mbalimbali vya kiuchumi, hatimaye Afrika Kusini ikasalimu amri na kumwachia huru shujaa huyo, mnamo mwaka 1990 na akaruhusiwa kugombea Urais wa nchi hiyo katika chaguzi zilizokuwa huru na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo, ikampata Rais was kwanza mwafrika mweusi na akajizolea umaarufu kuliko binadamu yeyote aliyewahi kuishi ndani ya dunia hii katika karne ya 20

Kulitibitisha hilo, sanamu ya Nelson Mandela imekuwa sanamu ya kwanza kabisa duniani, tokea umoja wa mataifa uundwe mwaka 1945 na ndiyo sanamu pekee kuwekwa kwenye makao makuu hayo ya umoja w. wa mataifa, mjini New York

Tukumbuke kuwa mara tu ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Afrika Kusini, Mzee weyu Mandela aliunda Tume ya maridhiano ambapo alisamehe makosa yote aliyofanyiwa na serikali hiyo ya kibaguzi

Nimelazimika kurejea historia ya shujaa wetu huyo wa ukombozi, kwa kuwa hivi sasa nchi yetu, kwa Bahati mbaya sana inapitia kwenye njia hiyo hiyo ya kutengwa na Jumuiya ya kimataifa kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu hapa nchini, kutokana na kiburi cha tuliiowapa idhini ya kutuongoza

Hivi ni mtanzania gani asiyejua kuwa tayari nchi yetu ishaanza kutengwa na kuanza kunyimwa misaada kwa sababu zile zile walizofanyiwa nchi ya Afrika Kusini enzi zile za siasa za ubaguzi??

Hivi kuna sababu gani kwa watawala wetu kumkomoa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini kwa kumweka ndani mahabusu kwa sababu wanazoziita watawala kuwa ni makosa ya jinai, wakati makosa wanayotuhumiwa nayo ni ya kisiasa??

Hivi watawala wetu wanajua kuwa azma yao ya kutaka kuua upinzani nchini ni sawasawa na mtu anayekikimbiza kivuli chake, kwa kuwa kamwe hatakikuta??

Tujitafakari watanzania kubaini njia wanayopita watawala wetu kuwa siyo njia sahihi na ni wajibu wa kila mtanzania, bila kujali itikadi ya kisiasa, kukemea kwa nguvu zote matendo haya yanayofanywa na watawala wetu kabla nchi yetu haijaangamia kabisa
 
hakuweza au hakutaka kulipiza kisasi?

naamini siasani kuna mambo mengi yaliyo nyuma ya pazia na hutokaa uyajue kamwe!
 
Najaribu tu kuimagine, kama huyu kiongozi wetu ndiye angekuwa Mandela, hivi si "angewapoteza" makaburu karibu wote Afrika Kusini??
 
South Africa vile unavyoiona ni kazi ya wazungu, huyu asingefurukuta hata chembe angeshughurikiwa na weusi wenzake wazungu wangekuwa pembeni tu wanagonga cheers.

Je umewahi kujiuliza suicide bombers walianzaje?
 
Hebu tujikumbushe kidogo historia

Shujaa wetu wa ukombozi wa Bara hili la Afrika ndiye aliyefungwa miaka mingi jela kuliko mwafrika mwingine yeyote kwa sababu za kisiasa

Mnamo mwaka 1964 alihukumiwa kifungo cha maisha jela na mahakama za enzi hizo za kikaburu, kwa kile kilichoitwa na makaburu hizo za Afrika Kusini kuwa ametenda kosa la uhaini

Hata hivyo baada ya nchi hiyo kutengwa na kuwekewa vikwazo mbalimbali vya kiuchumi, hatimaye Afrika Kusini ikasalimu amri na kumwachia huru shujaa huyo, mnamo mwaka 1990 na akaruhusiwa kugombea Urais wa nchi hiyo katika chaguzi zilizokuwa huru na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo, ikampata Rais was kwanza mwafrika mweusi na akajizolea umaarufu kuliko binadamu yeyote aliyewahi kuishi ndani ya dunia hii katika karne ya 20

Kulitibitisha hilo, sanamu ya Nelson Mandela imekuwa sanamu ya kwanza kabisa duniani, tokea umoja wa mataifa uundwe mwaka 1945 na ndiyo sanamu pekee kuwekwa kwenye makao makuu hayo ya umoja w. wa mataifa, mjini New York

Tukumbuke kuwa mara tu ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Afrika Kusini, Mzee weyu Mandela aliunda Tume ya maridhiano ambapo alisamehe makosa yote aliyofanyiwa na serikali hiyo ya kibaguzi

Nimelazimika kurejea historia ya shujaa wetu huyo wa ukombozi, kwa kuwa hivi sasa nchi yetu, kwa Bahati mbaya sana inapitia kwenye njia hiyo hiyo ya kutengwa na Jumuiya ya kimataifa kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu hapa nchini, kutokana na kiburi cha tuliiowapa idhini ya kutuongoza

Hivi ni mtanzania gani asiyejua kuwa tayari nchi yetu ishaanza kutengwa na kuanza kunyimwa misaada kwa sababu zile zile walizofanyiwa nchi ya Afrika Kusini enzi zile za siasa za ubaguzi??

Hivi kuna sababu gani kwa watawala wetu kumkomoa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini kwa kumweka ndani mahabusu kwa sababu wanazoziita watawala kuwa ni makosa ya jinai, wakati makosa wanayotuhumiwa nayo ni ya kisiasa??

Hivi watawala wetu wanajua kuwa azma yao ya kutaka kuua upinzani nchini ni sawasawa na mtu anayekikimbiza kivuli chake, kwa kuwa kamwe hatakikuta??

Tujitafakari watanzania kubaini njia wanayopita watawala wetu kuwa siyo njia sahihi na ni wajibu wa kila mtanzania, bila kujali itikadi ya kisiasa, kukemea kwa nguvu zote matendo haya yanayofanywa na watawala wetu kabla nchi yetu haijaangamia kabisa
Mkuu unataka kufananisha Mandela na ndanda kosovo aah wapi ni sawa mbingu na ardhi!
 
Hahaaaaa.......:D:D

Vipi Mkuu Kipara Kipya, kuhusu lile bandiko lako kuwa kila mkijaribu kumvalisha nguo Mfalme lakini yeye anaamua kuzichojoa??
Mkuu usimsumbue mgonjwa.Bado hajakamilisha dozi.Yupo kwenye majaribio.Kuna kipindi dishi lake linanasa chaneli uzuri tu ila muda mwingine ndiyo kama unavyojionea.
 
Bwana wale walimwambia watampa Urais, ila awaache wafanye yao akifanya kinyume wata muua Soft killing
 
Back
Top Bottom