nimesoma pia mkuu.
nitaviweka hapa japo mwaka huu sijasoma kama nilivyojipangia nikiiangalia list ya vitabu,documentaries, biographies nilivyoiandika january 2016 leo naona sijafanya homework yangu vzr lkn mwaka 2017 ni mwaka wa marekebisho.
nitaweka list hapa baadae mkuu...
UPDATES
Nilikuwa na mpango wa kusoma Bibilia yote lakini haukufanikiwa kwa ufanisi nikaishia kusoma baadhi ya sehemu na Mwana 2017 ni fursa ya kujisahihisha ili angalau nimalize hata agano moja Maanaya Maneno yake ni ya kina sana na thamani kubwa kuliko kitu chochote maishani.
1:The Joy of Encouregement
Hapa nimejifunza kuna faida kubwa katika kuwekeza kwenye kuinua watu hasa waliokata tamaa na wenye changamoto. Dunia inapungukiwa na Kutiana Moyo,Upendo na Kujengana kati ya yetu sisi kwa sisi.
2:SECRET TERRORISTS
Hapa Huyu Mdau anazungumzia jinsi ambavyo Vyama vya siri vinavyooperate chini ya Carpet katika kufikia malengo yao. Kile tukionacho sio uhalisia wa mambo wakati wote. Inaelezea Jinsi katiba ya marekani na mataifa mengine yalivyoingiliwa,CRF,na matukio mbali ya kusisimua duniani katika mlengo wa NJAMA/CONSPIRANCY.
3:The BLACK POPE
Hiki kitabu kinaelezea Historia nzima ya Jesuits. Kinaelezea watu wawili wakubwa duniani walioshape historia ya dunia ambao ni MARTIN LUTHER na LOYOLA. Matukio mengi ya duniani enzi hizo na sinsi dunia ilivyoathiliwa na wazo la mtu mmoja Kutokea Hispania baada ya Kujeruhiwa na kushindwa kuwa kamanda wa vita na kuamua kuwekeza katika vita vya fikra. Loyola
4:ECONOMICS FROM BIBLICAL PERSPECTIVE
Hapa uchumi unachambuliwa kwa mlengo wa bibilia na inaonyesha jinsi ambavyo bibilia pia ni source ya kanuni nyingi za kiuchumi kutokea kitabu cha mwanzo.
5:HOW WE GOT TO KNOW SIX INNOVATIONS THAT MADE OUR MODERN WORLD
Hapa inaelezwa jinsi ambavyo, Kioo, Baridi, SAuti,HYGINE, Muda,Mwanga vitu hivi vilivyoibadili taswila ya dunia ya technolojia tangu siku kimojawapo kilipogunduliwa . Mabadiliko haya yamekuwa katika mfumo wa HUMMING BIRD. Yaani Mfano Ugunduzi wa kioo, Kikasababisha Miwani baada ya kugunduliwa printer na watu wengi kuanza kusoma hadi leo kimepelekea kuwa na SELFIE technology wakati kilianza kama kioo cha kujionea. Kupitia kioo Tukapata Darubini Tukaona vijidudu, Tukapata Telescope galileo akaona miezi ikisunguka sayari anga za mbali.
6
EEP WORK
hapa kuna vitu vingi mfano. Mapumziko mtandao, ATTENTION RESIDUE, na vitu vingine vingi ikiwepo mbinu mbalimbali za kuwa focused katikati ya dunia hii iliyobize sana.
7:MAKING IDEAS HAPPEN
Kitabu hiki kinaelezea jinsi ya kufanya mawazo yako yawe katika uhalisia na mbinu mbalimbali ambazo zikiwekwa kwenye uhalisia zinaweza kufanya kutoka mahali ulipokwama.
8:
The Moral Saying of Publius Sylus: A roman slave
Humu anaelezewa kijana mmoja mtumwa aliyenunuliwa kutoka syria lakni hekima,Vipaji na busara zake huko Roma zilimfanya apendwe na kuwa mtu mkubwa katika historia ya enzi hizo. Na misemo na Mithali yake ilikusanywa na kufanywa kitabu.
DOCUMENTARIES
1:THE UNTOLD HISTORY OF ISLAM
Hizi ni series zilizoelezea kuanzia kwa Baba yake Mtume Mohammad SAW, Maisha yake,Kufa kwake, Islamic Calphates chini ya Viongozi wake Abu Bakar, Umar, Uthman, ALi na Kuanguka kwa Dola hilo la kiislam na kuibuka kwa makundi mbalimbali ya kidini ikiwemo Sunni na Shia na mambo yaliyokuwa yakiendelea kipindi hicho.
2:CREATIONISM VS EVOLUTION SERIES
Hapa nilipitia Chanzo cha elimu ya Evolution, Madhaifu yake na Changamoto zake katika ulimwengu wa sasa ukilinganisha na Creation.
3:THE OPERATION PAPERCLIP
hii ni documentary inayoelezea kilele cha vita vya dunia vya pili na jinsi ambavy majasusi,wa Urusi,Marekani na Uingereza walipoingia katk vita vya kuwasaka wanasayansi wa Hitler ili elimu waliokuwa nayo waihamishie kwenye nchi zao. Hii inaelezea nini US walifanya na matokeo yake.
BIOGRAPHIES OF FAMOUS AND INFLUENTIAL PEOPLE
1:Biography of Lee Kuan Yew
2:Biography of Zhao Zhiyang
3:Biography of Narendra Modi
4:Biography of Madam C.J Walker