umeshawahi kupigana?

mambo zenu.Vipi wenzangu mshawahi kupigana? Ilikuwa lini? Ulipigana na nani? Kwanini ulipigana? Je ulishinda/droo au ulidundwa? Nalog off

Dah, nimewahi mara mbili. yote nilibondwa vibaya mno. magomvi mengi option yangu huwa ni kuota tairi.
 
Dah umenikumbusha mbali sn enzi hizo za std 1&2 kijijin huko,nilikuwa napenda sn haka kamchezo tena nipigane na mtoto wa kiume ila mie ilikuwa ikiwekwa tu mstari dah unakuta mwenzangu anakazana kunipiga mie nakomaa na kaptura mpaka niivue siunajua za kijijin alafu watoto,nikiivua tu mambo hazaran hakuna cha chupi wala nn hapo watazamaji wote wananishangilia tu na nakua mshindi!
Mpaka nikaletewa kesi hm bibi yangu akanitembezea stiki za kutosha ndio nikaacha hiyo tabia lol!
 
Heheheh..
Yeahh nimewahi. Nadhani nlikua na miaka 8 then...na nlipigana na aliekuja kuwa best friend wangu throughout primary school.
Sikumbuki sababu ila nakumbuka tulikua tumetoka shule na nlikua nimevaa ovaroli ya kigauni akashika vile vimikanda akaninyanyua juu.
Inawezekana yeye ndie alieshinda...

Miaka kadhaa baadae sijui kama naweza nilipigana ila kuna kaka yangu sijui alifanya nini nikamkimbiza sana na kumpiga na mawe.
Alafu kaka yangu mwingine yeye hatujawahi kupigana ile kupigana japo kuchokozana kulikuwepo sana ila zamani nilimvuta kwenye ngazi akaanguka na kuvunjika jino. Sasa hivi ni kama ana mwanya vile.
 
Lol, ulianza zamani eeh? No wonder... Hahaha

Back
Top Bottom