Umeshawahi panda/endesha gari ya Mkata Kimeo?

Duh kuna siku niko kwenye foleni sambamba na kigari kimoja cha ajabu ajabu nikakiangalia like wtf! Haikupita dakika gari yangu taa ya coolant ikawaka mara mvuke kama wote! Nikapaki pembeni kile kigari kikanipita taratibu nimefungua duka! Kuna water connector ilikuwa ime crack! Aisee kile kigari sasa hivi nikikiona nakiheshimu(tunatumia njia moja)
😂😂😂😂😂 Ki starlet nini?
 
Mwamba alianza nisaliti yeye kwa kunambia gari yake ilikuwa poa haya tungetaka irudisha ulaya inaenda. Kumbe Moro tu hapo inachechemea. Nmefika Moro kiuno kinauma ile mbaya na mafua,kikohozi choka mbaya....alibaki kutengeneza
Safari mlianza saa ngapi na mlifika mda gani?
 
Hii gari ungekuwa na picha ngeipenda sana. Ilikuwa aina gani?
Nakumbuka miaka ya 2003-2004 nilikuwa Shanta Kwenye taxi ya anko wangu aisee hiyo gari ilikuwa kimeo hatari Sana....
Brake fluid ilikuwa inatumika povu la sabuni ya unga..
Bonnet inafungwa na waya,gari haina kibali wala Bima inaendeshwa usiku Tu
 
Duh kuna siku niko kwenye foleni sambamba na kigari kimoja cha ajabu ajabu nikakiangalia like wtf! Haikupita dakika gari yangu taa ya coolant ikawaka mara mvuke kama wote! Nikapaki pembeni kile kigari kikanipita taratibu nimefungua duka! Kuna water connector ilikuwa ime crack! Aisee kile kigari sasa hivi nikikiona nakiheshimu(tunatumia njia moja)
Hahaha kuna siku nimetoka Tabata nakuja Ubungo, kuna watu wana IST mbele wanasua sua nikawapigia horn nyingi na nawawashia taa maana walikua sambamba na roli. waliposogea pembeni niliwaovertake kibati sana, nafika mataa ya External AC ikaanza toa joto, gari inatikisika feni ipo maximum, taa ya coolant inawaka, taa ya overheating ya njano ikawaka dakika 2 mbele ikawa nyekundu, weee.. kwenye bonnet ulitokwa mlipuko sijawah usikia. Nasimama wale wenye IST ndio waliokuja nisukuma nikaweka pembeni pale njiapanda ya Mabibo hostel. water pump ilikua imenifia. aisee nilikonda ndani ya week 1 kupata ile pump.
 
Kuna gari ya mjomba wangu tulikuwa tunapiga safari sheria yake ilikuwa haizimwi mpaka ufike unapoenda, ikigoma kuwaka unaipulizia dawa ya mbu ndio inawaka, kwenye foleni haitakiwi uwashe AC au radio, inakata moto na kuwaka mpaka iamue🤣
Hilo lilikuwa pepo sio gari😅
 
Hahaha kuna siku nimetoka Tabata nakuja Ubungo, kuna watu wana IST mbele wanasua sua nikawapigia horn nyingi na nawawashia taa maana walikua sambamba na roli. waliposogea pembeni niliwaovertake kibati sana, nafika mataa ya External AC ikaanza toa joto, gari inatikisika feni ipo maximum, taa ya coolant inawaka, taa ya overheating ya njano ikawaka dakika 2 mbele ikawa nyekundu, weee.. kwenye bonnet ulitokwa mlipuko sijawah usikia. Nasimama wale wenye IST ndio waliokuja nisukuma nikaweka pembeni pale njiapanda ya Mabibo hostel. water pump ilikua imenifia. aisee nilikonda ndani ya week 1 kupata ile pump.
😂😂😂
 
Nyie jamaa ndo huwa mnaona wenzenu wanaishi barabarabani. So mnawapigia horn wawapishe mna haraka...

Jamaa mmoja wa IST naye alinikuta mitaa flani naendesha gari taratibu napiga hesabu kwenye dimbwi nipite wapi. Akaona namchelewesha. Akaanza piga horn. Hapo gari yangu ni ya kuu kuliko kigari chake kabeba mademu music mkubwa. Nikampisha. Akatangulia.akaenda kumbe sehemu wahuni wamechimba sana dimbw upande wa kulia. Gari ikazama ikazima,maji yaliingia mpaka kwenye engine.

Mi wahuni wakanielekeza nipite wapi. Wakanambia bro huyu jamaa tuachie we nenda tu au kama unataka check movie. Jamaa walimtoa tsh 30,000 kukitoa kigari chale pale. Maji machafu yananuka na ndani yupo na washakji na mademu wakali. Kile kigari kiligoma kabisa kuwaka.
 
Kuna siku nimetoka kupandisha milima ya goba narudi zangu home, nakaribia kabisa home gari ikaanza kuchemsha. Sijawahi kukutana na shida kama ile. Ndo mara ya kwanza. Niliikokota taratibu mpaka home.

Usiku mzima niligeuka fundi, usingizi hauji. Kesho yake nilitakiwa nisafiri nayo. Ikabidi nimuite fundi umeme akagundua kuna sensor inayoregulate cooling imekufa. Nikaifunga nikasafiri muda huohuo.
 
Back
Top Bottom