Umeshawahi panda/endesha gari ya Mkata Kimeo?

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,745
Mwaka 1998 nlipanda gari ya jamaa yangu. Benz akanishawishi sana siku hiyo twende Morogoro na gari yake akaoneshe ndugu zake ana Mercedes Benz.

Hapo kabla nlienda naye ila tulitumia gari yangu. Ile safari siwezi isahau...ilikuwa na kwikwi nyingi na chafya mfululizo gari kila baada ya muda tunakata kimeo.(kufungua bonnet kujaza maji)

Hadi raha ya safari iliisha maana tulikuwa na madumu ya maji kwenye gari na tukifika vijjini tunaenda omba maji. Tulifika Morogoro lakini kwa mbinde sana. Tulifikia hatua tukawa tunapokezana kushuka kujazia maji.yaani ile gari mtu angedhani badala ya petrol inatumia maji.

Leo nmefika sehemu moja nikawaona jamaa wamefungua bonnet Toyota Opa pembeni ya barabara wapo vijana kama 6 hivi wanaangalia kwenye bonnet gari inatoa mvuke ile mbaya.

Gari ilikuwa kama ya kujivukizia Corona. Ingakiwa miaka hii mle ndani tungeweka limao,mwarobaini na tangawizi so ikitembea mwendo flani tunaenda jifukiza.

Umewahi kutana na gari ya namna hii spana mkononi?au ndo ya kutembea na maji muda wote? Gari ya mkata kimeo.
 
Dah huwa sipendi kudrive gari isiyo hata na ac tu achilia mbali kuchemsha. Maana mwanzo mwisho madirisha ni sealed
 
Duh kuna siku niko kwenye foleni sambamba na kigari kimoja cha ajabu ajabu nikakiangalia like wtf! Haikupita dakika gari yangu taa ya coolant ikawaka mara mvuke kama wote!

Nikapaki pembeni kile kigari kikanipita taratibu nimefungua duka! Kuna water connector ilikuwa ime crack! Aisee kile kigari sasa hivi nikikiona nakiheshimu(tunatumia njia moja)
 
Hahah kwahio bora usiichunguze tu ukiwa huna hela
Ukienda Kwa fundi anakupigia hesabu vitu ambavyo unaweza kubadisha inafika laki 5 alafu mfukoni mwako Una buku 3 Tu ebu niambie Kwa style hiyo utakuwa na hamu ya kufanya service??haya Magari sometimes ni vilio Tu...
Unafanya safari ya kwenda morogoro huku mnapita kuomba MUNGU masaa yote Ili gari isiharibike
 
Ukienda Kwa fundi anakupigia hesabu vitu ambavyo unaweza kubadisha inafika laki 5 alafu mfukoni mwako Una buku 3 Tu ebu niambie Kwa style hiyo utakuwa na hamu ya kufanya service??haya Magari sometimes ni vilio Tu...
Unafanya safari ya kwenda morogoro huku mnapita kuomba MUNGU masaa yote Ili gari isiharibike
Hahahahah af gari lenyewe benz bili ingekuja million 2 bora mlijiongeza kubeba vidumu
 
Duh kuna siku niko kwenye foleni sambamba na kigari kimoja cha ajabu ajabu nikakiangalia like wtf! Haikupita dakika gari yangu taa ya coolant ikawaka mara mvuke kama wote! Nikapaki pembeni kile kigari kikanipita taratibu nimefungua duka! Kuna water connector ilikuwa ime crack! Aisee kile kigari sasa hivi nikikiona nakiheshimu(tunatumia njia moja)
Hii kitaalamu tunaita..Umdhaniae ndiye, siye..
 
Back
Top Bottom