Umesha wai Safiri namna hii kwenye Ndege?

hahaa itakuwa ni kule kwa bakongo na hii ni kutok bukavu mpaka mbuyi mayi
 
Hii itakuwa kongo. Inanikumbusha ile ajali ya ndege ya mwaka jana au juzi iliyosababishwa na mamba aliyekuwa akisafirishwa kwenye ndege usafiri wa watu. Mamba sijui alitokajs kwenye kasha lake akajichanganya na wasafiri ikawapatashika mpaka ndege ikaanguka. Loh!
 
Mzee ''mbuzi mzee'' pasipo shaka ni moja ya ndege zinazofanya safari zake DRC, mitaa ya Entebbe-Bunia-Beni, Bunia-Goma-Kisangani, Bukavu-kisangani-Kinshasa. kwa kifupi usafiri wa anga DRC ni hatari zaidi ya unavyoweza kufikiria. kwanza karibu ndege zote zinazofanya safari ndani ya DRC zimechoka hujapata kuona na zinapakia mzigo hakuna kipimo, korido yote huwa imejaa mizigo na mabegi na kama inavyoonekana hapo kwenye picha yako mabegi yanakua juu ya seats, yaan kwa kifupi mzee ni mawazo mno usafiri wa ndege DRC, lakin hakuna jinsi inabidi upande tu hizo ndege zao, maana hakuna barabara DRC kabisa Congo, na kama ni umasikini wa watu DRC imevuka viwango zaidi ya kawaida.
 
Huku kwetu Congo mbona tunasafiri na mbuzi, kuku ,bata n.k kwenye hizi antonovu zetu.

Halafu wamechomea mabomba kwa juu ya kushika kwa abiria wanaosimama.

Huku kwetu usafiri wa ndege ni kama daladala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…